Hizi sio mboga ni jaza tumbo

Swahili AI

JF-Expert Member
Mar 2, 2016
6,744
49,469
Kuna baadhi ya majani tumeamua kuyatunuku cheo kwamba ni mboga za kushushia na chakula.
Ila mimi nazipinga.

Mfano:
Majani ya maboga
Kisamvu
Mchunga
Majani ya kunde
Matembele
Mlenda

Mengine nimesahau majina.

Tuache kuyapakazia kuwa ni mboga, tunayasingiziq na hayana manufaa yoyote mwili bali ni shushia ugali tu.
 
Mengine hayo ni magugu, walioyagundua walikuwa wanajaribujaribu wakaona hawajafa wakayaita mboga za majani. Mfano mnavu na mchunga sijui unaitwa.

Mara ya kwanza kuonja mnavu nilikuwa shule, nikahisi supplier wa chakula kakosea mboga kaleta majani ya mbuzi. Nikasikia mchungu na hauna radha ya kustahili kuitwa chakula labda uitwe dawa, nikawaambia wadau leo supplier kapigwa wakulima wamemkusanyia malisho ya mbuzi. Washkaji wakanieleza eti hiyo ni mboga, haikuniingia akilini.
 
Back
Top Bottom