Hivi ni kwanini jua linapochomoza na linapokaribia kuzama sio kali sana kama linavyokuwa muda wa mchana?

Aisee kuna watu hawakq serious kama yule aliyesema jua linatua kwenye mapembe ya shetani sijui aliitoa wapi idea hii ya kipumbavu
Screenshot_20240427-115310_Google.jpg
 
Mfano ni toch inavyokumilka, chukua mpo watu wawili umbali wa mita 100 then toch imlenge mmoja, obviously mtu wa pili ambaye hajalengwa (pembeni) ataona mwanga hafifu (joto) tofauti na aliyemulikwa centre.
Umejibu vyema.

Mwambie pia kuna sehemu huwa hawana jua la katikati linapita pembeni kulee. Pia hawana jua la masaa 12 yaweza kuwa saa 8 tu linapotea.
 
Jua linapochomoza au linapokaribia kuzama, nuru yake inapitia katika tabaka kubwa zaidi la angahewa kuliko wakati wa mchana.

Wakati wa mchana, nuru ya jua inapita katika tabaka la chini zaidi la angahewa, ambalo linasababisha nuru yake kupunguzwa kwa kiasi kikubwa zaidi.

Tabaka hili la chini la angahewa linasababisha nuru ya jua kugongana na chembe ndogo za vumbi na molekuli za hewa, hivyo kufanya nuru iwe kali zaidi na kusababisha anga kuonekana kuwa bluu.

Lakini wakati jua linapochomoza au linapokaribia kuzama, nuru yake inapita kwenye tabaka kubwa zaidi la angahewa. Kwa kuwa nuru inapitia umbali mrefu zaidi katika angahewa, chembe za vumbi na molekuli za hewa zina nafasi zaidi ya kuyatawanya mwanga mwekundu na rangi nyingine zenye mawimbi marefu.

Hii husababisha jua kuonekana kuwa na rangi ya machungwa au nyekundu, na pia kufanya nuru yake isiwe kali sana ukilinganisha na wakati wa mchana.
Dah! Umenikumbusha mambo ya rayleigh scattering kwenye course ya hydrometeorology. Umeeleza vyema sana.
 
Ikiwa miale ya point a,hufika duniani ikiwa dhaifu zaidi kutokana na umbali zaidi mpaka kusababisha barafu wakati mwingi eneo hilo,basi hata point C niliyoweka alama inaathirika kwa mtindo ule ule wakati jua litakapokuwa limesogea kuzunguka upande wa nyuma.
Tofauti ya C na A ni kwamba c inakuwa na vipindi vyote kwa masaa 24 tu,ila a haifikiwa na miale jua sawa sawa zaidi ya mwanga hafifu tu.

Labda swali gumu ni kujiuliza kwanini huwa linaonekana ni kubwa zaidi.View attachment 2975139

Physical Geography Advance.

Hapo majibu ni mawili tuu.
Ni length of Insolation
Distance between Earth and Sun
 
Jua linapochomoza au linapokaribia kuzama, nuru yake inapitia katika tabaka kubwa zaidi la angahewa kuliko wakati wa mchana.

Wakati wa mchana, nuru ya jua inapita katika tabaka la chini zaidi la angahewa, ambalo linasababisha nuru yake kupunguzwa kwa kiasi kikubwa zaidi.

Tabaka hili la chini la angahewa linasababisha nuru ya jua kugongana na chembe ndogo za vumbi na molekuli za hewa, hivyo kufanya nuru iwe kali zaidi na kusababisha anga kuonekana kuwa bluu.

Lakini wakati jua linapochomoza au linapokaribia kuzama, nuru yake inapita kwenye tabaka kubwa zaidi la angahewa. Kwa kuwa nuru inapitia umbali mrefu zaidi katika angahewa, chembe za vumbi na molekuli za hewa zina nafasi zaidi ya kuyatawanya mwanga mwekundu na rangi nyingine zenye mawimbi marefu.

Hii husababisha jua kuonekana kuwa na rangi ya machungwa au nyekundu, na pia kufanya nuru yake isiwe kali sana ukilinganisha na wakati wa mchana.
Sio kweli kama mtaalamu
Hujajibu swali.
0.5/10
Umeelezea concept ya usiku na mchana. Sio intensity of Sunrays during the day time.
 
Nauliza tu wakati wa kipindi cha mvua jua huwa linazuiwa na kitu gani?
Ni very simple kufahamu. Kuna aina za mawingu na sifa zake. Lakini pia kiasi cha humidity huweza kupunguza miale ya jua hado 60%. Dust on atmosphere, quantity of water vapour.nk Lakini hali hii haifany joto kupotea. Dunia ikipoteza joto lake kwa dk 3 hakuna maisha katika dunia.
 
Ikupe kufahamu kuwa, Dunia haizunguki, ila jua na mwezi huzunguka kufanya movement.

Shule zimewajaza matango pori,

BIBLIA ilishasema wazi, jua na mwezi huzunguka.
Imani ni shambulio la akili.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom