SoC03 Familia: Jiko la mapishi ya Uwajibikaji na Utawala Bora katika jamii

Stories of Change - 2023 Competition
Jul 29, 2023
2
4
1690827036734.png

Picha: Gazeti la Mtanzania

UTANGULIZI.

Katika jamii, familia ni msingi thabiti wa ujenzi wa maadili na tabia za kijamii na kizazi kijacho. Kama vile jiko linavyokuwa kitovu cha mapishi, familia pia ni kitovu cha kuhamasisha uwajibikaji na utawala bora. Katika mataifa ya Ulaya na Uarabuni familia za kifalme zimebaki kuaminika kuwa ndizo zina mapishi sahihi ya viongozi wenye kuraghibisha hulka hizo kwa wananchi wengine. Kwa upande mwingine Nchi kutoka Bara la Afrika, Bara la Amerika na baadhi ya Nchi za Asia, zimekuwa zikichagua viongozi kutoka katika familia yoyote ile.kwa kuzingatia vigezo vilivyowekwa kikatiba. Hata hivyo njia zote kwa pamoja zimekuwa na matokeo chanya na hasi.

Nchini Tanzania, tunayo mifano mingi sana ya viongozi mashuhuri, na watendaji wa makampuni na taasisi za umma na binafsi ambao kutokana na malezi bora ya familia wameacha alama kubwa katika jamii. Tanzania tunaye mtu kama Hayati Baba wa Taifa Mwl. Julius K. Nyerere, Bibi Titi Mohamed, Reginald Mengi na wengine wengi. Hawa na wengine wengi ukiwa taja leo Tanzania utasikia sifa kedekede zikiwahusu na hasa katika maeneo mawili uwajibikaji na utawala bora.

Katika hali ya kusikitisha dunia kote, Viongozi na watu wa Kariba hii wanaendelea kuwa adhimu siku hadi siku kiasi ambacho jamii imeendelea kuathiriwa na viongozi na rasilimali watu ambao hawatekelezi wajibu wao ipasavyo. Swali ni Je, Watu wa Kariba hii wamepotelea wapi? Ni dhahiri kuwa familia kama kitovu cha kujenga maadili, uwajibikaji na misingi ya kujiongoza na kuongoza wengine zina majibu kuhusu swali hili kuliko chombo kingine chochote. Familia inaweza kuchangia kuleta mabadiliko chanya katika jamii kupitia malezi bora ya Watoto yanayotoa mafunzo ya uwajibikaji na kuendeleza maadili ya utawala bora.​

Malezi ya familia yanaweza kuhamasisha uwajibikaji na utawala bora endapo tutajenga familia kuwa;

Chombo cha kulea maadili na Mfano Bora:

Kizazi cha karne ya 21 kinauliza, hivi rushwa na ufisadi vitaisha lini? Jibu sahihi lipo kwa wazazi wa kizazi hiki kwani bila wao kufanya maamuzi hali ya rushwa na ufisadi itazidi kuliweka taifa letu katika hali mbaya zaidi. Familia ni lazima iwe na kanuni za maadili ambazo zinakataa vitendo vya ufisadi na rushwa kwa kuweka mipaka na kuchukua hatua za kuzuia ufisadi na ukiukwaji wa maadili ndani ya familia. “Watoto ni muhimu kujengewa uwelewa kuwa fedha na mali siyo kila kitu, na kwamba heshima na sifa njema ni muhimu zaidi.” Hii itabadilisha mtazamo wa watoto kuhusu ufisadi. Kwa kufundisha maadili mema na kuishi kwa kuzingatia kanuni za uadilifu, watoto watajifunza umuhimu wa kuwa wakweli na waadilifu katika maisha yao yote. Watoto wakikua katika mazingira yanayohimiza maadili haya, watakuwa viongozi bora na watu wanaojitolea kwa jamii.​

Jukwaa la mazungumzo na majadiliano.

Ni nadra sana kwa familia zetu za kiafrika kumpa mtoto nafasi ya kutoa maoni yake juu ya jambo la kifamilia. Familia inapaswa kuwaweza Watoto kuwa na fikra tunduizi kwa kuwapa nafasi ya kuchangia katika mambo yanayohusu familia. Kupitia mawasiliano wazi na familia kushirikisha watoto katika majukumu ya kila siku, watoto watapata ujuzi wa uwazi na uwajibikaji. Wazazi wapaswa kuwapa watoto fursa ya kutoa maoni yao na kujisikia sehemu ya maamuzi ya familia, itawajengea utayari wa kubeba uwajibikaji katika matendo yao. Zaidi ya kutoa maoni, Watoto watajifunza masuala ya kijamii na kisiasa jambo ambalo litawafanya kufahamu changamoto na fursa zilizopo katika jamii.​

Chombo kinacholea Utamaduni wa Kushirikiana na Kuaminiana:

Kushirikiana na kuaminiana ni muhimu katika familia na jamii kwa ujumla. Kupitia kuaminiana na kushirikiana, watoto watapata uelewa wa thamani ya kuwa na uhusiano wa kutegemeana na kuaminiana na wengine, na hivyo kudumisha umoja, mshikamano na amani ambazo ndizo tunu za kuimarisha uwajibikaji na utawala bora. Familia inaweza kuhimiza watoto kuchukua hatua hizi za kijamii kwa kushirikiana katika miradi ya maendeleo na kusaidia jamii zao. Kupitia kujitolea na kushirikiana katika shughuli za kijamii, watoto watajifunza umuhimu wa kujali wengine na kuhakikisha kuwa fedha na rasilimali za umma zinatumika vizuri.​

Chombo cha kukuza uwajibikaji.

Familia kwa kushirikiana na taasisi nyingine za kijamii kama shule na serikali inajukumu la kuwafundisha watoto kuhusu uwajibikaji. Watoto wanapaswa kuhimizwa kufanya kazi kwa bidii na kwa uadilifu katika masomo yao na kazi zao za baadaye. Kuelewa kuwa mafanikio yanategemea juhudi za dhati na siyo njia za mkato, itawapa moyo wa kufanya kazi kwa bidii na kuepuka vitendo vya ufisadi na rushwa. Kupewa majukumu ndani ya familia huwajenga watoto kuwa na uwajibikaji na kuona umuhimu wa kushiriki katika maendeleo ya familia yao. Kupitia mfano wa wazazi na walezi, watoto hujifunza jinsi ya kusimamia rasilimali, kama vile pesa na mali. Kupanga matumizi na kuonyesha uwazi kuhusu masuala ya fedha huwajengea watoto utambuzi wa thamani ya rasilimali na jinsi ya kuzitumia kwa manufaa ya familia na jamii kwa ujumla.​

Chombo cha kufundisha demokrasia na utawala bora

Familia inaweza kutoa elimu kwa watoto kuhusu umuhimu wa kushiriki katika shughuli za kijamii na za kisiasa ili kuwajengea tabia ya kufuatilia na kubaini changamoto zinahusu jamii yao. Familia inawajibu wa kuhamasisha ushiriki wa vijana katika majadiliano na mazungumzo kuhusu masuala ya kijamii na kisiasa ili kuwajengea watoto ufahamu na mtazamo wa uwajibikaji na utawala bora. Pia familia inawajibu wa kuhamasisha vijana kushiriki katika chaguzi za serikali za mitaa na za kitaifa. Vijana wanapaswa kupewa haki ya kugombea au kuchagua viongozi wanaowakilisha maslahi yao katika nafasi za siasa kuanzia ngazi ya kifamilia.​

HITIMISHO.

Kama familia, kujenga jiko la mapishi ya uwajibikaji na utawala bora kunahitaji kujitolea na kufanya kazi kwa pamoja. Kila mwanafamilia ana jukumu katika kuhamasisha na kudumisha misingi hii. Kwa kufanya hivyo, tunaweza kuunda jamii zenye uwajibikaji, haki, na maendeleo endelevu kwa siku za usoni. Familia inaweza kuwa chombo cha kuleta mabadiliko chanya katika familia zetu na hatimaye katika jamii nzima. Kwa kuweka msingi imara wa uwajibikaji na utawala bora, tunaweza kuunda jamii yenye amani, maendeleo, na usawa.​

KUMBUKUMBU ZA REJEA.

Julius K. Nyerere, Uhuru na Umoja. Chambuzi kutoka katika machapisho na hotuba 1952-65. (London: Chuo kikuu cha Oxford, 1966 (366p.).​
 
View attachment 2704142
Picha: Gazeti la Mtanzania

UTANGULIZI.

Katika jamii, familia ni msingi thabiti wa ujenzi wa maadili na tabia za kijamii na kizazi kijacho. Kama vile jiko linavyokuwa kitovu cha mapishi, familia pia ni kitovu cha kuhamasisha uwajibikaji na utawala bora. Katika mataifa ya Ulaya na Uarabuni familia za kifalme zimebaki kuaminika kuwa ndizo zina mapishi sahihi ya viongozi wenye kuraghibisha huluka hizo kwa wananchi wengine. Kwa upande mwingine Nchi kutoka Bara la Afrika, Bara la Amerika na baadhi ya Nchi za Asia, zimekuwa zikichagua viongozi kutoka katika familia yoyote ile.kwa kuzingatia vigezo vilivyowekwa kikatiba. Hata hivyo njia zote kwa pamoja zimekuwa na matokeo chanya na hasi.

Nchini Tanzania, tunayo mifano mingi sana ya viongozi mashuhuri, na watendaji wa makampuni na taasisi za umma na binafsi ambao kutokana na malezi bora ya familia wameacha alama kubwa katika jamii. Tanzania tunaye mtu kama Hayati Baba wa Taifa Mwl. Julius K. Nyerere, Bibi Titi Mohamed, Leonard Mengi na wengine wengi. Hawa na wengine wengi ukiwa taja leo Tanzania utasikia sifa kedekede zikiwahusu na hasa katika maeneo mawili uwajibikaji na utawala bora.

Katika hali ya kusikitisha dunia kote, Viongozi na watu wa Kariba hii wanaendelea kuwa adhimu siku hadi siku kiasi ambacho jamii imeendelea kuathiriwa na viongozi na rasilimali watu ambao hawatekelezi wajibu wao ipasavyo. Swali ni Je, Watu wa Kariba hii wamepotelea wapi? Ni dhahiri kuwa familia kama kitovu cha kujenga maadili, uwajibikaji na misingi ya kujiongoza na kuongoza wengine zina majibu kuhusu swali hili kuliko chombo kingine chochote. Familia inaweza kuchangia kuleta mabadiliko chanya katika jamii kupitia malezi bora ya Watoto yanayotoa mafunzo ya uwajibikaji na kuendeleza maadili ya utawala bora.​

Malezi ya familia yanaweza kuhamasisha uwajibikaji na utawala bora endapo tutajenga familia kuwa;

Chombo cha kulea maadili na Mfano Bora:

Kizazi cha karne ya 21 kinauliza, hivi rushwa na ufisadi vitaisha lini? Jibu sahihi lipo kwa wazazi wa kizazi hiki kwani bila wao kufanya maamuzi hali ya rushwa na ufisadi itazidi kuliweka taifa letu katika hali mbaya zaidi. Familia ni lazima iwe na kanuni za maadili ambazo zinakataa vitendo vya ufisadi na rushwa kwa kuweka mipaka na kuchukua hatua za kuzuia ufisadi na ukiukwaji wa maadili ndani ya familia. “Watoto ni muhimu kujengewa uwelewa kuwa fedha na mali siyo kila kitu, na kwamba heshima na sifa njema ni muhimu zaidi.” Hii itabadilisha mtazamo wa watoto kuhusu ufisadi. Kwa kufundisha maadili mema na kuishi kwa kuzingatia kanuni za uadilifu, watoto watajifunza umuhimu wa kuwa wakweli na waadilifu katika maisha yao yote. Watoto wakikua katika mazingira yanayohimiza maadili haya, watakuwa viongozi bora na watu wanaojitolea kwa jamii.​

Jukwaa la mazungumzo na majadiliano.

Ni nadra sana kwa familia zetu za kiafrika kumpa mtoto nafasi ya kutoa maoni yake juu ya jambo la kifamilia. Familia inapaswa kuwaweza Watoto kuwa na fikra tunduizi kwa kuwapa nafasi ya kuchangia katika mambo yanayohusu familia. Kupitia mawasiliano wazi na familia kushirikisha watoto katika majukumu ya kila siku, watoto watapata ujuzi wa uwazi na uwajibikaji. Wazazi wapaswa kuwapa watoto fursa ya kutoa maoni yao na kujisikia sehemu ya maamuzi ya familia, itawajengea utayari wa kubeba uwajibikaji katika matendo yao. Zaidi ya kutoa maoni, Watoto watajifunza masuala ya kijamii na kisiasa jambo ambalo litawafanya kufahamu changamoto na fursa zilizopo katika jamii.​

Chombo kinacholea Utamaduni wa Kushirikiana na Kuaminiana:

Kushirikiana na kuaminiana ni muhimu katika familia na jamii kwa ujumla. Kupitia kuaminiana na kushirikiana, watoto watapata uelewa wa thamani ya kuwa na uhusiano wa kutegemeana na kuaminiana na wengine, na hivyo kudumisha umoja, mshikamano na amani ambazo ndizo tunu za kuimarisha uwajibikaji na utawala bora. Familia inaweza kuhimiza watoto kuchukua hatua hizi za kijamii kwa kushirikiana katika miradi ya maendeleo na kusaidia jamii zao. Kupitia kujitolea na kushirikiana katika shughuli za kijamii, watoto watajifunza umuhimu wa kujali wengine na kuhakikisha kuwa fedha na rasilimali za umma zinatumika vizuri.​

Chombo cha kukuza uwajibikaji.

Familia kwa kushirikiana na taasisi nyingine za kijamii kama shule na serikali inajukumu la kuwafundisha watoto kuhusu uwajibikaji. Watoto wanapaswa kuhimizwa kufanya kazi kwa bidii na kwa uadilifu katika masomo yao na kazi zao za baadaye. Kuelewa kuwa mafanikio yanategemea juhudi za dhati na siyo njia za mkato, itawapa moyo wa kufanya kazi kwa bidii na kuepuka vitendo vya ufisadi na rushwa. Kupewa majukumu ndani ya familia huwajenga watoto kuwa na uwajibikaji na kuona umuhimu wa kushiriki katika maendeleo ya familia yao. Kupitia mfano wa wazazi na walezi, watoto hujifunza jinsi ya kusimamia rasilimali, kama vile pesa na mali. Kupanga matumizi na kuonyesha uwazi kuhusu masuala ya fedha huwajengea watoto utambuzi wa thamani ya rasilimali na jinsi ya kuzitumia kwa manufaa ya familia na jamii kwa ujumla.​

Chombo cha kufundisha demokrasia na utawala bora

Familia inaweza kutoa elimu kwa watoto kuhusu umuhimu wa kushiriki katika shughuli za kijamii na za kisiasa ili kuwajengea tabia ya kufuatilia na kubaini changamoto zinahusu jamii yao. Familia inawajibu wa kuhamasisha ushiriki wa vijana katika majadiliano na mazungumzo kuhusu masuala ya kijamii na kisiasa ili kuwajengea watoto ufahamu na mtazamo wa uwajibikaji na utawala bora. Pia familia inawajibu wa kuhamasisha vijana kushiriki katika chaguzi za serikali za mitaa na za kitaifa. Vijana wanapaswa kupewa haki ya kugombea au kuchagua viongozi wanaowakilisha maslahi yao katika nafasi za siasa kuanzia ngazi ya kifamilia.​

HITIMISHO.

Kama familia, kujenga jiko la mapishi ya uwajibikaji na utawala bora kunahitaji kujitolea na kufanya kazi kwa pamoja. Kila mwanafamilia ana jukumu katika kuhamasisha na kudumisha misingi hii. Kwa kufanya hivyo, tunaweza kuunda jamii zenye uwajibikaji, haki, na maendeleo endelevu kwa siku za usoni. Familia inaweza kuwa chombo cha kuleta mabadiliko chanya katika familia zetu na hatimaye katika jamii nzima. Kwa kuweka msingi imara wa uwajibikaji na utawala bora, tunaweza kuunda jamii yenye amani, maendeleo, na usawa.​

KUMBUKUMBU ZA REJEA.

Julius K. Nyerere, Uhuru na Umoja. Chambuzi kutoka katika machapisho na hotuba 1952-65. (London: Chuo kikuu cha Oxford, 1966 (366p.).​
Kaka unajua sana 👏
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom