Hivi ni kweli TPDC wanasambaza LPG? Au kuna makosa katika uandishi?

inayosambazwa ni CNG yaani Compressed Natural Gas.

Liquefied Natural Gas inataka mitambo maalumu kuchakata CNG kuwa LNG.

Sio kweli kuwa hatuna petroli ( mafuta ghafi yaani crude oil) kwenye visima vyetu vya gesi asili,mimi nimeshuhudia huko South East Asia kukiwa na crude oil pammoja na gesi asilia kwenye kisima kimoja yote yanachimbwa .

Wakati mwingine mazao ya petroli yanaweza yakawa kidogo mno si economical viable. Wakati mwingine ikaamua kuyaacha huko chini ya ardhi ikachimba gesi asilia au mazao ya gesi asilia yakiwa kidogo huchomwa kama mwenge wa uhuru,na kuchimba crude oil.

Visima hivyo vina mchanganyiko wa maji,crude oil,na gesi asilia,kwa kupitia michujo you will end up with crude oil plus natural gas and other traces etc etc..
 
Nilivyowahi kusikia toka TPDC gesi ya LPG inaagizwa toka nje ya nchi, labda wameibadili na kuwa LPG.
 
inayosambazwa ni CNG yaani Compressed Natural Gas.
Liquefied Natural Gas inataka mitambo maalumu kuchakata CNG kuwa LNG.
Sio kweli kuwa hatuna petroli ( mafuta ghafi yaani crude oil) kwenye visima vyetu vya gesi asili,mimi nimeshuhudia huko South East Asia kukiwa na crude oil pammoja na gesi asilia kwenye kisima kimoja yote yanachimbwa .
Wakati mwingine mazao ya petroli yanaweza yakawa kidogo mno si economical viable. Wakati mwingine ikaamua kuyaacha huko chini ya ardhi ikachimba gesi asilia au mazao ya gesi asilia yakiwa kidogo huchomwa kama mwenge wa uhuru,na kuchimba crude oil.
Visima hivyo vina mchanganyiko wa maji,crude oil,na gesi asilia,kwa kupitia michujo you will end up with crude oil plus natural gas and other traces etc etc..
Gas inayosambazwa majumbani ni PNG.
 
Swali ni je hayo mabomba ni kwaajili ya LPG au PNG?
Hawawezi kuelewa mkuu,ukiwafafanulia kwanza,waelewe Piped Natural Gas,liquefied Natural gas,compressed natural gas,liquefied petroleum gas ,hivyo ni vitu gani kwanza,Maana inaonesha hadi baadhi ya watoa maamuzi pia hawajui
 
Ni changamoto kubwa sana.
 
CNG huwezi kupikia mkuu.
Mkuu nachojua gesi inayosambazwa kupitia mabomba ya TPDC ni compressed Natural Gas, ndio hiyo inatumiwa na viwanda,magari,mitambo ya kufua umeme na matumizi ya majiko ya nyumbani,swali langu kama unasema CNG haiwezi kupika kwanini TPDC imewafungia hadi nyumba za vigogo hao?Kwa matumizi yapi?
Tatizo ni nini?
 
Mtujuze vzr mnaojua maswala ya gesi.Nini tofauti ya LPG,LNG na PNG ili tuende pamoja
LPG kirefu chake ni liquified Petroleum Gas au gesi za petroli zilizo katika hali ya kimiminika kwa kiswahili. LPG imeundwa kwa kiwango kikubwa cha kekimikali za propane na butane ambazo ndizo zinaitwa petroleum gas au gesi za petroli.
Unatumia mgandamizo (pressure) ndogo sana kuzibadili gesi za petroli (petroleum gas) kuwa kimiminika na kuzijaza kwenye mtungi.
Kwa kutumia huo mgandamizo mdogo unaweza kujaza kiwango kikubwa cha LPG kwenye mtungi ambacho kinaweza kutosha kwa kupikia.

LNG kirefu chake ni Liquified Natural Gas au gesi asilia iliyo katika kimiminika kwa kiswahili. LNG imeundwa kiwango kikubwa cha kemikali ya methane.
LNG inapatikana kwa kuipoza Natural gas (gesi asilia) kwenye joto la nyuzi joto -162 centigrade.
Yaani chukulia unapoza kitu kwenye joto la barafu mara 162.
Sababu za kuibadili gesi asilia kuwa LNG ni ili kurahisisha usafirishaji kwenda masoko ya mbali lakini ili kuitumia inabidi ibadilishwe tena kuwa gesi asilia.

PNG kirefu chake ni piped natural gas au gesi iliyo kwenye bomba kwa kiswahili.
Ili kupikia gesi asilia majumbani ni lazima utumie bomba litakalo kusambazia hiyo gesi mpaka jikoni kwako kama tunavyo fanya kwenye maji.
 
Back
Top Bottom