Great Leap Forward 1958-62: Vita ya mwanadamu dhidi ya viumbe ilioua watu Million 50

zitto junior

JF-Expert Member
Oct 7, 2013
19,169
28,936
Habari za sikukuu wana JF natumaini kila mtu ni mzima wa Afya bila kupoteza muda twende kwenye mada na ningeomba tuisome kwa umakini sana maana kuna jambo kubwa nataka tujifunze mwishoni, Karibuni.
images (59).jpg

UTANGULIZI
Tumeshazoea mara zote vita ni kati ya mataifa na mataifa au serikali na waasi n.k lakini kwa Mao Zedong Kiongozi mkuu wa China mwaka 1958 alileta mpya ambapo alitangaza vita dhidi ya viumbe wa jamii 4 akiamini kwamba hao ni moja ya maadui wakubwa wa maendeleo hivyo ili china isonge mbele ilitakiwa kuwateketeza kabisa. Vita hii ilikuwa chini ya sera kuu ya ''GREAT LEAP FORWARD'' ikiwa na nia ya kuifanya China iwe ya kisasa na kupaa kiuchumi ukizingatia ilikuwa imetoka kwenye vita iliyomaliza kabisa uchumi na nguvu kazi yake. Ukizingatia kwa takwimu,China ilipoteza watu zaidi ya million 20 kwenye vita kuu ya pili ya Dunia na bado vita kati ya KMT na waasi wa kikomunisti chini ya Mao Zedong nayo ilivuruga sana shughuli za maendeleo hivyo china kuwa moja ya nchi maskini zaidi duniani katika muongo ule wa 1950s.

MAADUI
Maadui waliotajwa ni wale wanaosababisha magonjwa ya wanyama na mimea, kuvuruga shughuli za uzalishaji n.k na list ikatolewa ya viumbe 4 yaani panya,ndege(sparrow),mbu na nzi ambapo walitangaziwa vita ilioitwa "4 pests campaign" na aliyekuwa kipaumbele zaidi kwenye vita hii alikuwa ndege aina ya sparrow ambaye alikuwa na mashtaka ya kula matunda,nafaka shambani na mbegu. Nzi pia wana kesi ya kusababisha magonjwa ya mlipuko, mbu magonjwa kama malaria inayohusika na vifo vingi zaidi duniani pamoja na panya ambao pia wanafahamika kwa uharibifu.
tyh-394x600.jpg

VITA
Vita ilianza kupiganwa kwa kushirikisha wananchi,askari na wataalamu wa mifugo/wanyama n.k ambapo kemikali zilipulizwa, sumu kumwagwa kwenye mazalia ila vita ilikuwa kubwa zaidi kwa ndege huyu sparrow. Kuna wengine walitumia mpaka bunduki kuwatungua ndege, wananchi wengine kwa mamilion walishika sufuria na mabakuli na kuyapiga na mwiko ili kutengeneza kelele kwa ndege kiasi kwamba washindwe kutua na hivyo kupaa hadi kuchoka na mwishowe kuanguka na kufa. Pia viota vyao viliharibiwa,mayai yao kupasuliwa na pia vichanga vyao kumalizwa. Na ilifika mahali mashuleni iliwekwa shindano la atakayeua ndege wengi zaidi ndani ya wiki au mwezi anapewa zawadi nono. Ndege wengi walikimbilia kwenye ofisi za ubalozi wa nchi mbalimbali maana ni maeneo hayo tu ndio waligoma kutekeleza kampeni hii ya kinyama. Wananchi walituma maombi waruhusiwe kuingia kwenye balozi hizo ili kuwamaliza ''maadui'' hao wa taifa walioenda kutafuta hifadhi, ila walikataliwa kwa mfano kwenye ubalozi wa poland. Hivyo basi wakaamua kujiorganize kwenye balozi zote wakiwa na ngoma kubwa na masufuria wakiyagonga na kucheza kwa siku mbili mfululizo yaani usiku na mchana mwisho wa siku ndege waliosalia humo ubalozini walifariki hivyo kukamilisha vita hii dhidi ya ndege na viumbe wengine. Kufikia mwisho wa vita hii, ndege 1 billion , panya 1.5 billion , kilo million 100 za nzi, and kilo million 11 za mbu waliuawa au kuteketezwa.
yjy-415x600.jpg


MATOKEO YA VITA
Baada ya vita kuisha magonjwa yakapungua kwa kiasi kikubwa na maadui hao wanne ni kama walikuwa wametokomezwa kabisa hivyo ilikuwa shangwe kila mahala. Baada ya miezi michache wachina wakapigwa na butwaa baada ya kuona matokeo ya vita sio yale waliyotarajia Yaani wakakuta mazao yao na matunda yamevamiwa na kumalizwa na wakabaki wanajiuliza maswali mengi ni sawa na kufanya msako wa wachawi wote Tanzania na kuwaua alafu kesho yake unakuta umechanjwa usiku kucha!!. Baada ya tafakuri kubwa ikagundulika ndege hawakula tu mazao ya binadamu bali walikuwa wanakula wadudu hatarishi watambaao wengi tu hivyo kuuawa kwa ndege ilikuwa furaha ya wadudu hao ambao ssa walizaliana kwa wingi na hivyo wakawa huru kushambulia chochote mbele yao hivyo mashamba,nafaka,matunda yalivamiwa na wadudu hawa na yakafyekwa kabisa hivyo badala ya kuongeza mazao vita hii ndio ikaporomosha uzalishaji wa mazao kabisa.
523.jpg


NJAA KALI
Kufikia mwaka huo 1958 mwishoni njaa kali sana ilianza kuripotiwa Huko China ambako watu wengi walikufa sababu ya kukosa chakula ambapo vifo vilivyohusiana na njaa vinaanzia million 45 kwa makadirio ya chini mpaka million 70 kwa makadirio ya juu ingawa serikali ya china inasema ni watu 15 million pekee!!! Lakini yote kwa yote watu wengi sana walikufa. Hayakuwahi kuonekana mateso kama haya huko china kwa wakati huo (ukiachana na rape of nanjing) ambapo watu walianza kulana wenyewe kwa wenyewe yaani mwenye nguvu anaua mwenzake na kumla mzima mzima, pia kuna kesi ziliripotiwa za watu kula maiti ambapo kuna wazazi walikula watoto wao, waume kuua wake zao na kuwala n.k kiufupi watu hawakuwa wanadamu tena na wakaanza kujuta kwanini walifanya unyama ule ingawa walikwisha chelewa sana.
famine.jpg


HATUA ZA SERIKALI
Kinachoshangaza katika kampeni hii ni kwamba china ilikuwa na store za vyakula ambazo zingeweza kutosha kulisha nchi nzima ila bado haieleweki ni kwanini walikataa kuisambaza kwa wananchi ingawa nahisi udikteta wa Mao ulichangia maana inaelezwa kila akitembelea miji kadhaa kukagua shughuli za maendeleo wale viongozi wa maeneo hayo walificha ukweli maana waliogopa kuhoji kampeni yake hiyo au kumkosoa. Kuna kisa kimoja kinasema alipoenda kutembelea mji fulani wale viongozi usiku kucha walikesha kupandikiza shamba yaani wakachukua mazao kutoka mashamba ya miji jirani na kuyaleta kwenye maeneo yao kwa uangalifu sana kiasi Mao alipokuja aliona mashamba ni mazima kabisa kumbe hakujua yamepandikizwa tu ili kumfurahisha. Hali hii ya uoga kwa dikteta huyu ilichangia kuongeza vifo maana anapewa taarifa tofauti na hali halisi na hata wale waliohoji na kuropoka kuwa kuna njaa walishughulikiwa kama wachochezi na wapinga maendeleo hivyo nao waliuawa kwa ukatili kabisa. Baada ya kufunika ukweli kwa muda mrefu majanga yalizidi kiasi hakuweza kufichwa mtu hivyo serikali ikakubali kushindwa vita hii na ikaamua kumtoa ndege kama adui wa nchi na ikamuongeza kunguni kwenye ''maadui 4 wa taifa'' ingawa madhara yalishakuwa makubwa na watu kibao walishafariki.
bengal.jpg

HITIMISHO
Hapa tunaweza kupata funzo kubwa kuwa kila kitu kina umuhimu wake duniani ndio maana Mungu alikiumba hivyo ni vizuri tukitunze na kuheshimu uwepo wake. Hata nje ya wadudu tu hata duniani kuna baadhi ya watu wanaona vyama vingine havina haki ya kuwepo au watu fulani hawastahili kuwepo kwenye maisha yako bila kujua pale walipo wanazuia mengi sana yasikukute maishani mwako au uongozi wa nchi yako ila siku vyama hivyo vikifa au watu hao wakaondoka kwenye maisha yako ndipo utagundua umuhimu wao hivyo tujifunze kuheshimu utofauti wetu uwe wa mazuri au mabaya.

Naomba kuwasilisha
images (60).jpg

Jiulize nani ni sparrow kwenye maisha yako?
 
Hapa nimepata funzo kubwa sana hasa hili la uongozi, udikteta, au utii wa sheria na kutimiza wajibu wako kulingana na mamlaka uliyo nayo no matter unaonekana msaliti au huheshimu mamlaka.

Katika hiki kisa ni kwamba viongozi wengi wa mashinani kule china walikuwa wanamuogopa bwana Mao ili tu waweza kulinda vyeo vyao na maisha yao hivo wakawa ni sawa bwana mkubwa, watu wa kuitikia kila kitu..

Jambo hili tunaliona sasa nchini Tanzania bila kupepesa macho wala uoga watu ambao ni viongozi hapa nchini wanafanya mambo Kwa kumuogopa bwana magufuli hivo hawa ni mabwana ndio!

Wakimpinga watakula wapi, hawajui kulima, kufuga wala ubunifu wowote.

Jambo hili linatukwamisha kama taifa.

Fikiria lile suala lililojitokeza mwaka 2016 madai ya kwamba Kuna njaa nchini, viongozi walitumia nguvu kumuaminisha magufuli kwamba wananchi wana chakula cha kutosha.

Hii yote ni kumuogopa, kutoonekana msaliti, na kumtukuza binadamu mwenzako.

Viongozi acheni hizo, mjitambue bhana mnaboa kishenzi yaani.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hii ilikua laana tu kwao

Sent using Jamii Forums mobile app
Ni kweli mkuu hawakujua kila kiumbe duniani kina maana yake kwanini Mungu amekiweka.... Ssa walipoua ndege wakaharibu food chain ya viumbe mwisho wa siku majanga yakaanza. Ndio maana nlishangaa documentary moja ya wazungu wanakamata majoka makubwa huku mijini alafu badala ya kuyaua wanayarudisha msituni wanamaana yao sababu wakisema waue nyoka wote duniani vitatokea tusivyotarajia.
 
Mkuu zitto junior naomba kuuliza,baada ya kumtoa ndege walifanikiwa?
Pia kama kuna strategy nyengine walizotumia naomba utuwekee

Sent using Jamii Forums mobile app
Hawakufanikiwa sababu lengo lao ilikuwa kuongeza uzalishaji sasa walimuona ndege ni kizuizi, walivyomuua ndio wadudu wengi wakawa huru kuvamia mashamba hivyo uzalishaji ukapungua ikapelekea njaa na mwishowe wakasalimu amri na ndege wakamfuta kama adui wa nchi sasa akawa Rafiki wa nchi

Strategy zingine zilikuja baadae na zikafanikiwa sana kwenye eneo la kilimo ila katika hili la kudhani wadudu fulani ni maadui wa nchi waliingia chaka kabisa na Waikiri hilo mwaka 1962.
 
Hawakufanikiwa sababu lengo lao ilikuwa kuongeza uzalishaji sasa walimuona ndege ni kizuizi, walivyomuua ndio wadudu wengi wakawa huru kuvamia mashamba hivyo uzalishaji ukapungua ikapelekea njaa na mwishowe wakasalimu amri na ndege wakamfuta kama adui wa nchi sasa akawa Rafiki wa nchi

Strategy zingine zilikuja baadae na zikafanikiwa sana kwenye eneo la kilimo ila katika hili la kudhani wadudu fulani ni maadui wa nchi waliingia chaka kabisa na Waikiri hilo mwaka 1962.
Asante mkuu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom