Fahamu Mbinu na vifaa vilivyotumika kutoa adhabu kwa wahalifu enzi za zamani. (Ancient torture methods)

Bob Maxwell

JF-Expert Member
May 16, 2021
279
513
Katika historia, watawala walitumia mbinu kali za adhabu kwa lengo la kuadhibu maadui zao pamoja na wale walio tekeleza matukio ya kihalifu. Pia walitumia mbinu hizo kama njia ya kuwafanya wahalifu hao kusema na kutaja wenzao ambao walihusika katika uhalifu huo.

Ancient rome, Greek, China, ni mojawapo ya sehemu ambazo mbinu hizi zilitumika kwa kiasi kikubwa.

Zifuatazo ni mojawapo ya mbinu maarufu kuwahi kutumika katika historia;-

1. The Brazen Bull
Hii ni mbinu ya mateso ambayo kwa kiasi kikubwa ilitumiwa sana katika medieval era au dark ages katika 6th century BCE. Hapa iliundwa sanamu mfano wa n'gombe kwa kutumia material ya chuma ambayo ndani yake kuna nafasi inayo tosha mwili wa mtu mzima.

Mtuhumiwa hufungwa kamba mikono na miguu kisha huwekwa ndani ya n'gombe huyo. Moto mkubwa utawasha mahali ambapo n'gombe amewekwa, yani kwa upande wa chini.

Baada ya kumuweka mtu ndani ya tumbo la huyo n'gome, chuma kinapata moto mkali mpaka huanza kubadilika rangi yani kuwa nyekundu.

Jamaa anaanza kuungua na kuiva, hupiga makelele ambayo sauti hutokea katika matundu ya mdomo wa ngombe na kutoa mlio unao fanana na ngombe halisi.

1715141622888.png


2. The judas cradie
Hichi nikifaa ambacho huchongwa katika umbo la pyramid yenye ncha kali, mtuhumwa hukalishwa juu ya kifaa hichi akiwa hajavaa nguo au kizuizi chochote na kufungwa kamba kwa lengo la kubanwa na kushindwa kutoka.

Miguu hufungwa vitu vizito ili uzito wa mwili uelemee upande wa chini. Ncha hiyo kali huanza kumtoboa jamaa mpaka kufikia katikati mwa tumbo lake na kupelekea kifo.

Pia walihakikisha jamaa wanamuweka au kumkalisha juu ya ncha kwa kuhakikisha sehem za nyuma zimelenga vyema ncha ya kifaa hicho.

1715135190617.png


3. Rat torture
Mbinu hii imekuwa maarufu sana na hata imewashawishi baadhi ya waandaaji wa movies kuitumia katika kazi zao. Katika zoezi hili hutengenezwa cage au kifaa ambacho panya mkubwa atafungwa ndani yake.

Mtuhumiwa hulazwa katika meza na kufungwa vyema kamba katika mikono na miguu yake.

Cage hiyo ambayo panya yupo kwa ndani, inafungwa kifuani mwa jamaa huku upade wa chini ukiwa wazi, yani panya husimama katika kifua cha jamaa.

Kwakua cage huundwa kwa chuma basi wanaiwekea moto kwa juu ili panya aanze kuhisi moto na kufurukuta. Panya huanza kuhangaika na mwisho huamua kutoboa kifua cha jamaa kwa lengo la kutafuta njia ya kutoka.

Mateso na maumivu makali humpata kadri panya anavyo jaribu kutoboa kifua chake. Wakati mwingine mbinu hii hutumika kwa kuweka cage katika uso wa mtuhumiwa.

1715136281857.png


4. Bamboo torture
Mbinu hii ilitumiwa sana na Japanese empire katika wakati wa second world war. Bamboo ni mmea ambao huchipua kwa kasi ya centimeters 4 kwa saa. Mtuhumiwa hukalishwa katika mmea hua pale ambapo unakuwa unaanza kuchipua ardhini.

Mmea huu huanza kukua kwa kasi wakati jamaa ameukalia, huanza kutoboa sehemu za nyuma kisha kuingia ndani ya mwili.

Ukuaji wa mmea ndiyo maumivu huzidi na kufikia hatua ya matawi kuanza kuchomoza katika maeneo mengine ya mwili.

1715136810056.png


5. Chair of torture or iron chair
Hichi ni kiti amabacho kimewekwa misumari yenye ncha kali pande zote, mtuhumiwa hukalishwa na kufungwa vyema pande zote za mwili wake. Mbinu hii ilitumiwa kwa lengo la kuhoji na kulazimisha mtuhumiwa atoe siri au taarifa ambazo inaaminika anazifahamu.

Baada ya kuwekwa katika kiti, misumari huanza kuingia pande tofauti za mwili na kusababisha maumvu na uchungu mkali mno.

Ndugu msomaji jaribu kufikiri wewe ndyo upo katika hali hiyo, je utabaki kimya na kugoma kutoa siri za kambi?

1715137622919.png



6. Chasity Belts
Tafiti zinasema kwamba mbinu hii ilikuwepo kabla ya 15century. Hichi ni kifaa ambacho kiliundwa mahsus kwa ajili ya wanawake. Mwanamke hufungwa kifaa hichi katika sehem zake za kiuno kama vile nguo ya ndani.

Inasemekana kwamba lengo la mbinu hii ni kupima na kutunza uaminifu wa wanawake kwa waume zao. Pindi Knight anapotoka na kwenda vitani kupigania nchi, mwanamke wake hufungwa kifaa hichi kwa lengo la kutunza kitumbua kisiingie mchanga.

Imekuwepo mijadala kwa baadhi ya wana historia kwamba kifaa hichi kilitumika kwaajili ya adhabu au kulinda uaminifu wa mke kwa mume na jamii kwa ujumla.

1715138720212.png



7. Anti-masturbation armour
katika juhudi za kukomesha vitendo vya kujichua kwa mongoni mwa vijana, kifaa hichi kiliundwa rasmi katika miaka ya 19century. Kwa wale walio bainika kujihusisha na mchezo huo, wali kamatwa na kufungwa kifaa maalumu katika maumbile yao.

Kifaa hicho kiliweza kuzuia jaribio la kutaka kujichua japo wakati mwingine huleta maumivu makali kwa waathirika.

Mdau, unadhani mbinu hii inapaswa kurejeshwa katika dunia ya leo kutokana na kukua kwa tabia hii kwa baadhi vijana?

1715142624420.png




Torture methods zipo nyingi sana, natumai hizo zinatosha kwa leo na endapo utapata muda wa kufanya tafiti, basi ni vyema ukapitia katika vyanzo vingine kupata kufahamu mbinu nyinginezo.
Kwa maoni yako ndugu msojami, unadhani ni ipi ambayo ni hatari na yenye mateso makali kati ya mbinu tajwa hapo juu?
 

Attachments

  • 1715135285789.png
    1715135285789.png
    83.3 KB · Views: 4
  • 1715136219474.png
    1715136219474.png
    98.5 KB · Views: 5
Back
Top Bottom