Hii vita kati ya mwanadamu na shetani ni vita ya uonevu(haina usawa na haki)

Tajiri Tanzanite

JF-Expert Member
Oct 23, 2016
2,085
3,729
Hapo vip!!
Awali ya yote nadeclare yakwamba ni lazima nitalipiza kisasi cha milele dhidi shetani na lazima nitalipa kisasi juu yake.

Nije kwenye mada husika yakwamba ninaposema hii vita kati ya mwanadamu na shetani sio sawa na haki ni kwasababu zifuatazo.

1. Vita hii mwanadamu ni kiumbe ambayo kwa namna alivyoumbwa anauwezo wa kumbambana na kiumbee kwa umahiri, ubora, kiustadi na uwezo umkubwa kwa adui wake katika hali ya nyama na damu na sio katika ulimwengu wa roho, ndio maana ameweza kubuni na kutengeneza silaha kama, mishale, mikuki, mabomu, mabomu ya nyuklia nakadhalika.

Hivyo basi kujificha kwa shetani na kupewa uwezo wa kumuingia na kumshambulia na kumtesa mwanadamu katika ulimwengu wa roho pasipo mwanadamu kujua tayari ni vita isiyokuwa ya haki na usawa.

Nadhani ingekuwa shetani ni kiumbe chenye kutumia mwili na nyama katika vita hii ni wazi asinge mweza mwanadamu ndio maana akajificha na kupewa uwezo wa kumuingia, kumtumia, kumtesa na kushambulia mwanadamu pasipo mwanadamu kujua ila anakuja kujua baadaye akiwa amesha umizwa na kuteswa na shetani kwa kutumia mapepo, majini, mizimu na wachawi.

Hii vita hata mdhaifu wa kwanza na wa mwisho angesimama upande wa shetani angeonekana mwenye nguvu, wakutisha na mwenye uwezo sana.

2. Hii vita ilikuwa kati ya Mungu na shetani kwa mujibu wa vitabu vyote vya dini Biblia na kuruani lakini anashambulia ni mwanadamu tena kwa mazingira yasiyokuwa ya haki na usawa ni mwanadamu. Shetani ameshindwa huko mbinguni kwenye vita kati yake na jeshi la Mungu ambaye ni malaika, halafu anakuja kufanya vita ambayo sio ya haki na usawa.. ndio maana nasema lazima nitalipiza kisasi huko kwenye ulimwengu wa roho milele juu yake.

NB.kama kweli shetani anauwezo na anamuweza mwanadamu avae mwili na nyama kama Bwana Yesu alivyofanya then aje Duniani kupambana na mwanadamu. Tunamsubiri na dhahiri anaonekana ni kiumbe dhaifu mno hataweza kufanya hivyo kwasababu ya udhaifu wake
 
Unamuita dhaifu kiumbe aliyeshawishi theluthi ya Malaika wa Mbinguni wakamfuata?

Unamuita dhaifu kiumbe ambaye kwasababu ya uwezo wake mkubwa ilimlazimu Malaika Mkuu Mikael kuongoza majeshi ili kupambana nae?

The Devil is powerful, smart and very calculative.Without God's help and Mercy WE are like insects before the Devil.
 
Ndio maana shetani hafanyi attack kwenye phyiscal body baadala yake,he does attack spiritual part(Your body consists of phyiscal body and spiritual body (according to philosophy and theology))

Kama anafanya mashambulizi spiritually basi jua battle ni fair kwa sababu your spiritual part is equipped with everything to win the battle.So,choose wisely.Jesus is Lord.Amen
 
Unamuita dhaifu kiumbe aliyeshawishi theluthi ya Malaika wa Mbinguni wakamfuata?
Unamuita dhaifu kiumbe ambaye kwasababu ya uwezo wake mkubwa ilimlazimu Malaika Mkuu Mikael kuongoza majeshi ili kupambana nae?
The Devil is powerful,smart and very calculative.Without God's help and Mercy WE are like insects before the Devil.
You not me...ni wewe sio mimi
 
Haya mambo bana some time tuyaache kama yalivyo lkn ukituliza akili ukatafakali bila mihemuko utaona mambo haya ya dini yanadosari nyingi sana.
 
Hapo vip!!
Awali ya yote nadeclare yakwamba ni lazima nitalipiza kisasi cha milele dhidi shetani na lazima nitalipa kisasi juu yake.

Nije kwenye mada husika yakwamba ninaposema hii vita kati ya mwanadamu na shetani sio sawa na haki ni kwasababu zifuatazo.
KWANZA, JUA KUWA, VITA ILIYOPO ni kati ya watu waliookoka na shetani. ninyi msiookoka shetani hata hapigani vita na ninyi kabisa, tayari ninyi ni wa kwake, alishawateka, mpo mfukoni mwake anaweza kuwafanya lolote apendalo.

kwetu sisi tuliompa Yesu Maisha ndio tunapigana naye usiku na mchana. hata hivyo ni vita rahisi sana, kwasababu Yesu Kristo alishamshinda shetani. Ukiokoka, Yesu anakaa ndani yako hivyo unamshinda shetani kwa Nguvu za Mungu, na mbele ya nguvu hizo shetani hana lolote kabisa kabisa. alishashindwa. kwahio ni uamzi wako, ukae nje ya wokovu upambane kwa nguvu zako, na katu hautamshinda shetani, au uingie kwenye wokovu shetani apambane kukukimbia. kwa taarifa yenu, sio kwamba namwinua shetani, ila kama hauna nguvu za Mungu shetani atakufanya lolote atakalo, ila ukiokoka ukawa na Nguvu za Mungu, shetani hana nguvu yeyote dhidi yako, na akikudhuru jua umemruhusu.

unamruhusu vipi? kwa kutenda dhambi, unapungukiwa utukufu wa Mungu na pakiwa pachafu tu unakuwa umefungua mlango wa shetani kuingia na kufanya yake, ila kama unaishi katika utakatifu, ukikosea unajitakasa haraka kabla hajaingia, shetani hatakuja kukufanya lolote, utamshinda kila siku. kwahiyo, hii vita labda tuseme shetani ndio amelemewa, kwasababu Nguvu tunazokuwa nazi sisi tuliookoka, ni kuu mno kuliko shetani.

YOHANA 14:30 INASEMA; Mimi sitasema nanyi maneno mengi tena, kwa maana yuaja mkuu wa ulimwengu huu, wala hana kitu kwangu.

WAEFESO 1:19 INASEMA; macho ya mioyo yenu yatiwe nuru, mjue tumaini la mwito wake jinsi lilivyo; na utajiri wa utukufu wa urithi wake katika watakatifu jinsi ulivyo; 19 na ubora wa ukuu wa uweza wake ndani yetu tuaminio jinsi ulivyo; kwa kadiri ya utendaji wa nguvu za uweza wake; 20 aliotenda katika Kristo alipomfufua katika wafu, akamweka mkono wake wa kuume katika ulimwengu wa roho; 21 juu sana kuliko ufalme wote, na mamlaka, na nguvu, na usultani, na kila jina litajwalo, wala si ulimwenguni humu tu, bali katika ule ujao pia; 22 akavitia vitu vyote chini ya miguu yake, akamweka awe kichwa juu ya vitu vyote kwa ajili ya kanisa; ambalo 23 ndilo mwili wake, ukamilifu wake anayekamilika kwa vyote katika vyote.
LUKA 10:19 IMEANDIKWA; 17 Ndipo wale sabini waliporudi kwa furaha, wakisema, Bwana, hata pepo wanatutii kwa jina lako. 18 Akawaambia, Nilimwona Shetani, akianguka kutoka mbinguni kama umeme. 19 Tazama, nimewapa amri ya kukanyaga nyoka na nge, na nguvu zote za yule adui, wala hakuna kitu kitakachowadhuru. 20 Lakini, msifurahi kwa vile pepo wanavyowatii; bali furahini kwa sababu majina yenu yameandikwa mbinguni.

WARUMI 8:37 INASEMA
; Lakini katika mambo hayo yote tunashinda, na zaidi ya kushinda, kwa yeye aliyetupenda. 38 Kwa maana nimekwisha kujua hakika ya kwamba, wala mauti, wala uzima, wala malaika, wala wenye mamlaka, wala yaliyopo, wala yatakayokuwapo, wala wenye uwezo, 39 wala yaliyo juu, wala yaliyo chini, wala kiumbe kinginecho chote hakitaweza kututenga na upendo wa Mungu ulio katika Kristo Yesu Bwana wetu.
 
Vita si ya kwako vita juu ya shetani ni vita kati yako na Mungu wewe tulia fuata amri zake uksaidie kupigana vita na jeshi lake, wewe
 
Umejuaje hajaokoka?
 
Wewe hujawahi kupigana vita kamwe... Ile vita ya Mungu na Shetani ilihamishiwa kwenye akili ya binadamu wala haikuosha hata...wewe umepewa tu uamuzi wa kuchagua ni upande upi wa kukaa na kuusimamia
 
Vita si ya kwako vita juu ya shetani ni vita kati yako na Mungu wewe tulia fuata amri zake uksaidie kupigana vita na jeshi lake, wewe
ukiwa kifungoni kwa shetani ndio unaweza kuwa na fikra kama hii. kwa sababu ni kweli, ukiwa haujaokoka, hupigani vita kabisa, shetani ameshakushinda na amekuweka mfukoni. ila ukiokoka ndipo unaanza kupigana vita, vita ya kutenda mema dhidi ya yeye anakufanya utende mabaya, na anakazia na kukuharibu kwa namna yeyote ile atakayopata njia. huwezi kushika amri za Mungu au kufanya lolote linalompendeza Mungu kama bado upo mfukoni mwa shetani, hiyo nafasi hatakupatia, ndio maana kuna watu wamepambana kuacha uzinzi wameshindwa, kuacha madawa wameshindwa, kuacha sigara wameshindwa, kuacha ujambazi wameshindwa, kuacha dhambif ulani wameshindwa, kuacha ulevi wameshindwa, kwasababu tayari wapo mfukoni mwa shetani.

ila walipompa Yesu Kristo maisha yao, kiu ya uzinzi ilikwisha, ulevi byebye, Mungu anakupatia uwezo wa kushinda dhambi ukimpa maisha yako kwa kuokoka kwa Yesu Kristo, bila Mungu kukusaidia kushinda dhambi, huwezi kuacha chambi. na hupigani vita, wewe ni wa shetani, na mtaenda wote jehanum hata kama unasali kwenye dini ya wakristo.
 
Back
Top Bottom