Gerald Hando: 99% ya wanaozungumzia suala Bandari na DP World ni Mbumbumbu

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,448
8,266
Mtangazaji wa kipindi cha Good Morning cha Wasafi FM, Gerald Hando amesema asilimia 99 ya Watanzania wanaoongelea suala la Ubinafsishaji wa Bandari hawajui chochote kuhusu suala hilo na wengi wao ni Maamuma au Mbumbumbu.

"Asilimia 99 tena naitamka kwa kujiamini kabisa, hata ikiwemo mimi, tunaozungumzia huu mkataba ni mambumbumbu kwenye eneo hilo, kabisa kabisa. Ni watu weupeeee. Ni watu wa kulishwa maneno tu na kuyarudia kama recorder. Ni tahari sana"

Aidha, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Amos Makalla amesema kwa watu waliosoma Cuba (kama yeye) kupinga mkataba wa DP World ni propaganda tu kama zilivyo propaganda zingine na CCM inafanya jambo zuri kujieleza maana uongo ukiachwa hugeuka kuwa ukweli.

Mtangazaji wa Wasafi FM Gerald Hando amesema 99% ya wanaozungumzia mkataba wa bandari ni mambumbumbu.

"Asilimia 99 tena naitamka kwa kujiamini kabisa, hata ikiwemo mimi, tunaozungumzia huu mkataba ni mambumbumbu kwenye eneo hilo, kabisa kabisa. Ni watu weupeeee. Ni watu wa kulishwa maneno tu na kuyarudia kama recorder. Ni tahari sana"

Aidha, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Amos Makalla amesema kwa watu waliosoma Cuba (kama yeye) kupinga mkataba wa DP World ni propaganda tu kama zilivyo propaganda zingine na CCM inafanya jambo zuri kujieleza maana uongo ukiachwa hugeuka kuwa ukweli.

Hando anamaanisha watanganyika hawajui kusoma vipengele kwenye ule mkataba wa hovyo wa bandari na kuona ubovu wake?

Au ameamua kujitutumua ili asikike baada ya kufanya lile igizo lao lililofeli na kina Kitenge na Zembwela?

Au bado mgao wa ile kazi ya hovyo waliyofanya kwenda Dubai bado unawataka kuendelea kutetea ule mkataba wa hovyo kwa kila njia?

Waache maigizo ya kitoto.
 
Hiyo kajigeuzia yeye 99% matap*iko
Dah, inauma sana ndugu kuona watu kama hao wakina hando, kitenge na zembwela wamejipa uhalali na mamlaka ya kuzungumza kwa niaba ya Watanganyika. Hakika wanatudharau sana. Hawa, ikitakiwa tushughulike nao kimya kimya, yaani tunaanza nao huko majumbani mwao ndiyo akili zitawakaa sawa.

Nadhani mpaka sasa, katika wote wanaouzungumzia ule mkataba baina ya Tanzania na DP World, hakuna anaye pinga uwekezaji. Ila watu wanapinga aina ya mkataba tulioingia kama taifa, maana hauna faida kwetu.

Kama hao wamelipwa kuupigia debe huo mkataba, ni bora wakae kimya, maana Watanzania wameshaamka na siyo wajinga tena!
 
Mtangazaji wa kipindi cha Good Morning cha Wasafi FM, Gerald Hando amesema asilimia 99 ya Watanzania wanaoongelea suala la Ubinafsishaji wa Bandari hawajui chochote kuhusu suala hilo na wengi wao ni Maamuma au Mbumbumbu.

"Asilimia 99 tena naitamka kwa kujiamini kabisa, hata ikiwemo mimi, tunaozungumzia huu mkataba ni mambumbumbu kwenye eneo hilo, kabisa kabisa. Ni watu weupeeee. Ni watu wa kulishwa maneno tu na kuyarudia kama recorder. Ni tahari sana"

Aidha, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Amos Makalla amesema kwa watu waliosoma Cuba (kama yeye) kupinga mkataba wa DP World ni propaganda tu kama zilivyo propaganda zingine na CCM inafanya jambo zuri kujieleza maana uongo ukiachwa hugeuka kuwa ukweli.

Ni kweli kabisa kuwa yeye Mhando, Zembwela, Kitenge na the like, ni mbumbumbu sana, tena watu waliopoteza utu kwa kukosa uadilifu wa nafsi.

Jambo ambalo siyo kweli ni kuamini kuna watu wengi mbumbumbu kama wao.
 
Mtangazaji wa kipindi cha Good Morning cha Wasafi FM, Gerald Hando amesema asilimia 99 ya Watanzania wanaoongelea suala la Ubinafsishaji wa Bandari hawajui chochote kuhusu suala hilo na wengi wao ni Maamuma au Mbumbumbu.

"Asilimia 99 tena naitamka kwa kujiamini kabisa, hata ikiwemo mimi, tunaozungumzia huu mkataba ni mambumbumbu kwenye eneo hilo, kabisa kabisa. Ni watu weupeeee. Ni watu wa kulishwa maneno tu na kuyarudia kama recorder. Ni tahari sana"

Aidha, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Amos Makalla amesema kwa watu waliosoma Cuba (kama yeye) kupinga mkataba wa DP World ni propaganda tu kama zilivyo propaganda zingine na CCM inafanya jambo zuri kujieleza maana uongo ukiachwa hugeuka kuwa ukweli.

Popomalism hilo...
 
Wabongo kwanini tuangaike na kusumbuka? Kama mkono unaenda kinywani na unanguvu za kugegeda why kusumbuka sumbuka.
 
Back
Top Bottom