Shining Light
JF-Expert Member
- Jan 8, 2024
- 327
- 419
Sober House zipo 40 nchini, na tatizo la waathirika wa dawa za kulevya ni wengi sana, ila huwa wanakamatwa tu bila kutibiwa. Hivyo serikali inabidi ifanye mipango mizuri wa kuwekeza katika hizi sober house zilikuwepo na hata kuanzisha zingine ili kuweza kutibu waathirika wa dawa hizo za kulevya Nchini na sio tu kuwakamata.
Kwa mtazamo wangu nahisi jambo hili ni muhimu sana kuwekeza katika rehabilition centers itasaidia sana watu wengi walioathirika, kwa sababu inaweza saidia kuwapa waarithika hawa matumaini na purpose katika maisha yao tena, hizi center hazitibu tu kwa tiba bali kushirikishwa katika elimu mbalimbali na kuoneshwa namna kwa wao kutumia madawa inaathiri vipi watu wengine pia.