Rweyemam105
Member
- Sep 8, 2012
- 33
- 54
Hallo wana JF.
Nimekuja na hoja binafsi, Kwanini sasa hivi kumeibuka wimbi la wanaojiita wachungaji, pale wanapofanya maombi either kwa njia ya hadhara au kwenye TV au Radio na mitandao ya Jamii, hutanguliza mbele Sadaka ili waweze kukuombea matatizo yako!?
Naomba nitoe mfano ili niweze kueleweka vizuri mada yangu ninayoileta hapa JF.
Majuzi kati nilikuwa zangu pande za Moshi, wakati nimejipumzisha usiku, nikawa nimefungulia Radio moja pendwa pande za Moshi, kukawa na kipindi cha mahubiri. Mchungaji akawa anahubiri kwa mbwembwe huku akitabiria wale wanaopiga simu na wengine wakiwa wanalipuka Mapepo kwenye Radio, baadae wanajifanya wameponywa kwa maombezi hayo kupitia simu. Binafsi yangu nilipojaribu kupiga simu, namba zake zote nne alizotoa, hazikuwa zinapatakana zaidi ya kusema "Simu unayopiga inatumika kwa sasa" hata pale ambapo hakuwa anaongea na mtu online/live kwenye radio, simu zote zilikuwa Busy.
Cha ajabu na kushangaza akawa anahimiza watu waendelee kupiga simu au kutuma ujumbe "Yesu Nitendee Muujiza"
Baada ya kuona namba zote hazipatikani, nikajitosa kwa maelekezo kwamba utume ujumbe wa sms "Yesu nitendee Muujiza" baada ya kipindi kuisha saa sita na nusu usiku, nikapokea sms inayonitaka kutoa kwanza Sadaka ili niweze kuombewa na kutabiriwa Maisha yangu.
Najaribu kujiuliza, ni wajinga wangapi wanaoingia kwenye hii mitego ya hawa wachungaji ambao wako kimaslahi yao binafsi.!? Mchungaji badala ya kusaidia waumini walio na shida, wewe ndio unakuwa wa kwanza kuwakandamiza kwa kuwakamua Sadaka ya kujimaliza, yaani unatoa hadi sent ya mwisho ili Mungu aweze kukutendea Miugiza, huku, huyo mchungaji akiwa na shida ya Makazi au usafiri, waumini ndio wanachangishwa harambee ili kufanikisha hitajio la Mchungaji. Ikifikia Zamu yako, umepatwa na dhahama ya kukosa RENT au Ada ya watoto shuleni, uongozi wa Kanisa unaitwa kwa ajili ya kuwaombea maombi na miugiza. Huku sadaka na ZAKA, fungu la kumi, sadaka za shukrani zikienda kujenga miradi kama Shule/hotel/hospital binafsi ya Kiongozi wa huduma(Pastor/Muonaji wa Sadaka zenu).
Kweli waumini waliowengi tutafika mbinguni tumechoka na viboko juu kwa kukosa maarifa. Na wala hakuna atakaye kusikiliza utetezi wako kuwa sikujua kama yule Pastor alikuwa Mchumia tumbo.
Ni wasaa umefika, serikali kuangazia ktk haya Makanisa na huduma ambazo ziko kimkakati wa kujinufaisha wao kama kikundi/genge huku waumini wakibakia maskini, wavivu wa kufanyakazi huku wakiaminishwa kuwa watakuwa matajiri pale watakapo ambatana na huduma zao.
NB: Watanzania tuamke. Ni kazi pamoja na bidii ndio itakayo kukwamua katika hali ngumu unayopita. Usisubirie Muugiza popote pale. Miugiza ingekuwepo, usingeitishwa kwenda kwenye harambee ya kuchangisha pesa ya kumnunulia Pastor usafiri au kumjjengea makazi, huku wewe/mimi tukikimbizana kumkwepa Mama mwenye nyumba.
Sifundishi watu kuwa makaidi kutokutoa sadaka, La hasha. Ila pale unapohitajika kufanya hivyo, basi uwe umeongozwa na Roho wa Mungu na wala sio mihemko ya Pastor wako ambaye mkishaachana hapo kanisani, anapopaita madhabahu, dakika mbili tatu, Sadaka yako inapeleka watoto wake KFC, Shule Ulaya/Feza schools.
Wenye mtazamo mdogo, wataona kuwa ninawaonea Wachungaji wivu. Ila ukweli siku zote ni mchungu, na utabakia kuwa ukweli daima.