Hizi kadi nyekundu zinazofutwa ni kielelezo cha jinsi hawa jamaa wanavyobebwa

Cashman

JF-Expert Member
Jun 8, 2018
2,362
4,062
Licha ya kuwa na timu nzuri,mipango mingi ya kimafia nje ya uwanja,na ushindi dhidi ya Simba,bado kumekuwa na kubebwa sana kwa hii timu ya serikali.

Ni kawaida wachezaji wa hii timu huwa na ujasiri wa kukaba kwa jinsi yoyote kwa kutumia maguvu sana.Akiingia vibaya akaanguka mwenyewe, mpinzani ataadhibiwa.Wakikabwa wakanyang'anywa mpira sehemu ya hatari,tegemea utasikia kipenga kwamba mchezaji wa timu pinzani ametumia nguvu kupita kiasi. Hii imekuwa ndiyo kawaida na kwa vyovyote vile watatafuta na kutafutiwa ushindi.

Akiwepo mchezaji kikwazo kwao,atapigwa kadi bila utaratibu.Haya yote yanatokea hasa wanapoona timu imewakazia. Sasa matukio mawili ya kadi nyekundu zisizohalali zinafutwa.Walipaswa kuona aibu sana kwa matukio kama haya.

Nimechoma kichaka tu,kenge wataanza kutoka ni kawaida
 
Tayari wana Pointi 6 za dhuluma.

Pointi 3 waliwapoka Kagera Sugar baada ya goli la Kagera kukataliwa kiubabe.

Pointi 3 wamezipata kwa Coast kupunguzwa na kadi nyekundu kuwadhoofisha ili Uto washinde.

Ligi yetu pia imeshuka ubora Barani Afrika kutokana na matukio kama haya.
 
Iliyofutwa ni straight red card au ni kipi maana huyo mchezaji tayari alishakuwa na kadi ya njano hivyo hata pale angepewa kadi ya njano bado angepaswa kwenda nje.
 
Wakubebwa Fc ni kawaida yao...wakiona maji marefu wanafanyiwa figisu na marefa wao...
 
Yanga ni Tai (Eagle); atabeba mbuzi mmoja mmoja mpaka wote waishe. Kama kuna timu ambayo haijawahi kufungwa na Yanga ijitokeze hapa, timu nyingine zimelambwa jumla ya mabao 7 -2 (ndani na nje)

1714595121782.png
 
Tayari wana Pointi 6 za dhuluma.
Pointi 3 waliwapoka Kagera Sugar baada ya goli la Kagera kukataliwa kiubabe.

Pointi 3 wamezipata kwa Coast kupunguzwa na kadi nyekundu kuwadhoofisha ili Uto washinde.

Ligi yetu pia imeshuka ubora Barani Afrika kutokana na matukio kama haya.
Na wanapoint 06 za Simba baada ya kuwauzia mchezaji mzee kupitia Geita Gold
 
Simba na Yanga wanakuja ofa sana toka KWA marefa. Wote wawili.

Kati ya hao wawili(Simba,Yanga) anayekuwa bora sana msimu husika ni rahisi kuonekana kufaidika zaidi kwasababu akibebwa kidogo tu anakuwa ameshinda

Mchovu wa msimu husika hata akibebwa anakuwa hafaidiki sana inaonekana hajabebwa sana
 
Tuanzie mapinduzi Cup kujadili.... Refa alichezasha dk ngapi vile?...... Mbona huwa hamlalamikii mechi za Simba kuwa yanga kabebwa ila mnalalamikia mechi za timu nyingine?. Kwahiyo kwenye zile point 6 mlizotoa kwa yanga hakuna mechi yanga amebebwa?. Vipi ile mechi na mashuja mliyopewa penalty au umesahau?.
 
Back
Top Bottom