Nguruvi3
Platinum Member
- Jun 21, 2010
- 15,419
- 31,439
HISIA ZAJITOKEZA, UTAIFA WATAWALA ''WATANGANYIKA WAKITOA YA MOYONI HAPAKALIKI' WAZANZIBAR WATAWANYIKA, HAWANA KAULI, SASA NGUMI MKONONI
SEHEMU YA I
Ndugu wanaduru Bunge la katiba la CCM au Samwel Sitta linaendelea kwa kuunga unga, likipoteza mvuto maana na thamani. Wajumbe wameacha kazi aliyodai wanaifanya, sasa wageuza ukumbi eneo la mipasho dhidi ya UKAWA
Jitihada za kutoa zawadi ili kuungwa mkono zinaendele. Mwenyekiti Sitta akiahidi kutumia pesa za umma kama mali yake, vifungu nyeti kama cha 1 na 6 vikiwekwa pembeni ili kujadili vile venye mvuto hasa wa kupendeza wazanzibar
Kila kifungu kimejadiliwa kkidhi haja za Wazanzibar ili mradi 2/3 ya nguvu ipatikane. Vifungu ambavyo ni moyo wa katiba vimewekwa kiporo kuchelea Unyeti ''sensitivity' kulivunja bunge la CCM bila UKAWA au jambo jingine.
SINTOFAHAMU ILIANZA SIKU NYINGI
Wazanzibar waliondoka kwao na msimamo wa S3, msimamo uliosimamia mambo mengi yakiwemo kuvunja katiba, kuondoa mambo ya muungano, kupunguza madaraka ya rais wa JMT visiwani n.k.
Ni haki kusema bila kujali CCM au CUF msimamo wa S3 ni wao. Hata kura za maoni ikiwemo maoni ya tume yanaeleza hivyo.
Hulka ya wazanzibar ni wamoja kwa baadhi ya nyakati, lakini huwa wamoja zaidi dhidi ya 'adui' yao Tanganyika. Wznz hukumbwa na kihoro wanapotoka znz. Waliofika Dodoma, umoja wa S3 ukatawanyika. Pandu kificho akisema hakuwemo, waziri wa sheria akilalamika 'tulikubaliana'
UMOJA KATIKA UNAFIKI
Umoja wa wazanzibar una aina za unafiki. Kama tulivyosema, kuvunjika kwa msimamo wa S3 ni dalili moja.
Kujitoa kwa mwanasheria mkuu katika kamati ya uandishi wa katiba ya Sitta, nao unawakilisha unafiki. Maana yake, wapo wanaoamini maafikiano yao kabla, wanaoamini S3 na mkataba bila kujali mrengo wa kisiasa,kwa pamoja hawawezi kusema. Wapo UKAWA wanaosema na CCM wanaotetea mfumo uliopo.
Unafiki una mizizi,ni wznz wanaosema Tanganyika imewageuza koloni, wananyonywa, wanaibiwa na wanateseka ndani ya muungano,waasisi wa muungano wakitukanwa hadharani. CUF wakimshambulia Karume kwa ukatili, CCM&CUF wakimzodoa Nyerere laana .
Ni Wazanzibar wanaodai muungano hauna faida, laiti ingekuwepo nchi za jirani zingeshajiunga Na ni wazanzibar wanaodai, muungano umefunga fursa zao za kukigeuza kisiwa chao kuwa 'pepo' ya Afrika. Madai hayo yakiwemo matusi yanapotolewa, hakuna kiongozi wa CCM au CUF anayesimama kukemea.
Tena wapo wanaorudia maneno kama Nyerere! ilimradi wanazi wao waitikie Laanatullah Hakujatokea kiongozi yoyote kusimama na kukemea dhihaka na kejeli hizo. Leo wanapotokea wazanzibar wakitetea muungano eti kumuenzi Nyerere, duru hatuelewi ni unafiki wa kiwango gani. Kutokana na kutoelewana au kuelewa wanachokizungumzia, hamkani si shwari tena kwa upande wao
Inaendelea sehemu ya II...