Hii hali mpaka lini? Tulaumu mvua?

o_2

JF-Expert Member
Jul 20, 2017
349
287
Habari ndugu mdau,

Baada ya salamu, naomba niende moja kwa moja kwenye mada kama inavyo jieleza. Kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha, mayowe ni mengi sana kila kona kwenye mvua.

Bahati nzuri hizi mvua sio mwaka huu tu ndio zinanyesha, miaka yoote zinanyesha lakini akili tuko nazo zimeshindwa kutatua changamoto zinazosababishwa na mvua.

Mafuriko kupelekea miundombinu hovyo kuharibika hovyo ni wa kujilaumu wenyewe. Ukianzia Rufiji, kichangani (Morogoro), Kyela, mbeya, Tabora, Geita kote huko ni vilio vya athari zitokanazo na mvua zinazoendelea kunyesha. Lakini kama miundombinu ingekuwa imara, huenda athari zisingeekuwa kubwa kiasi hiki.

Wizara ya ujenzi, Tanroad na Tarura ni kichefuchefu. Watu wa mipango miji ndio wa hovyo kuliko na wenyeviti wao wa vijiji ( baadhi). Kama kila mtu angefanya majukumu yake sawasawa haya yasingetokea.

Barabara kutoka Lukozi (Lushoto) ilipaswa kuweka lami kutokana umuhimu wake wa kuzalisha mazao ya matunda na mbogamboga. Wale wafanyabiashara wa karoti na kabichi kama nawaona hali walizonazo. Gari zimekwama. Huo ni mfano mmoja, weka Rufiji, weka handeni huko kwa wazigua n.k.

Kila mwaka mvua zinanyesha, vilio vile vile. Lini tutapata akili ya kumaliza changamoto tunazokutana nazo hasa misimu ya mvua?
 
Back
Top Bottom