Edo Kumwembe: Fiston Mayele anaumia sana kuona Yanga inafanikiwa bila yeye

Mayele ni mchezaji wa kawaida sana hapa bongo alionekana mchezaji mzuri kwasababu club aliyokua anaichezea ni ya kawaida sana
Alikuwa anazifunga Club za kawaida sana.
Ngao ya jamii anapiga kisha anawageuza tena kwenye ligi kuu anachapa tu.
Anawachapa kama anakomoa anatafuta ndoa kwa lishangazi.
 
Kutoka kwa mchambuzi wa masuala ya soka, Edo Kumwembe ambaye amefunguka sakata la mshambuliajiwa Pyramids Fc ya Misri, Fiston Mayele kuwatupia madongo waajiri wake wa zamani, Klabu ya Yanga.

“Nadhani kuna tabia ambayo Mayele aliificha akiwa Young Africans na sasa ameifichua. Kutaka kuonekana mkubwa na mfalme. Bahati mbaya inamuumiza pia kwamba Young Africans wanasonga mbele bila ya yeye. Huwa inatokea unapoachana na mpenzi wako. Hautaki yamtokee mema mbele ya safari.

Lakini kuna uwezekano mkubwa Mayele anaumwa ugonjwa wa kupenda nyumbani (home sickness). Tayari Tanzania kulishakuwa nyumbani kwake na aina ya maisha ya Tanzania yalimuingia kwelikweli.

Maisha ya uwanjani, mitaani na mitandaoni. Tanzania bado haijamtoka. Bado ipo akilini mwake. Mwili upo Misri, lakini akili ipo Tanzania.

Inawatokea wageni wengi waliowahi kuishi Tanzania. Sio tu wanasoka kama kina Bernard Morrison ambao tunaona kila siku wanazurura Dar es salaam ingawa wanacheza soka la kulipwa Morocco, lakini pia kwa wageni wengine. Hata kuna mabalozi wa nchi za nje hawaishi kurudi kutembea Tanzania baada ya muda wao kuisha," amesema Edo Kumwembe.

-------------------

Kwa bahati mbaya sana nakubaliana na Kumwembe kwa hili. Yanga imekwenda robo fainali bila yeye wakati timu yake imeshia makundi tu; hiyo inaweza kuwa factor moja kuwa Yanga inasonga mbele bila yeye.

Kubwa zaidi ni kwamba maisha ya Tanzania kwa mastaa ni mazuri sana; atakuwa anayamiss sana.
 
Ameandikwa vibaya au imesemwa ukweli?
Tuongee ukweli Mayele anazingua.
Kati ya Mayele na Feisal kwa yaliyotokea nani alifaa kusema ana uhasama na Yanga!?
Unadai Yanga inakutupia majini mbona Feisal yupo hapo Chamazi na yuko fresh!?
FAisal kwa zenji majini yalikozaliwa yanga wamemshindwa,yanga wachawi sana
 
Kutoka kwa mchambuzi wa masuala ya soka, Edo Kumwembe ambaye amefunguka sakata la mshambuliajiwa Pyramids Fc ya Misri, Fiston Mayele kuwatupia madongo waajiri wake wa zamani, Klabu ya Yanga.

“Nadhani kuna tabia ambayo Mayele aliificha akiwa Young Africans na sasa ameifichua. Kutaka kuonekana mkubwa na mfalme. Bahati mbaya inamuumiza pia kwamba Young Africans wanasonga mbele bila ya yeye. Huwa inatokea unapoachana na mpenzi wako. Hautaki yamtokee mema mbele ya safari.

Lakini kuna uwezekano mkubwa Mayele anaumwa ugonjwa wa kupenda nyumbani (home sickness). Tayari Tanzania kulishakuwa nyumbani kwake na aina ya maisha ya Tanzania yalimuingia kwelikweli.

Maisha ya uwanjani, mitaani na mitandaoni. Tanzania bado haijamtoka. Bado ipo akilini mwake. Mwili upo Misri, lakini akili ipo Tanzania.

Inawatokea wageni wengi waliowahi kuishi Tanzania. Sio tu wanasoka kama kina Bernard Morrison ambao tunaona kila siku wanazurura Dar es salaam ingawa wanacheza soka la kulipwa Morocco, lakini pia kwa wageni wengine. Hata kuna mabalozi wa nchi za nje hawaishi kurudi kutembea Tanzania baada ya muda wao kuisha," amesema Edo Kumwembe.

-------------------
Nakazia
 
Mkuu ana changanya kivipi wakati kila mashindano yana vigezo ya timu kushiriki, mfano Champion league ni kombe ambalo washiriki wake % 99 ni mabingwa kutoka kwenye ligi za nchi zao.
Hajielewi mkuu.
Anakwambia kombe la shirikisho sio kombe la CAF.
Kama sio kombe la CAF limeandaliwa na nani??
 
Mayele anatakiwa kuachana na tabia ya uropokaji na pia ajifunze kuishi kama professional player. Hana sababu ya kulumbana na watu asiowajua mitandaoni, na pia kutoa siri za timu alizochezea/anazochezea.

Ikimpendeza, ajikite zaidi kwenye kazi yake ya kucheza mpira.
Naushangaa sana, akiwa Yanga alikuwa mchezaji wa kuigwa ila sasa hata sijui kawaje.
 
Mkuu huo ndo ukweli.. ukijaribu kufatilia hili sakata huwezi kuona popote uongozi wa Yanga umemletea zengwe Mayele
Yanga inapigwa vita sana, kizuri ni kuwa viongozi washajua hili na wana deal nazo vita hizi kisomi sana
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom