Hili ndilo kosa kubwa alilofanya Warioba. CCM na Serikali walitaka afanye kama Mwakyembe!

Tulimumu

JF-Expert Member
Mar 11, 2013
14,308
12,972
Jaji Joseph Sinde Warioba, amekuwa adui namba moja wa rais, viongozi wa CCM na serikali kutokana na tume aliyoingoza ya kukusanya maoni ya wananchi kuhusu katiba mpya kuleta maoni halisi na ya kweli kama yalivyopendekezwa na kutolewa na wananchi kuhusu muundo wa muungano ambapo mapendekezo ya wananchi waliowengi ni kuwa ili kuwa na muungano wa haki ni lazima tuwe na serikali tatu, ya Zanzibar, Tanganyika na ya Muungano. Mapendekezo hayo yaliyotolewa na wananchi kupitia tume ya rais ya kukusanya maoni ya katiba mpya chini ya jaji Warioba yamemuudhi rais, viongozi wa CCM na serikali wanataka mfumo uliopo wa serikali mbili uendelee. Baada ya rais kufungulia mvua ya lawama, kejeli na vijembe dhidi ya Warioba imekuwa kama ni ruksa kamili kwa viongozi wa CCM na serikali sasa kumtukana, kumshutumu na kumjeli kwa kuleta maoni ya wananchi kama yalivyo. CCM ikaanza ziara nchi nzima kupitai katibu wake mkuu Kinena kumshutumu Warioba, serikali ikaandaa makongamano na kuwatumia baadhi ya wasomi wenye njaa kumnanga Warioba na hata katika kongamano mojawapo lililoandaliwa na serikali tumesikia baadhi ya wachangiaji walioandaliwa kuvurumisha matusi kwa Warioba wakisema ameleta mapendekezo ya serikali tatu kwakuwa yeye muda wake wa kuishi umeisha! Kwenye bunge la katiba nako kila mchangiaji mwenye mlengo wa CCM aliposimama adui yake namba moja amekuwa Warioba. Mawaziri nao wamekuwa ndio makamanda wa kuongoza mashambulizi wakiongozwa na Lukuvi. Kikubwa ni kuwa Warioba amekuwa adui namba moja wa chama tawala na serikali iliyopo madarakani na anashambuliwa yeye binafsi kana kwamba hiyo kazi aliifanya peke yake na hakutumwa na rais. Ashukuru Mungu yale mambo yaliyowakuta akina Ulimboka na Kibanda yalijulikana na wahusika walinusurika vinginevyo na yeye si ajabu angekutwa Mabwe pande.

NI KOSA GANI KUBWA ALILOFANYA WARIOBA? Kosa kubwa alilofanya Warioba na tume aliyoingoza ni kuleta maoni na mapendekezo ya wananchi kama walivyotaka walivyotaka wananchi wenyewe. Kwa ufupi ni kwamba kosa ambalo linamgharimu sasa ni kutoa na kuusema ukweli mtupu. Warioba ameiita koleo kuwa ni koleo na hajasema kijiko kama walivyotaka CCM na serikali. Warioba na tume aliyoingoza hawakutaka kuchakachua maoni na mapendekezo ya wananchi.

CCM NA SERIKALI WALITAKA WARIOBA AFANYE KAMA ALIVYOFANYA MWAKYEMBE KWENYE RICHMOND. Kwakuwa CCM na seikali wanataka serikali 2 na kuwa hiyo ndiyo sera ya chama kilichopo madarakani, walitaka Warioba achakachue maoni ya wananchi, yaani atoe rasimu yenye mapendekezo kinyume na yale waliyoyatoa wananchi kuhusu muundo wa muungano wa serikali tatu. CCM na serikali walitaka Warioba afiche ukweli kama alivyofanya Dk Harrison Mwakyembe ambaye aliongoza tume ya kuchunguza kashfa ya Richmond ambapo baada ya kuupata ukweli wakautoa nusu kadiri ya matakwa ya serikali na kumbebesha mzigo wote wa kashfa ile Edward Lowassa ambaye alijiuzulu uwaziri mkuu pamoja na mawaziri wawili. Wakati mjadala wa ripoti ya Richmond ulipopamba moto huku Lowassa akijitetea kuwa hakupewa nafasi ya kujitetea aliinuka Mwakyembe na kusema kama watu hawaridhiki waombe kanuni zivunjwe ili wawasilishe upya taarifa yao ambapo watatoa hata siri walizozificha ili kuiokoa serikali isiporomoke yote. Kufikia hapo wenye akili tukajua taarifa ya tume yote kuwa ni sifuri. Kumbe walificha siri ambazo zilisababisha aliyepaswa kuwajibishwa abaki madarakani na ambaye hakuwa na hatia ndiye awajibike. Pamoja na kuficha siri hata mapendekezo yote au maazimio yaliyotolewa na bunge kutokana na ripoti nusu ya Richmond hayakutekelezwa kwakuwa aliyepaswa kuyatekeleza ndiye aliyepaswa kuwajibishwa. Hivyo waliopaswa kuchukuliwa hatua kwa mujibu wa taarifa nusu ya Richmond wakaachwa mpaka wastaafu na kujichotea mafao yao ya kustaafu. Ni jambo la ajabu kuwa bunge liliendelea kujadili ripoti ambayo ilikuwa haikukamilika kwa maana ya kuwa imeondolewa mambo muhimu kuhusiana na kashfa husika. Mwishoni tukashuhudia spika wa bunge Samweli Sitta anayejidai na wa viwango na spidi akiufunga mjadala wa Richmond kihuni kabisa.

Baada ya hapo Mwakyembe na Sitta wakaunda kamtandao kalikojiita ni ka wapambanaji wa ufisadi. Walipoonekana wanaelekea kuwa tishio kwa utawala na hatimaye wangetoa siri walizozificha kwakuwa walikuwa wameshaunda chama cha CCJ kwa siri, serikali ikaamua kuwapa vyeo ili watulie. Ndipo tukashuhudia Mwakyembe akipewa unaibu waziri wa Ujenzi na hatimaye waziri kamili wa uchukuzi. Sitta yeye akaundiwa wizara ambayo haina tija yoyote na hakuna maana ya yenyewe kuwepo maana ingekuwa ni idara au kurugenzi tu ndani ya wizara ya mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa. Akaundiwa wizara ya ushirikiano wa Afrika mashariki. Mwanamama anayejiita injinia Stella Manyaya yeye akapewa ubunge wa viti maalu na kisha akaongezewa na ukuu wa mkoa wa Rukwa. Lucas Selelii yeye alinyimwa hata kugombea ubunge kupitia CCM pamoja na kuwa aliongoza kwenye kura za maoni kwa maelezo kuwa hana mvuto. Haijulikani kama alipingana na wenzake kuhusu kuficha siri au ilikuwaje. Naye yuko kimya kama Aboud Jumbe aliyefungiwa kigamboni kwa "kosa" la kutaka serikali tatu. Hivyo hadithi ya Richmond ikaishia hapo ingawa sasa hivi tunalipa fidia kwa kuvunja mkataba. Haya yote ni kutokana na Mwakyembe na Sitta kuuficha ukweli kwa tamaa ya madaraka na pesa. Jambo la ajabu Mwakyembe huyu huyu mnafiki ndiye anayejifanya kutamba bungeni kuwa yeye ni msomi na kuwadharau wenzake. Anajifanya yeye ndio msomi na kuwakandia wenzake wakati ndiye aliyetuingiza katika matatizo makubwa kiuchumi kwa kuficha ukweli. Sasa hivi wananchi tunaumia kwa kulipa mabilioni kama fidia.

Nichukue nafasi hii kumwambia Warioba kuwa hana budi kupokea matusi, kejeli na dharau kwa furaha kubwa kwani ameushinda unafiki kwa kutoa ukweli. Ni msomi aliyeelewa kuwa ukweli huwa haufunikwi na huwa haupotei moja kwa moja. Mungu ambariki sana na historia itamkumbuka kama mwanamwema aliyeuweka ukweli hadharani licha ya kuwa yeye mwenyewe ni muumini wa serikali 2. Waovu nao wakae wakijua kuwa Historia ni mwalimu mzuri sana. Kama yasiposemwa leo wakiwa hai, yatasemwa wakiwa kaburini na juu ya makaburi yao na kukiabisha kizazi chao watakachokiacha.WALAANIWE WOTE WANAOUBEZA UKWELI NA WANAOTAKA KULETA CHOKO CHOKO ZA KIKABILA, KIDINI, KIKANDA NA KIJESHI KWASABABU TU YA TAMAA YAO YA MADARAKA NA KUUKANA UKWELI. TOKA LINI MUUNGANO UKALINDWA NA JESHI. MUUNGANO NI SUALA LA MARIDHIANO KAMA ILIVYO NDOA. HUWEZI KUMLAZIMISHA MTU KUOA AU KUOLEWA NA MTU ASIYE MPENDA HALAFU UKAIITA HIYO NI NDOA. HATA HILO JESHI LENYEWE MNALOTAKA KULITUMIA KULAZIMISHA NA KUTISHA WANANCHI LITACHOKA KWANI WANAJESHI NI RAIA WA NCHI HII NA WAO WANAMTIZAMO NA MAONI YAO BINAFSI KUHUSU MUUNGANO NA WALITOA MAONI YAO. UKWELI MCHUNGU NI KUWA NDANI YA JESHI KUNA WANAJESHI WANAOTAKA SERIKALI 1, 2 NA 3. SASA IKITOKEA WANAOTAKA 1 AU 3 WAKO WENGI WATAULINDAJE MUUNGANO WA SERIKALI 2? Tatizo la viongozi wa serikali huwa wanafikiri wanapowatumia polisi na jeshi kuwa wao hawana hisia au uchungu. Wakati mwingine polisi na wanajeshi mnaowatumia kukandamiza raia huwa wanafanya mnayoyataka huku wakiwa na uchungu kama binadamu. Si kweli kuwa wanafurahia kupiga na kutesa watu. Wanafanya hivyo kwakuwa ndio utaratibu wa kazi yao kutii kwanza. Siku wakichoka watawageukia na kuwapigisha magoti ninyi wenyewe. Hapo ndipo itakuwa kilio na kusaga meno. Ole wenu siku hiyo ikifika.
 
Bravo! Kweli JF ni jukwaa la Ma- "Great Thinkers" pamoja na kwamba kuna wachangiaji wengine wana Itikadi Kali!
 
Mtoa mada safi sana. Sisi tunaopenda Amani tumwombee Mzee na tumwombe Mungu awape nafasi wazalendo kama Warioba ili waibadilishe Nchi
 
Hakuna Mzalendo wa kweli kama Warioba hapa Tanzania kwa kipindi hiki kama watatokea basi ni baadaye sana, CCM hawaweziu kufikiri , maana Warioba amewambia wazi kuwa msimamo wake yeye kama Warioba ni Serikali mbili lakini akaamua kuweka msimamo wake pembeni na kuwasilisha maoni ya wananchi walio wengi
 
Ningependa kuuliza swali moja kwa watanzania wenzangu wasiopendelea itikadi wala mlengo wowote. Hivi ni kwanini tume zote zinazoundwa tanzania zikiwakilisha ripoti zao kwa watawala huwa hawataki kuzikubali hasa zinapokuwa zimegusa masuala ya muungano?
Mfano: 01: Tume ya jaji nyalali
02: Tume ya jaji kisanga
03: Tume ya jai warioba
 
Warioba alikuwa anawakilisha mawazo ya shetani kwenye katiba mpya. Bahati nzuri Mungu yu pamoja nasi
 
Ningependa kuuliza swali moja kwa watanzania wenzangu wasiopendelea itikadi wala mlengo wowote. Hivi ni kwanini tume zote zinazoundwa tanzania zikiwakilisha ripoti zao kwa watawala huwa hawataki kuzikubali hasa zinapokuwa zimegusa masuala ya muungano?
Mfano: 01: Tume ya jaji nyalali
02: Tume ya jaji kisanga
03: Tume ya jai warioba
Ni kwa vile mawazo ya tume hiyo yanawakilisha fikra za kishetani
 
UMENENA VEMA. Ombi kwa serikali ya Tanzania. Next time wakitaka kuweka maslahi yao mbele na wasipotaka ukweli wamchague (sorry to mention!) Lukuvi awe mwenyekiti wa tume, hawatapata tabu. Ila naiomba serikali pia Wakome kabisa kuteua wasomi halafu wanakuja kuwadhalilisha kama walivyomfanyia Mzee Wetu Warioba.
 
Hakuna Mzalendo wa kweli kama Warioba hapa Tanzania kwa kipindi hiki kama watatokea basi ni baadaye sana, CCM hawaweziu kufikiri , maana Warioba amewambia wazi kuwa msimamo wake yeye kama Warioba ni Serikali mbili lakini akaamua kuweka msimamo wake pembeni na kuwasilisha maoni ya wananchi walio wengi

Kwa zile logic walizotoa kwa serikali tatu wanaosema mbili wanasema tu wakiwa na imani watawaambia waZenj watupe katiba yao jambo ambalo sio rahisi!
 
Thanks Warioba, wewe ni jasiri kama Baba wa Taifa.

Ingekuwa nchi inawatu waelevu kama Kenya mbona Mwakyembe na Sita tumewasahaukwanini watubebeshe gharama kubwa za umeme hivi kwa tamaa zao hata watoto wao wasingetamba
 
Safi sana Warioba siyo kuzazi cha zaluma cha akina Sita na Mwakyembe
 
Ningependa kuuliza swali moja kwa watanzania wenzangu wasiopendelea itikadi wala mlengo wowote. Hivi ni kwanini tume zote zinazoundwa tanzania zikiwakilisha ripoti zao kwa watawala huwa hawataki kuzikubali hasa zinapokuwa zimegusa masuala ya muungano?
Mfano: 01: Tume ya jaji nyalali
02: Tume ya jaji kisanga
03: Tume ya jai warioba
CIA inawalazimisha watawala hivyo.Huoni Kikwete mwanzoni aliridhia kaja kugeuka mwishoni
 
Hakuna Mzalendo wa kweli kama Warioba hapa Tanzania kwa kipindi hiki kama watatokea basi ni baadaye sana, CCM hawaweziu kufikiri , maana Warioba amewambia wazi kuwa msimamo wake yeye kama Warioba ni Serikali mbili lakini akaamua kuweka msimamo wake pembeni na kuwasilisha maoni ya wananchi walio wengi

!
!
bila kumsahau Mch. Christopher Mtikila.......huyu harakati kazianza kitambo mno na hatuna budi kutambua mchango wake.
 
Warioba alikuwa anawakilisha mawazo ya shetani kwenye katiba mpya. Bahati nzuri Mungu yu pamoja nasi

!
!
afadhali...naona unaweza kunisaidia kitu unaonekana kuna kitu unakijua kuhusu Mungu na Shetani. Nisaidie yafuatayo,

2. Shetani ni nani/nini?...Yuko wapi?.... ana nguvu kiasi gani?....pia kama unajua alitokea wapi.
kuna uzi nimeomba "msaada kwa anayemjua vizuri shetani" hebu pitia unisaidie...ili nami nichangie kama kweli ni mawazo ya kishetani au lah
 
Back
Top Bottom