Gari yangu imeingia maji

dracular

JF-Expert Member
Dec 24, 2013
767
1,057
Habari za majukumu wakuu?

Gari yangu aina ya Toyota RAV 4 miss TZ jana ilinasa kwenye dimbwi la maji kwenye kina kirefu kidogo ikabidi mpaka tuite watu yale magari ya breakdown waje waitoe baada ya juhudi zetu kugonga mwamba.

Sasa wakuu kwanza gari baadae ikagoma kuwaka kabisa tukachaji betri ndo ikawaka. Sasa baada ya hapo ikawa ina mis gia na kupoteza nguvu kabisa na sasa imezima kabisa na haiwaki.

Naombeni msaada wa kitaalam hapa shida itakuwa ni nini maana mimi sina uelewa sana kuhusu magari.

Natanguliza shukrani ndugu zangu
 
Pole masta.

Hapo haina maneno mengi, gari maji yameingia inawezekana kwenye engine, sehemu za umeme, etc.

Nashauri umuite fundi afanye ukaguzi mkubwa.
ahsante sana ndugu yangu kwa ushauri wako 🙏
 
Usijaribu kuiwasha ipeleke kwa fundi.
Inawezekana maji yameingia mwenye spark plugs, mfumo wa hewa n.k ila kwa namna yeyote tu maji yameingia kwenye mfumo wa engine hii lazima ipelekee gari kukosa nguvu.
Ahsante.. kwahiyo hapo tatizo ni kubwa sana?
 
Upo umuhimu mkubwa sana kwa mmiliki wa gari kuhakikisha unakuwa na fundi walau mmoja permanent wa gari yako.

Hii husaidia sana kwakuwa fundi anakuwa anaijua gari yako hivyo huhangaiki sana kupeleka gari yako kwa mafundi usiowafahamu.

NB; Hakikisha unamjali fundi wa gari yako kwa kumpa ujira wake bila kupuuzia
 
Gari ikiingia maji usijaribu kuiwasha unatengeneza matatizo makubwa mtafute fundi wa umeme na Engine uone baada ya kufungua na kufuta futa vitu inakuaje hasa sehemu za plug na fuse box...watumie mashine ile ya upepo kukausha kausha...Rav 4 itawaka haina umeme mwingi ila mafundi wahusike msilazimishe kuwasha wakati gari halijachekiwa vizuri...
 
Ahsante mkuu ushauri mzurii huu
 
ahsante nitafanya hivi mkuu
 
Usingewasha hiyo gari ilitakiwa kutoa betri na kuita fundi waangalie wwpi kuna shida. Inawezekana maji yameingia kwenye spark plug na kufanya hiyo missing.
Pia kwenye control box hapo ni shida nyingine.

Ita fundi akufanyie tathmini na kukushauri vyema.
 
Back
Top Bottom