EWURA yawataka Wadau wa Gesi Asilia kufuata Sheria

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,884
12,133
Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), leo Tar. 15/05/2023, imetoa semina kwa wadau wenye vituo vya kujaza gesi asilia iliyokandamizwa (CNG) kwenye magari, karakana za kuweka mifumo ya gesi kwenye magari, waidhinishaji na wakaguzi wa mifumo ya gesiz hiyo na kuwataka kufanyakazi kwa kufuata sheria, kanuni na miongozo ili kuhakikisha usalama wa huduma,mali, watu na mazingira.

Wadau hao pia wametakiwa kujisajili katika Mfumo wa Kitaifa wa Taarifa wa Petroli na Gesi Nchini (NPGIS), unaoratibiwa na EWURA ili kuwasilisha taarifa za utendaji wao wa kila siku kwa lengo la kufuatilia mwenendo wa maendeleo ya sekta ya gesi asilia nchini zitakazoisaidia EWURA kufanya maamuzi ya kiudhibiti na katika kuishauri Serikali.

Shirika la Viwango Tanzania (TBS), ni miongoni mwa waliohudhuria semina hiyo, ambapo waliwataka washiriki kuzingatia viwango vya ubora katika kuidhinisha mifumo ya gesi, kukagua magari yanayotumia gesi asilia, pamoja na kuwa na nyenzo sahihi za kazi.

Kwa upande wa Bodi ya Usajili wa Wakandarasi (CRB) walieleza kuhusu utaratibu wa kufuatwa katika usajili wa karakana za kuweka mifumo ya gesi asilia kwenye magari. Aidha wawakilishi kutoka Chuo kikuu cha Dar es Salaam pia walihudhuria semina hiyo.

Hadi sasa vituo vya kujaza gesi asilia kwenye magari ni pamoja na PAET Filling Station, iliyopo Ubungo, Anric Gas Filling Station, Tazara na Dangote Filling Station kwa matumizi binafsi kilichopo Mtwara.

Karakana zinazinazojihusisha na kuhuisha mfumo wa magari ili yaweze kutumia gesi asilia ni pamoja na UDSM & Triangle Energy (T) Ltd (UDSM), Dangote Cement Factory for own use (Mtwara), Darajani Garage (Ubungo- DSM), DIT & Anric Gas Technology (DIT), BQ Contractors (Goda- DSM).

EWURA ina jukumu la kudhibiti mkondo wa Chini na Kati wa Shughuliza gesi asilia zinazojumuisha usindikaji, usafirishaji, uhifadhi na usambazaji wa gesi asilia Tanzania Bara kwa kutoa vibali vya ujenzi, leseni, bei na kuangalia ubora wa miundombinu ya kutolea huduma.
IMG-20230515-WA0013.jpg
IMG-20230515-WA0011(1).jpg
IMG-20230515-WA0008.jpg
IMG-20230515-WA0012.jpg
IMG-20230515-WA0010.jpg
IMG-20230515-WA0009.jpg
IMG-20230515-WA0011.jpg
 
Siku hii nchi ikijua madhara ya udhibiti uliopitiliza ndo siku tutatoka. Watu wanaona sifa kudhibiti kila kona kuliko biashara kufanyika. CNG kwa magari imeanza karibia miaka 10 sasa, cha ajabu magari yaliyobadilishwa ni machache mno, hata hao EWURA na TPDC bado hawatumii gesi, wameshikilia udhibiti.
 
EWURA WAPUMBAFU SANA! ni aibu kwa Nchi.kuwa na vituo viwili tu kujazia Gesi halafu tuna hiyo raslimali imejaa tele!
Mkurugenz wa Ewura angefukuzwa tu maana anasumbua sana kutoa vibali vya gesi! ni Uhaini anaoufanya
 
umekuwa consistent sana kuwalaum ewura nimeweka mfumio wa gesi na changamoto kubwa ni ujazaji , niliwauliza pan africa ubungo kwanii hawaongezi pump wakasema ewura haijawapa kibali.
 
Siku hii nchi ikijua madhara ya udhibiti uliopitiliza ndo siku tutatoka. Watu wanaona sifa kudhibiti kila kona kuliko biashara kufanyika. CNG kwa magari imeanza karibia miaka 10 sasa, cha ajabu magari yaliyobadilishwa ni machache mno, hata hao EWURA na TPDC bado hawatumii gesi, wameshikilia udhibiti.
Kazi za watu mjini hizo
 
EWURA WAPUMBAFU SANA! ni aibu kwa Nchi.kuwa na vituo viwili tu kujazia Gesi halafu tuna hiyo raslimali imejaa tele!
Mkurugenz wa Ewura angefukuzwa tu maana anasumbua sana kutoa vibali vya gesi! ni Uhaini anaoufanya
Mume wa Tulia,Tulia kama tulia.
 
Back
Top Bottom