Elections 2015 Edward Lowassa sio lazima yeye tu ndiye awe Rais wetu 2015, Rais wetu wa 2015 ni...

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,615
113,833
...Yule Aliyepangiwa na Mungu!.
Wanabodi,
2015 ndio hii, mimi ni miongoni mwa tuliojibainisha wazi, kumkubali Edward Lowassa as "The One and Only" Best President this country can ever have apart from Nyerere!. Hii haina maana Lowassa ndio lazima yeye ndiye awe rais wetu, bali rais wa Tanzania kwa 2015 ni yule tuu, aliyepangiwa na Mungu, sio lazima awe ni Lowassa, ila kwa vile mpaka sasa, Mungu bado hajatuambia amempangia nani awe rais wetu kwa mwaka 2015, asuming hoja hii
Uchaguzi 2015 - Mgombea wa Urais Kwa tiketi ya CCM, 2015 "Could Be ... sio mpango wa Mungu, kama aliepangiwa na Mungu ni Edward Lowassa, then, Lowassa ni lazima awe rais wetu 2015!, lakini kama hajapangiwa, then, rais wa Tanzania kwa 2015 ni yule tuu aliyepangwa na Mungu!.
Nakiri nimekuwa inspred kuandika mada hii, kufuaria mchango wa mwana jf huyu kwenye uzi fulani!
Kafanya jambo gani la kutukuka huyu Pasco katika tasnia ya habari ? Pasco ni mshereheshaji wa maonyesho ya saba saba, zaidi ya hapo alikuwa spokesperson wa Lowasa lakini loyalty yake kwa Lowasa imeisha inaonekana mzee wa mvi kawa na mkono wa birika, najaribu kutafuta baada ya lowasa sijui anamlamba nani miguu.
Mkuu So Notorious, kwanza nakubaliana na wewe, Pasco huyu unayemjua sasa ni mshereheshaji tuu wa maonyesho ya Saba Saba na Nanenane, kwa nyie watu wa kisasa. Pasco aliondoka rasmi newsroom mwaka 2002 na tangu hapo hajawahi kuajiriwa tena, sasa amebaki kama Mwandishi wa habari wa kujitegemea kwa kujitolea. Sasa ili kumjua Pasco, rudisha mawazo yako mwaka 2002 ulikuwa level gani, na kuanzia hapo ndipo turudi nyuma!.

Pasco hajawahi kuwa spokesperson wa Lowassa, hajawahi kufanya kazi yoyote kwa Lowassa, hajawahi kuhudhuria press conference yoyote ya Lowassa, hajawahi kuandika au kuripoti news yoyote ya Lowassa na wala hajawahi kufika Monduli, au kuhudhuria zile sherehe maarufu za Monduli!.
Kitu pekee alichofanya Pasco humu jf, ni kumkubali Lowassa, katika ukweli dhahiri usio na mawaa yoyote kuwa ndani ya CCM, Edward Ngoyai Lowassa, ndie the one and only best presidential material candidate CCM has, na ikitokea asipitishwe, then asipitishwe kwa haki, vinginevyo patachimbika!.

Hata hivyo kumkubali kwangu Lowassa, ni personal tuu, tena kwa kujitolea, siko Team Lowassa!, sijawahi kuwepo!, wala sijawahi kupokea hata senti moja kutoka kwa Lowassa!, hivyo hoja ya kumlamba mtu miguu kwangu haipo!, ningekuwa mlamba miguu, ningemlamba Mkapa ambaye mtoto wake nimesoma naye darasa moja sekondari kwa miaka minne!, wakati kwa wengine wote kwao Mkapa ni rais, mimi kwangu, Mkapa ni Baba fulani na nimekwenda kwake kama baba wa rafiki yangu!. Ningekuwa ni mtu wa kujikomba komba na kujipendekeza, ningejikomba kwa Riz 1, nimekutana nae UDSM na tunaiva sana, hivyo angenishika mkono anipeleke kwa mshure wake!, why nilambe miguu ya mtu?!. Mimi niko kwenye lile kundi la "Maskini Jeuri" kama kina "Kozi mwana mandanda, kulala njaa kupenda!".
Ila pia nina mtu wangu wa karibu kwenye Team Lowassa, hii ndio timu yenye mkono mrefu kuliko team nyingine yoyote so far!. Tatizo langu na timu hii ni moja tuu, hali ya Afya ya Mzee wetu!, kwa vile rais wa Tanzania 2015, ameishachaguliwa na Mungu, and not necessarily ni Lowassa, then, alilolipanga Mungu, binadamu hawezi kulipangua!, ndio maana kule nyuma Mungu aliwahi kufanya muujiza wa "Jiwe walilolikataa waashi likafanywa kuwa jiwe kuu la pembeni!", na kuna mtu alielezwa kuwa "Wewe ni mwamba, na juu ya mwamba huu, nitalijenga taifa langu!", kwa Tanzania hapa tulipofika, tuna mwamba mmoja tuu, "Mwamba wa Kaskazini!" lazima awe!, na asipokuwa basi itakuwa Mungu hakumpangia!, hivyo atakayekuwa rais wetu, 2015, ni yule tuu Mungu aliyempangia and not necessarily ata make the best president kwa sababu the best presidential material candidate is one and only Lowassa, ila kwa CCM, usually they don't pick the best, Mwinyi was not the best lakini ndie Mungu alimpangia, Mkapa was not the best lakini ndie Mungu alimpangia, JK pia was not the best lakini ndilo chaguo la Mungu, hivyo whoever atakayekuwa rais wetu 2015, huyo ndie chaguo la Mungu kwa Tanzania yetu!.
Wasalaam!.
Pasco
 
....

Hata hivyo kumkubali kwangu Lowassa, ni personal tuu, tena kwa kujitolea, siko Team Lowassa!, sijawahi kuwepo!, wala sijawahi kupokea hata senti moja kutoka kwa Lowassa!,

.....

Ila pia nina mtu wangu wa karibu kwenye Team Lowassa, hii ndio timu yenye mkono mrefu kuliko team nyingine yoyote so far!.

.....

Wasalaam!.

Pasco.
Unajikanganya Pasco, wewe hela ya lowassa ushawahi kula au bado? Unasifia mtu wako muhimu kuwepo kwenye timu yenye hela, then eti hujawahi kuila hiyo hela, how?

Usitufanye watoto kaka!!
 
Kama Mungu atatupangia rais mwenye tuhuma za wizi tangu ujana wake, na tena mgonjwa..huyo Mungu atakuwa mwenyekiti wa CCM anaekutana na wezi kwenye kiti cha enzi (ikulu)
Kuna vitu Mungu anavifanya ili tuu kuuthihirisha utukufu wake!, kama pale alipoweza kulifanya "jiwe walilolikataa waashi, likafanywa kuwa jiwe kuu la pembeni!", au juu ya mwamba ambapo watu hawawezi kujenga!, YEYE akawaambia "Juu ya Mwamba Huu, Nitalijenga Kanisa Langu!", lisilowezekana kwa mwanadamu, kwa Mungu linawezekana!.

Pasco
 
EL akipitishwa na ccm kwa ushabiki; tena kwa sababu ya vijisent tu! Tutakuwa tumepitisha dalali aliyepindukia kwenye mambo ya ufisadi. Nchi ilipo kwa sasa inataka rais msafi asiye na makundi.
 
Nakubaliana na ww Pasco asilimia mia. .. na ikitokea asipitishwe, then asipitishwe kwa haki, vinginevyo patachimbika!.-
 
Unajikanganya Pasco, wewe hela ya lowassa ushawahi kula au bado? Unasifia mtu wako muhimu kuwepo kwenye timu yenye hela, then eti hujawahi kuila hiyo hela, how?

Usitufanye watoto kaka!!
Mkuu Shark, ukweli ndio huo!, ni kweli team EL sio ina hela, bali in a mihela!, na mimi lazima nikiri, Pasco ni masikini wa kutupa!, ila kuna aina mbalimbali za masikini, na fedha sio kila kitu!, mimi ni ile type ya masikini tunaitwa masikini jeuri!, yaani ninakaa na jirani tajiri, jirani yangu anatupa mkate jalalani nje kwangu, huku mimi sina chakula kabisa!, kuliko kuuokota huo mkate, ni bora nitalala na njaa yangu. Sisi ndio tunaitwa masikini jeuri!, nilikuwa na access na Mkapa, ningemtumia kutoka, lakini sijamtumia!, nina access na JK, simtumii, naendelea na maisha yangu kwenye lindi la umasikini wa kutupa uliotopea, but I'm happy kuliko kuwa ombaomba tajiri!.

Watu wa aina yangu tupo, tena tupo wengi tuu!.

Pasco.
 
Kuna vitu Mungu anavifanya ili tuu kuuthihirisha utukufu wake!, kama pale alipoweza kulifanya "jiwe walilolikataa waashi, likafanywa kuwa jiwe kuu la pembeni!", au juu ya mwamba ambapo watu hawawezi kujenga!, YEYE akawaambia "Juu ya Mwamba Huu, Nitalijenga Kanisa Langu!", lisilowezekana kwa mwanadamu, kwa Mungu linawezekana!.

Pasco
Natamani nimuone huyu Pasco ambaye anaandika kinabii. ni kweli Rais ajaye atatoka kusini na sio Lowassa.
 
Nakubaliana na ww Pasco asilimia mia. .. na ikitokea asipitishwe, then asipitishwe kwa haki, vinginevyo patachimbika!.-
Mkuu Bucho, CCM ni chama huru, kiko huru kujipangia taratibu zake za kupata viongozi wake kwa uhuru na haki bila kuingiliwa wala kushinikizwa, ila utaratibu huo uwe wa haki!, mfano Sitta alikuwa ni the best speaker this country had ever had apart from Chief Adam Sapi Mkwawa, Sitta akawa mwiba kwa serikali ya CCM, wakataka kumfukuza, wakashtuki chama kitaumia!, wakaamua next speaker lazima awe wa jinsia ya kike!, that was it!.

Vikao vya maamuzi kuhusu utaratibu wa CCM bado havijakaa, wanaweza as well kuamua kwa 2015, CCM imeamua kumsimamisha mgombea kutoka Zanzibar!, au wameamua mgombea awe wa jinsia ya kike!, that will be it!, lakini hawawezi kumuengua Lowasaa kwa mizengwe yoyote na CCM ikabaki Salama!, patajimbika!.Pasco
 
Natamani nimuone huyu Pasco ambaye anaandika kinabii. ni kweli Rais ajaye atatoka kusini na sio Lowassa.
Mkuu Kanyamgo, utaniona sana tuu, kwa sababu very soon from now, narudi front, kwenye uwanja wa mapambano tena nitakuwa mstari mbele, front line kwenye line of fire!, ama zao, ama zetu, mpaka kieleweke!.Pasco.
 
Mkuu Shark, ukweli ndio huo!, ni kweli team EL sio ina hela, bali in a mihela!, na mimi lazima nikiri, Pasco ni masikini wa kutupa!, ila kuna aina mbalimbali za masikini, na fedha sio kila kitu!, mimi ni ile type ya masikini tunaitwa masikini jeuri!, yaani ninakaa na jirani tajiri, jirani yangu anatupa mkate jalalani nje kwangu, huku mimi sina chakula kabisa!, kuliko kuuokota huo mkate, ni bora nitalala na njaa yangu. Sisi ndio tunaitwa masikini jeuri!, nilikuwa na access na Mkapa, ningemtumia kutoka, lakini sijamtumia!, nina access na JK, simtumii, naendelea na maisha yangu kwenye lindi la umasikini wa kutupa uliotopea, but I'm happy kuliko kuwa ombaomba tajiri!.

Watu wa aina yangu tupo, tena tupo wengi tuu!.

Pasco.

That is the spirit, mtu yeyote mwenye akili hawezi kuwa tajiri ombaomba, we need to learn living within our means. hii kanuni ya kujipendekeza ili kuishi ndio imeliangamiza TAIFA letu kwa kutupa watu wasio na uwezo sehemu mbalimbali nyeti za maamuzi ya taifa hili, just because umejitoa utu na kujipendekeza unakuwa rewarded na nafasi fulani. Tuache hiii tabia else tutaufilisi nchi yetu.
 
Pasco mkuu nakupa taji kwa kuchanganya na kujichanganya kwa makusudi. Kuwa tu wakwanza kulijuza jamvi kwamba team Lowassa sasa ndani ya PCR (palliative care room) kwasababu kuu tatu.

Moja timu hii imegundua kwamba chama hakipo pamoja nao na hii imewekwa wazi na jinsi Lowassa alivyofanyiwa Songea na wakuu wa chama huku hotuba ya JK ikimlenga moja kwa moja. Tathmini ya team Lowassa kwa hotuba ya JK haikufurahisha team na ndio maana sasa mkakati ni kutanganza nia kabla au siku chache baada ya adhabu yake kwisha ili kushinikiza chama kikubali kwa kuuandaa umma.

Pili, ni dhaihiri rais ajaye ni yule ambae hatatiliwa shaka kama ambavyo JK amesema kwenye hotuba Songea na tayari team husika imepigwa nusu-kaputi kwa criteria hii maana mtu wao ndio anayeongoza kwa kuwa na mashaka mengi kupita mgombea yeyote anayetarajiwa. Well labda kamzidi Chenge...sijui.

Tatu UKAWA wameamua kutompokea Lowassa endapo atahasi ccm kwasababu kwamba hawataeleweka kwa umma kwa kumpokea mtu waliyemtaja miaka ya nyuma kwamba ni Fisadi Papa. Hii inaondoa plan B ya Lowassa maana team inajikuta ipo kati ya nyundo na jiwe gumu.

Sasa mkuu Pasco amesoma upepo na kutoka na gear ya afya mbaya kana kwamba ubaya wa afya yake umeanza jana.
 
Mkuu Shark, ukweli ndio huo!, ni kweli team EL sio ina hela, bali in a mihela!, na mimi lazima nikiri, Pasco ni masikini wa kutupa!, ila kuna aina mbalimbali za masikini, na fedha sio kila kitu!, mimi ni ile type ya masikini tunaitwa masikini jeuri!, yaani ninakaa na jirani tajiri, jirani yangu anatupa mkate jalalani nje kwangu, huku mimi sina chakula kabisa!, kuliko kuuokota huo mkate, ni bora nitalala na njaa yangu.

Sisi ndio tunaitwa masikini jeuri!, nilikuwa na access na Mkapa, ningemtumia kutoka, lakini sijamtumia!, nina access na JK, simtumii, naendelea na maisha yangu kwenye lindi la umasikini wa kutupa uliotopea, but I'm happy kuliko kuwa ombaomba tajiri!.

Watu wa aina yangu tupo, tena tupo wengi tuu!.

Pasco.

Pasco,

Hizi Habari kua umejitoa #TeamLowassa na ndio maana siku hizi unamuandika vibaya sababu tu umenyinwa kile cheo alichonacho Abubakar Liongo ni kweli?
 
Nakubaliana na ww Pasco asilimia mia. .. na ikitokea asipitishwe, then asipitishwe kwa haki, vinginevyo patachimbika!.-
Hii lugha ya patachimbika ni hatali kwa mustakabali wa taifa letu. Kama kweli kachaguliwa na Mungu, kuna binadamu wa kuzuia? Kama Lowasa hatapitishwa, basi ujue kuwa amekataliwa na Mungu
 
Naunga mkono hoja lowasa siyo mtanzania pekee ukichanganya na ufisadi ndiyo kabisa hafai kuwa kiongozi wa taifa hili.
 
Back
Top Bottom