Hivi ni kwanini jua linapochomoza na linapokaribia kuzama sio kali sana kama linavyokuwa muda wa mchana?

Hivi ni kwanini jua linapochomoza na linapokaribia kuzama sio Kali sana kama linavyokuwa muda wa mchana?

Wajuzi karibuni.

Asante sana.
Jua linapochomoza au linapokaribia kuzama, nuru yake inapitia katika tabaka kubwa zaidi la angahewa kuliko wakati wa mchana.

Wakati wa mchana, nuru ya jua inapita katika tabaka la chini zaidi la angahewa, ambalo linasababisha nuru yake kupunguzwa kwa kiasi kikubwa zaidi.

Tabaka hili la chini la angahewa linasababisha nuru ya jua kugongana na chembe ndogo za vumbi na molekuli za hewa, hivyo kufanya nuru iwe kali zaidi na kusababisha anga kuonekana kuwa bluu.

Lakini wakati jua linapochomoza au linapokaribia kuzama, nuru yake inapita kwenye tabaka kubwa zaidi la angahewa. Kwa kuwa nuru inapitia umbali mrefu zaidi katika angahewa, chembe za vumbi na molekuli za hewa zina nafasi zaidi ya kuyatawanya mwanga mwekundu na rangi nyingine zenye mawimbi marefu.

Hii husababisha jua kuonekana kuwa na rangi ya machungwa au nyekundu, na pia kufanya nuru yake isiwe kali sana ukilinganisha na wakati wa mchana.
 
Ukubwa wa jua haubadiliki
Joto la jua huwa haibadiliki
Ila
Jua katika mida ya saa 6 hadi 7,miale ya mwanga wa jua huwa inagonga perpendicular na atmosphere, inapenya kwa wingi ,joto huwa kali na jua huonekana dogo

Lakini jioni, Jua huwa kama lipo chini (Magharibi),kwahyo miale ya mwanga huwa inagonga katika angle kubwa na kufanya mingi ipotelee nje ya atmosphere/Tabaka la hewa

Miale inayofanikiwa kupenya ni michache kuliko mchana
Kwahyo joto huwa dogo na kuzagaa kwa miale hufanya Jua huonekana kubwa.
 
Hivi ni kwanini jua linapochomoza na linapokaribia kuzama sio Kali sana kama linavyokuwa muda wa mchana?

Wajuzi karibuni.

Asante sana.
Bujibuji mimi si msomi ila nina akili ambazo walioenda shule wengi hawana.
Kuna nadharia zangu mwenyewe naziamini kuliko za wana sayansi.

Naamini kwamba dunia siyo round kama mpira wa miguu ⚽ bali una umbo la mpira wa rugby.🏉

So jua linapochomoza hujikuta dunia kwenye ncha mchongoko. Hivyo halisi kali kwasababu mionzi yake inasafiri umbali mrefu zaidi hadi kufikia dunia.

Mchana dunia inakuwa imejizungusha hadi kwenye peak yake, ambapo ☀️ jua hufikia kwenye uso wa dunia ndani ya muda mfupi sana.

Jioni inakuwa kama ilivyokuwa asubuhi
 
Bujibuji mimi si msomi ila nina akili ambazo walioenda shule wengi hawana.
Kuna nadharia zangu mwenyewe naziamini kuliko za wana sayansi.

Naamini kwamba dunia siyo round kama mpira wa miguu ⚽ bali una umbo la mpira wa rugby.🏉

So jua linapochomoza hujikuta dunia kwenye ncha mchongoko. Hivyo halisi kali kwasababu mionzi yake inasafiri umbali mrefu zaidi hadi kufikia dunia.

Mchana dunia inakuwa imejizungusha hadi kwenye peak yake, ambapo ☀️ jua hufikia kwenye uso wa dunia ndani ya muda mfupi sana.

Jioni inakuwa kama ilivyokuwa asubuhi
1.So huko kwenye ncha mchongoko hakuna bara ?
2.Je,zile nchi za baridi kali, zipo upande upi wa huo mpira
3.Je,Jua ndiyo lazunguka ama dunia ?
4.Je,mwanga hata ukipiga kwenye mchongoko si bado limepiga kwenye dunia tu ,hiyo mda mrefu inakuwaje sasa.
5.Je,mwanga hutumia mda gani kufika duniani
6.Mbona hiyo shepu yako ya Rugby,haionekani kwenye Solar Eclipse
7.Kwenye Ramani ya dunia, huo mchongoko upo upande gani...?
8.Je,kwa nadharia yako kila ncha ya dunia inapata mwanga wa dunia kwa Idadi sawa ya siku
9.Je,kwenye kwenye miezi ambayo jua uwahi kuchomoza na kuchelewa kuzama, mzunguko wake ukoje...
10.Je.Katika solar system, sayari zote ni za mviringo ila dunia tu ndiyo umbo la rugby ?
11.Una ushahidi hata mitano ya ku-support nadharia hii...

12.Kwa nchi za Scandinavia,Kanada Kaskazini na Siberia, ambapo jua hujitokeza kipindi cha miezi sita tu kwa mwaka ,Kwenye huo mpira wako wa rugby ,hii imekaaje...?

13.Dira zote huelekea Kaskazini, Je ,kwenye rugby yako Kaskazini ni wapi...?


14.Halafu utujuze kwanini Genius kama wewe upo nchini na nchi haijui, itabidi tukujengee sanamu na kukupa ulinzi maalum....
 
Jawabu - ni Angle formation kati ya Jua na location husika ya Dunia.

Wakati wa Jua kuchomoza - kuna kuwa na narrow angle formation hii upelekea miale ya Jua kufika sehemu husika kwa asilimia ndogo.

Wakati wa mchana - kuna kuwa 90° degree angle formation, ndio maana tunaliita jua la utosi.

Wakati wa Jioni - pia kuna kuwa na narrow angle formation, the same to sunrise.

NOTE: Ukitaka kuelewa vizuri, cheza vizuri na kivuli chako katika nyakati zote (asubuhi, mchana na jioni), utaelewa hii scenario inavyoenda.
 
Hivi ni kwanini jua linapochomoza na linapokaribia kuzama sio Kali sana kama linavyokuwa muda wa mchana?

Wajuzi karibuni.

Asante sana.
Jua kali maana yake ni joto la uso wa dunia kuwa kali. Kwa sababu jua halibadiliki joto lake, bali ni uso wa dunia.

Hii inatokana na angle kati ya uso wa dunia na jua.

Dunia inazunguka mhimili wake mara moja katika masaa 24. Angle kati ya dunia na jua hubadilika kadri muda unavyosogea. Dunia inakuwa mbali zaidi na jua katika siku moja baada ya masaa 12.

Umbali wa dunia na jua huathiri joto la uso wa dunia kutokana na mavumbi kati ya dunia na jua na angle of incidence ya miale ya jua na uso wa dunia.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom