Hii ndiyo Derby yenye Maajabu sijawahi sikia wala ona

THE FIRST BORN

JF-Expert Member
Apr 24, 2019
1,760
3,323
Habari Mwanajukwaa.

Kesho Tarehe 20 siku ya Jumamosi kunaenda kupigwa Mchezo wa watani wa jadi kati ya Yanga Vs Simba.

Ila moja ya kitu ambacho hua kina staajabisha katika huu Mchezo ni Moja ya sifa ya Kipekeee kabisa ya Derby hii na huu upekee unaifanya hii Derby itofautiane na Derby zote Dunian uzijuazo wewe hapo.

Na maajabu yake ni haya.

Kama naongopa hii ndio DERBY Pekee ambayo watu wanakwambia waziwazi Miaka na Miaka kua Derby ya Kariakoo hua haieleweki ukimuuliza kivipi mtu anakujibu hii game haijawahi amuliwa kwa Ubora wa Team.

Ukimuuliza hua inaamuliwa na Nini sasa?

Atakujibu ina Mambo Mengi kuanzia nje ya Uwanja hadi ndani ya uwanja ila hasahasa Nje ya Uwanja.

Unauliza Tena kwahio huwa inahusisha ushirikina sana?

Atakujibu kwa nguvu kabisa anhaaa hapana hakuna uchawi kwenye mpira ni mambo tu ya nje ya uwanja.

Sasa unajiuliza Mambo gani hayo jaman?
Any way kama nimedanganya sema kuanzia mwanzo wa shamrashamra za hii match hujasikia hii kauli? Na usiniambie ndiyo utakua umesikia kwa Mara ya kwanza Big NO hua ipo kila Derby, sa swali jepesi ushawahi sikia Derby gani huko ulimwenguni ina sifa hii?

Yani Man City vs Man United watu watakua na kiwewe ila sio kwa kauli ya hivi.

Arsenal vs Chelsea the same.

Mi namaliza.
#USIKU MWEMA
 
Yanga itashinda bao mbili na kuzuia simba wasirudishe magoli, Mpira utakwisha na Yanga kuzima kabisa ndoto za Simba za ubingwa msimu Huu. Goli moja ni la Aziz Ki.
Kesho Yanga isiwakose Aucho na Mkude katikati na Musonda na Mzize kule mbele.
 
Back
Top Bottom