Hakuna taifa litakalo kua imara pasipo stable moral foundation

Shayu

Platinum Member
May 24, 2011
608
1,653
Haijalishi ukubwa wa harusi uliyofanya, kitu cha muhimu ni unachokwenda kukijenga baada ya harusi, baada ya watu wote kuondoka na kuwaacha peke yenu mwende nyumbani, mkaanzishe maisha yenu. hiko ndicho cha muhimu na ndicho kinachotakiwa kupewa umakini mkubwa. Sio kwako tu hata kwa taifa. Kwakuwa familia ni kiwanda cha kutengeneza raia wema.

Usisahau hilo jua kwamba una kazi kubwa mbele yako, na usichukulie harusi kwa ukubwa usiostahili zaidi ya kile unachoenda kukijenga. "Familia" Harusi na majigambo yake yote sio muhimu kiasi hiko.

Harusi ni ya siku moja, lakini unachokwenda kukijenga huenda kikaishi muda, zaidi ya uhai wako. Kwakuwa misingi utakayo wajengea watoto wako ndio misingi hiyo hiyo watakayo wajengea watoto wao. Ubora wa familia yako huenda ukawa pia ubora wa familia zao.

Wewe na mke wako mtakapofutika kwenye uso wa dunia, maisha yao duniani yatategemea misingi mliyowajengea.

Kwahiyo kuwa makini zingatia haya. Ongoza watoto waliotoka katika tumbo lako vyema nao watakupa faraja ya roho. Hakuna kinachoumiza roho kama kuwa na mtoto mpumbavu.

Katika kila mtoto kuna asili mbili ndani yake. The good and bad nature.

Ni wajibu wetu ku correct bad nature ya mtoto na kuruhusu good nature yake kukua.

Nature ya mtoto hukua kulingana na kilichoruhusiwa kuota ndani yake.

So ni wajibu wetu kama bwana shamba kupalilia na kuondoa magugu yote ili mimea iote vyema.

Kwakuwa mzazi katika malezi ni kama mkulima. Ambaye hupalilia shamba kuondoa magugu kisha kumwagilia mimea midogo ili ikue.

Na tunasemaga katika misemo yetu mtoto umleavyo ndivyo akuavyo. So if we ourselves we are bad tusitegemee watoto wetu watakuwa wazuri..kwahiyo ni wajibu wetu kuji correct kila siku na wakati huo huo tuki correct watoto wetu.

Hata sisi waswahili tuna msemo unaosema samaki mkunje angali mbichi. Kwahiyo tabia za vijana zinategemea sana malezi. Ndio maana familia ni kitu muhimu sana kwa maisha ya taifa lolote lile.

Bila familia imara huwezi kuwa na taifa imara. Hawa wanaotoka kwenye familia ndio wanaoingia makazini na kwenye mifumo ya kiserikali. Unaweza kufikiri kama maadili sio mazuri tutavuna nini? Na serikali isitegemee kupata raia wenye utii kama familia zimeparaganyika na hakuna utii wa watoto kwa wazazi wao.

Management inaanza huko chini kama familia zimeshindwa kuwa managed vizuri na watoto kukengeuka, tujue kwamba taifa litakuwa hatarini. Hakuna taifa litakalo kua imara pasipo stable moral foundation.
 
Back
Top Bottom