Gari linatoa moshi, msaada wa kiufundi unahitajika

Kaitaba

JF-Expert Member
Jun 30, 2009
916
52
Naomba msaada wa kiufundi, Gari langu linatoa moshi japo kidogo, pia linatumia fuel 8 km kwa lita, SPECIFICATION Spacio old model Petrol fuel SHIDA YA GARI INAKULA MAFUTA SANA INATOA MOSHI MSAADA JAMANI, shida ni kitu gani kwenye gari hili na nifanye nini?
 
Piston ring zimekwisha mkuu, nenda kwa fundi akakuchekie kama kuna uwezekano wa kuwekwa ring standard kama haiwezekani inabidi afanye overhall ya ingine.
 
Jaribu kufanya diagnosis.......utajua tatizo la gari......hii labda labda unaweza kuchokonoa na vingine.......
 
Moshi mana yake kuna partial fuel combustion, chek ring piston kwa fundi.

Pia angia expiry date ya hilo gari, pole sana
 
Piston ring zimekwisha mkuu, nenda kwa fundi akakuchekie kama kuna uwezekano wa kuwekwa ring standard kama haiwezekani inabidi afanye overhall ya ingine.
Nashukuru sana, ila suala hili linatakiwa lifanywe kwa mtaalamu aliyebobea, kwa hapa DAR, hasa Temeke, garage ipi inafaa.
 
Jaribu kufanya diagnosis.......utajua tatizo la gari......hii labda labda unaweza kuchokonoa na vingine.......

Nashukuru sana, Diagnosis inafanyiwa wapi na gharama zinafikia kiasi gani.
 
Moshi mana yake kuna partial fuel combustion, chek ring piston kwa fundi.

Pia angia expiry date ya hilo gari, pole sana
Expire date,,...!!!!!, inaangaliwaje hii, niko blind ktk masuala haya ya magari.
 
Na vipi hili la kutumia km 8 kwa lita moja. au normal inatakiwa iwe kiasi gani
 
Piston ring zimeisha, wasalime mafundi huko garage...

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Nashukuru sana, Diagnosis inafanyiwa wapi na gharama zinafikia kiasi gani.

kama upo Dar.....nadhani wanaojua watakuelekeza.......Huku Yaeda huwa tunafanyia pale garage ya Gidasaida...........
 
Naomba msaada wa kiufundi, Gari langu linatoa moshi japo kidogo, pia linatumia fuel 8 km kwa lita, SPECIFICATION Spacio old model Petrol fuel SHIDA YA GARI INAKULA MAFUTA SANA INATOA MOSHI MSAADA JAMANI, shida ni kitu gani kwenye gari hili na nifanye nini?

Gari lako litakuwa limetembea zaidi ya kilomita 100000 tangu litengenezwe. Bado linanguvu nzuri tu na linaweza kufika speed zaidi ya 100Km/h.

Tatizo la gari lako ni dogo sana. Usikimbilie kufunguwa piston rings utaliharibu gari lako.
unachotakiwa kufanya ni kubadilisha vijitu vidogo sana kwenye gari vinaitwa "Valve stem seals"
Sasa ili uweze kubadilisha huto tujamaa lazima ifunguliwe cylinder head. Na ikifunguliwa unatakiwa ununuwe overhaul gasket kit.
kama gari ingekuwa inakosa nguvu ndio tungehoji uhai wa piston rings.

Kazi ya huto tu jamaa ni kuzuia kiasi chochote cha oil kuingia kwenye combustion chamber ili mchanganyiko wa oksijeni na petrol unaohitajika usiwe na impurities zozote zinaoweza kusababishwa na oil ambayo huwa inawekwa kwenye injini.
 
Je moshi unaotoka ni wa rangi gani? Na je unatoka wakati wote au ukilizima kwa muda mrefu?
 
Na vipi hili la kutumia km 8 kwa lita moja. au normal inatakiwa iwe kiasi gani
Kwani mkuu hilo gari umelinunua karibuni? Gari kutoa moshi kuna sababu kubwa mbili moja oil inaunguzwa pamoja na mafuta, pili uwiano wa mafuta na hewa siyo mzuri (rich mix). Oil ikiungua moshi utakuwa mweupe na mafuta yakizidi moshi unakuwa black.
 
Haya majibu ni very specific Kama upo timamu na unajua magari huwezi toa haya majibu bila kuona gari na kulikagua gari....

Piston ring zimekwisha mkuu, nenda kwa fundi akakuchekie kama kuna uwezekano wa kuwekwa ring standard kama haiwezekani inabidi afanye overhall ya ingine.
 
Unachotakiwa kufanya ni overhaul ya engine ambapo utabadilisha gaskets na seals zote ndani ya engine kuepusha engine oil kuvuja...
Baada ya kufanya hivyo tatizo lako la gari kutoa moshi mara nyingi mweupe litakuwa limeisha...
 
Jamani mimi asubuhi nikiwasha gari inatoa moshi mweupe kama sekunde 30 hivi then unakata nikipiga lesi kama mara tatu hivi sioni moshi ila yanakuwa yanadondoka maji maji hii inaweza kuwa ni tatizo.
Ila huo moshi sio kila siku nauona au kwa sababu ya baridi kali huku niliko ??
 
Tatizo la gari lako itakuwa ni valve seal zimeanza kuzeeka.
 
Back
Top Bottom