Kuna haja serikali itafute njia mbadala ya kusafirisha viongozi maana ishakuwa adhabu kwa raia wengine hasa kwa Dar.
Leo kwa watumiaji wa Pugu Road kuanzia Vingunguti mpaka Airport watakuwa mashuhuda wa hili.
Barabara za Vingunguti kwenda kwa Mnyamani na ya Majumba Sita kwenda Kinyerezi zote zimefungwa sababu ya ujenzi. Mbadala pekee ni mchepuko wa mataa ya Airport.
Sasa leo bila taarifa maalum traffic wamejazana kwenye mataa ya Airport na kwa ubabe kabisa wanaforce watu waende moja kwa moja wasiingie barabara inayokwenda kulia kuelekea majumba sita.
Baada ya takriban lisaa limoja ndio misafara inaanza kutoka Airport. Sasa kwa starehe ya viongozi wachache nusu ya mji ulisimama ama kutaabisha watu kwenda masafa marefu kufika makwao. Kuna baadhi ya watu makazi yao yapo mita chache tu toka petrol station ya Airport lakini walilazimishwa kwenda mpaka mataa ya majumba sita ambapo napo kumefungwa kulazimisha kugeuza tena na kurudi nyuma.
Na hao matraffic waliokuwepo hapo walikuwa wakorofi na kuwa na lugha mbovu walipoulizwa sababu za kuzuia magari. Kuna polisi mmoja bonge alikuwa na uniform za khaki alidiriki hata kutishia kupiga baadhi ya madereva.
Nadhani ni wakati sasa serikali ijitathmini upya katika swala zima la kuratibu misafara ya viongozi. Maana hii ishakuwa kero kubwa hasa mida ya asubuhi na jioni njia ya Airport.
Kuna wakati hata ndege hazijatua magari yanasimamishwa, mpaka itue na hao viongozi wajivute kutoka wakati huo wengine wamenasa kwenye foleni tu.