Elimu ya dini iwekewe mkazo mashuleni na iwe ni somo la lazima kuanzia shule ya msingi hadi chuo kikuu

Maadili hutoa maana au muundo dhahiri wa maisha ya mwanaadamu, Maadili ni kanuni fulani za msingi ambazo zinapaswa kushikiliwa katika maisha. Maisha ya kuishi bila maadili hatimaye mtu ataishia kuhisi kutoridhika, kuhisi mwenye hatia na huzuni.

Kama mtoto asipolelewa bila sheria ni haraka zaidi kuharibika na kuharibiwa na jamii yake.

Maadili ndio yanatoa hekima ya kutofautisha kati ya lililo jema na lisilo sahihi. Uelewa wa kile kilicho sawa na kibaya (hayo ndio maadili).

Vituo vya kufundisha maadili ni Nyumbani, Shuleni na Vituo vya ibada (Misikiti, Makanisa, Madrasa na Sunday School). Kwasasa asilimia kubwa Majumbani kwetu hakuna maadili yanayofundishwa kwasababu wazazi hawana muda na watoto, wazazi wote wawili wako busy kutafuta pesa.

Hivyo sehemu inayotegemewa zaidi ni Vituo vya ibada ambapo napo kuna yumba sana hakutoi nafasi ya kutosha, nafasi iliyobaki pekee ipo Mashuleni ambapo mtoto anatumia muda mwingi zaidi huko shuleni.

Ajabu ni kwamba huko Shuleni somo la dini ambalo ndio kitovu cha maadili lipo tu kama sehemu ya mapumziko na halihesabiwi na kuwekewa uzito ipasavyo.

Ingawa nyakati za sasa watu hawalipi uzito mkubwa swala la maadili katika maisha yao. Lakini sababu kubwa ya kuporomoka kwake ni watu kuacha misingi ya dini zao na mafundisho ya imani zao, Serikali kufuta masomo ya dini na kutoyapa kipaombele katika kumpandisha au kumshusha mwanafunzi kitaaluma.

Wazazi sasa wanazingatia zaidi ujuzi wa watoto wao wa kielimu au kifedha, Lakini wakisahau kumfanya kijana wao kuwa "binadamu" mzuri, kwamba kuzingatia maadili yao kutawafanya kufanikiwa zaidi.

Ikiwa masomo ya dini yatapewa kipaombele mashuleni na kujumuishwa katika kumfelisha au kumfaulisha mwanafunzi bila shaka watoto watahudhuria Sunday School na Madrasa kwa wingi, bila shaka wazazi watawahimiza watoto wao kwenda Sunday school na Madrasa ambako huko ndiko maadili hufundishwa zaidi kuliko hata nyumbani.

Ni hatari sana binaadamu kuishi bila hofu, ni hatari sana binaadamu kuishi bila kujali chochote wala lolote. Maadili pekee ndio humpa hofu mwanaadamu, ni maadili pekee ndio humuwekea mipaka mwanaadamu.

Vijana wakiwa na maadili wizi na unyang'anyi vitapungua, umalaya na ukahaba vitapungua, wanawake watapunguza kutembea uchi, mashoga watapungua, mauaji yatapungua, talaka zitapungua, unyanyasaji utapungua, rushwa itapungua, ufisadi utapungua, ulevi utapungua, magerezani watu watapungua na bajeti ya serikali ya kukabiliana na uhalifu itapungua.

BAKIIF Islamic
Kimara, Dar Es Salaam


View attachment 2940837
Na asiye na dini afundishwe nini? Nafikiri kuwe na mtaala wa uraia mwema, huko wafundishwe Katiba yote, haki na wajibu wao, mambo yanayochukuliwa kama ni uhalifu, jinai, uhaini n.k. Upendo, nidhamu kwa kila mtu, kila jambo na kujitolea na ushirikiano.
 
Dini haijawahi kuacha mtu salama, Historically dini zimeua millions na zinaendelea kuua, kuanzia crusades mpaka leo Gaza chanzo ni dini tuu, tafadhari kaeni na dini zenu misikitini au makanisani kwenu, tukitaka tutakuja kujifunza huko
 
Na mkiongea habari za dini mpaka mbalance ukiristo na uislam kana kwamba mtoa maada una dini mbili

Unaogopa nini kuelezea maadili katika nyanja ya dini yako, nijuavyo maadili ni suala pana kuna maadhi ya dini hazina maadili naturally bora hata mila na tamaduni nyingine ambazo hazihusiani na dini

Mtoa mada kuwa specific
Kwasababu uislamu na Ukristo ndio dini kuu
 
Dini inahusika na mahusiano kati ya Mungu na mtu binafsi. Maadili hutegemea hiari na dini juu ya hisia za kiakili. Katika maendeleo ya mwanadamu, maadili na dini vyote viwili hukua pamoja na kuathiriana.
Kwa ni lazima wote twende mbinguni? Hamuoni kama mkienda nyie inatosha? Mbona mnapenda watu wengine nao wakajazane kwenye hiyo pepo yenu?
 
Back
Top Bottom