Peter Madukwa
JF-Expert Member
- Sep 20, 2012
- 3,137
- 2,478
Baadhi ya wananchi wa Nachingwea ambao wapo ktk kundi sogozi la WhatsApp la NACHINGWEA YETU, wamekabidhi mifuko 300 ya saruji kuunga mkono ujenzi wa mradi mpya wa Nachingwea boys high school inayojengwa kwa kutumia mapato ya ndani ya halmashauri ya wilaya ya Nachingwea iliyopo mkoa wa Lindi
Shule hiyo inatarajiwa kukamilika kwake kuchukua wanafunzi 1600 kuanzia kidato Cha Kwanza Hadi Cha sita.
Aidha shule hiyo mpya ya wavulana inatarajiwa kuwa na jumla ya majengo 54 ikiwemo madarasa, mabweni, nyumba za walimu, duka, zahanati na sehemu ya kula chakula.
Shule hiyo inajengwa nje kidogo ya mji wa Nachingwea katika kijiji Cha chiumbati kata ya chiumbati tarafa ya Naipanga
Akizungumza wakati wa kupokea mchango huo, aliyekuwa mkurugenzi wa halmashauri hiyo ambaye kwa sasa Ni katibu tawala mkoa wa DSM Bwn Hassan Abasi Rugwa, amewashukuru wadau hao wa Nachingwea Yetu Whatsapp group kwa mchango wao na kuwasisitiza wananchi wa Nachingwea kuendelea kushikamana kwa pamoja ili kufanya Mambo makubwa zaidi.
Wanafamilia hao wa Nachingwea Yetu WhatsApp group wamesema kuwa lengo la kuchangishana mchango huo Ni pamoja na
1. kushiriki kama wadau ktk ujenzi wa mradi huo
2. Kuwatia moyo watendaji wa halmashauri ya Nachingwea ktk jitihada za kutatua changamoto za elimu
3. Kutoka hamasa kwa wananchi kushiriki ktk ujenzi miradi ya maendeleo hasa miradi ya wananchi
4. Kujenga umoja na mshikamano miongoni mwa wananchi Kama silaha ya kutatua changamoto mbalimbali za wilaya ya Nachingwea
Serikali imeonesha Nia ya kuunga mkono ujenzi wa shule hiyo baada ya kuona jitihada za dhati zinazofanywa na wakazi wa Nachingwea