HALIMA MDEE bado anastahili kupewa heshima kwa yote aliyofanya

rosemarie

JF-Expert Member
Mar 22, 2011
6,887
3,413
Kwa mara ya kwanza tangu kuisha uchaguzi mwezi uliopita nilipatwa na mshtuko mkubwa sana kusikia Halima pamoja na wenzake wametusaliti lakini nimetafakari sana na nikaja na uamuzi wangu binafsi,pamoja na yote hayo lakini bado Halima ni bonge la mwanamke shupavu sana ambaye wengi tumeshindwa kufikia level yake
kama binadam Halima ametufanyia hayo,Biblia inasema amelaaniwa amtumainiaye binadam na kumfanya nguzo yake,inasema tena Mungu sio kama binadam kwa sababu Binadam ana tabia ya kubadilika badilika,kwa sababu hiyo tusihangae sana alichofanya Halima kwa sababu ni Binadam nahisi kama ametuvunja moyo hasa ukizingatia tulikuwa tunasubiri maamuzi kutoka Bunge la Ulaya pamoja na Nchi za Ulaya na Marekani kufanya maamuzi,lakini nahisi hilo haliaathiri mipango inayoendelea pamoja na yote hayo nipende kwambia Halima Mdee maneno yafuatayo!!!!!


Ulijitoa sana katika safari nzima ya mabadiliko na demokrasia kwenye nchi yetu,ulishiriki kuelimisha uma wa watanzania kuhusu demokrasia na haki,nakushukuru sana kwa hilo japo umenivunja moyo lakini bado nakuheshimu sana sana na Mungu wangu ni shahidi

Nakutakia kila heri na mafanikio huko uendako,umefanya wajibu wako na kama binadamu umeanya maamuzi yako vilevile

Kwetu sisi mapambano bado yanaendela mpaka dakika ya mwisho mama,ubarikiwe tu na Mungu
 
Ushupavu wake ungepimwa kipindi hii ambapo amekosa ubunge na akaendelea kuwa muaminifu kwa chama. Kuna wenzake wamepigana sana, wamekwatwa mara zote viti maalum na hawajawahi kuwa wabunge wa la mabarozi wapo na hawajawahi kukisaliti chama.
Kukisaliti chama kisa kakosa ubunge wa kupigiwa kura akapita mlango wa uani apate wa viti maalum ina maana ile vita yote aliyopigana ilikuwa kwa maslahi ya tumbo lake tu.
 
1606321610355.png
 
Kabla hujafa hujaumbika, ameanza vizur mwisho umekua mbaya, hata mm alima nilimuheshimu sana ila kwa kitendo alichofanya ni usaliti japo ninahisi yawezakua wamerazimishwa.
 
Sikitiko langu kubwa sio Halima kutu disapoint, sikitiko kubwa ni pale Mahakama, Serikali na Bunge waliposhirikiana kukiuka SHERIA za nchi kwa kumtoa Nusrat Hanje kinyume na utaratibu na kumuapisha. Jambo hilo litoshe kutuonyesha kwamba HAKUNA TENA UTAWALA WA SHERIA nchini.
 
Siku zote akifanyacho mtu huwa anafanya kwa mslahi yake binafsi na watu wake wa karibu, usipolijua hili utaendelea ku disappointiwa huku Dunia ikiku surprise kila kukicha
 
Back
Top Bottom