Paul Kimiti akiri kuhujumu Katiba ya Joseph Sinde Warioba

Izia maji

JF-Expert Member
Dec 1, 2021
2,215
3,859
Leo jumatatu katika kipindi cha Dakika 45 cha ITV kinachoongozwa na Farhia Middle aliyekuwa Waziri wa Kilimo na pia kada maarufu wa CCM amekiri kuhujumu katiba ya Warioba ambayo ilipendekeza serikali tatu.

Itakumbukwa Kimiti alikuwa mjumbe wa Tume ya Warioba iliyozunguka nchi nzima kutafuta maoni ya wananchi juu ya katiba mpya. Aidha alikuwa Mwenyekiti wa kamati namba 16 ndani ya Bunge la katiba.

Katika kipindi cha leo amesema aliona serikali tatu zitaleta mgawanyiko na hatimaye kuvunjika kwa Muungano baina ya Tanganyika na Zanzibar na hivyo kwenda kinyume na makubaliano ya Tume ya Warioba. Kwa hiyo alishiriki kuwashawishi wajumbe wa kamati yake namba 16 kupinga mapendekezo ya Tume ya Warioba.

Pole sana Mzalendo Warioba kwa kusalitiwa wa wajumbe wanafiki wa Tume yako!
 
Leo jumatatu katika kipindi cha Dakika 45 cha ITV kinachoongozwa na Farhia Middle aliyekuwa Waziri wa Kilimo na pia kada maarufu wa CCM amekiri kuhujumu katiba ya Warioba ambayo ilipendekeza serikali tatu...
Kueleza ukweli kinagaubaga, bayana tena hadharani, sio usaliti ni ungwana na uzalendrooo wa kiwango cha juu sana 🐒
 
Nasikia alitonywa na wavaa suti kuwa ajiandaye kuteuliwa kuwa PM (lkn iwe siri), yeye akaenda kumwambia mkewe. Mkewe akaenda saloon kutangaza halafu habari ikavuja.
Mkapa akabadilisha jina. Yeye kakopa hela huko, akashona suti za maana akashangaa jina linatajwa la Sumaye.
Ni kweli na kumbuka wakati ule aliyekuwa Mkuu wa Usalama wa Taifa alikuwa mtu wa kwao Rukwa Marehemu Walingozi.
 
Uungwana na uzalendo angejiondoa katika kuongoza kamati badala ya kubaki na kuipotosha!
Ajiondoe vipi akati amebaini, ametathimini na kujiridhisha kwamba jambo fulani likitekelezwa kama ambavyo lilikua, linaweza kuleta madhara ikiwa ni pamoja na kuvunjika kwa Muungano na kwahivyo halina tija 🐒

Kwasababu hiyo ajiuzulu, dah 🤣

Uzuri mzee wa watu, hana mihemko wala ghadhabu dhidi ya tofauti ya mawazo na mitazamo wa wengine,
so hawezi kuzira, kususa wala kujiuzulu 🐒
 
Nauona mwanga Nchi yetu naona wengi sasa wanaanza kusema siri walizozificha Moyoni..
Ninaamini Uzalendo unarejea!
tukiweza kudhibit external forces within our internal politics, na tukaweza kudhibit imotions zetu wenyewe kwenye masuala ya kitaifa, tukaamua kuwa waungwana na wastahimilivu dhidi ya mawazo na mitazamo tofauti yetu au ya wengine, Lazima tutapiga hatua kubwa mno ya maendeleo 🐒

misimamo binafsi na ya vyama vyetu wala haina tija, zaidi sana inatuchelewesha tu na kudhoofisha umoja na uzalendrooo wetu kwa Taifa letu...
Still we have a chance, we can...
 
ajiondoe vipi akati amebaini, ametathimini na kujiridhisha kwamba jambo fulani likitekelezwa kama ambavyo lilikua, linaweza kuleta madhara ikiwa ni pamoja na kuvunjika kwa Muungano na kwahivyo halina tija 🐒

kwasabb hiyo ajiuzulu, dah 🤣

uzuri mzee wa watu, hana mihemko wala ghadhabu dhidi ya tofauti ya mawazo na mitazamo wa wengine,
so hawezi kuzira, kususa wala kujiuzulu 🐒
Sasa huo ndiyo unafiki wenyewe ambao Kimiti ametuonyesha! Kwa kifupi haaminiki na ndiyo sababu inawezekana aliukosa u-PM!
 
Sasa huo ndiyo unafiki wenyewe ambao Kimiti ametuonyesha! Kwa kifupi haaminiki na ndiyo sababu inawezekana aliukosa u-PM!
unafiki vep tena 🐒

yaani kubainisha na kujiridhisha kwamba jambo fulani si sawa ndio unafiki?

si lazima umuamini wew, wengine watamuamini, kwan kuna shida gan 🐒

hayo mengine sijui ya kukosa nini ni mihemko, ghadhabu, dua la kuku na maneno ya mkosaji tu. ni useless 🐒
 
unafiki vep tena 🐒

yaani kubainisha na kujiridhisha kwamba jambo fulani si sawa ndio unafiki?

si lazima umuamini wew, wengine watamuamini, kwan kuna shida gan 🐒

hayo mengine sijui ya kukosa nini ni mihemko, ghadhabu, dua la kuku na maneno ya mkosaji tu. ni useless 🐒
Unafiki ni tabia ya mtu kutokuonyesha hisia zake halisi au kutokuwa mkweli, yaani mtu anafuata mkumbo ili asieleweke vibaya!

Kwa hiyo mtu wa namna hiyo si wa kumwamini katika kutoa maamuzi magumu kwani anaweza kuwaponza. Mtu wa hivyo haoni shida kwenda kuwachongea au hata kutoa siri kwa maadui wenu.

Kwa kifupi HAFAI KUSHIRIKIANA NAYE!
 
Nasikia alitonywa na wavaa suti kuwa ajiandaye kuteuliwa kuwa PM (lkn iwe siri), yeye akaenda kumwambia mkewe. Mkewe akaenda saloon kutangaza halafu habari ikavuja.

Mkapa akabadilisha jina. Yeye kakopa hela huko, akashona suti za maana akashangaa jina linatajwa la Sumaye.
Noma kweli !
 
Nami nilimsikia na kumuona kupitia hicho kipindi cha dk 45 ITV,alikuwa yupo na SODA aliyopewa na Bonite Bottles,soda ya PILI kuzalishwa mwaka 1987,ya KWANZA alipewa Hayati Ali Hasan Mwinyi

Ila yote kwa yote Jaji Warioba,atabaki SHUJAA wangu,kazi aliyofanya na TUME yake,ilikuwa ni KAZI TUKUKA..Kongole kwake !
 
Back
Top Bottom