nkongu ndasu
JF-Expert Member
- Jan 19, 2013
- 22,532
- 6,613
Uzee hupunguza maarifa? Huyu ndo Slaa niliekuwa namfahamu?
nimeshangaa sana.aise..
Uzee hupunguza maarifa? Huyu ndo Slaa niliekuwa namfahamu?
Hamna mtu mwenye akili timamu atakayeweza kukaa meza moja na lowassa halafu akajiita mzalendo
Aondoke tu, Slaa Slaa!! Yeye dudu gani?
Dr.Slaa tutakufuata popote utakapokwenda.hatuko tayari kukaa Meza moja na lowassa.utakuwa ni unafiki sana
Vyovyote itakavyokuwa, sitakuwa sehemu ya kumchafua Dkt Slaa . Huyu ni Baba Wa demokrasia hapa nchini. Dkt Slaa kwa sasa umeshikilia roho zetu wapenda mabadiliko. Uamuzi wowote utakaochukua usisahahau jambo hili. Tunakupenda, tunakukubali, na tunakuthamini.
Yericko,
Siasa ya unafiki sipendi. Nimenyamaza lakini naona mnazidi kunichokoza. Ni afadhali mngelikaa kimya kama nilivyonyamaza mimi. Uwongo wowote na upotoshwaji wowote sitauvumilia. Nitaukanusha hapo hapo. Hata kama una lengo lako ambalo silifahamu naomba sana usitumie jina langu. Nimefundishwa uwongo ni dhambi siko tayari kushiriki dhambi hiyo.
sina kikao chochote cha Secretariat sina mpango wowote ninaopanga kuwasilisha popote. Naomba watanzania wapuuze propaganda zote zinazofanyika kwa jina langu.
Ningehitaji kutuma taarifa yoyote kwa umma ningeliita Press Conference Mwenyewe au ningelitumia utaratibu wowote uliouliozoeleka.
Naomba kutoa onyo kwa mtu yeyote awaye, matumizi ya jina la Dr Slaa yakome.
Nenda kwenye profile yake, hiyo ndio account anayoitumia toka 2008
leo mnamwona DR SLAA sio chochote chadema?kumbuka anaulemavu wa mkono kapata kwasababu ya cdm wewe unaemtusi huna hata kovu dogo la cdm ktk mwili wako
Mzee Slaa anchana naye huyo!Yericko,
Siasa ya unafiki sipendi. Nimenyamaza lakini naona mnazidi kunichokoza. Ni afadhali mngelikaa kimya kama nilivyonyamaza mimi. Uwongo wowote na upotoshwaji wowote sitauvumilia. Nitaukanusha hapo hapo. Hata kama una lengo lako ambalo silifahamu naomba sana usitumie jina langu. Nimefundishwa uwongo ni dhambi siko tayari kushiriki dhambi hiyo.
sina kikao chochote cha Secretariat sina mpango wowote ninaopanga kuwasilisha popote. Naomba watanzania wapuuze propaganda zote zinazofanyika kwa jina langu.
Ningehitaji kutuma taarifa yoyote kwa umma ningeliita Press Conference Mwenyewe au ningelitumia utaratibu wowote uliouliozoeleka.
Naomba kutoa onyo kwa mtu yeyote awaye, matumizi ya jina la Dr Slaa yakome.
Tunamtaka Dr. Slaa atulie. Tunachotaka ni kuitoa CCM kushika Dola. Vyeo ni vingi baada ya hapo. Wewe utachagua cheo unachokipenda.
Dr. Slaa aliwahi kuweka wazi siku ya nyuma kuwa account hata mke wake huwa anaitumia kwa kuwa siyo account rasmi ya Chama bali ni yake Binafsi hivyo mke wake ana haki ya kuitumia pia na kwa muda mke amekuwata akiitumia hapa jf.
By the way, binafsi ninaheshimu sana mchango wa Dr. Slaa, sina namna ya kumuelezeakwa mazuri yake hata niweze kumtendea haki. Ila kitu ambacho sitathubu kukifanya ni kuelezea mapungufu yake, maana nitamkosea heshima moja kwa moja ingawa nitakua nimeuawasilisha ukweli katika sura yake halisi.
Nimeshangazwa sana kuona anasema hana mpango wowote na yeyote wakati jamii inatambua fika kuwa yeye bado ni katibu mkuu wa chama na mipango mingi inamuangalia yeye kipindi hiki kama ilivyokuwa katika kipindi kilichopita, lakini tumemsoma akikana kuwa hana mpango wowote wakati huo huo hatakai kutoa tamko rasmi kwamba anajiweka pembeni. Naomba binafsi niishie hapa kumjadili Dr. Slaa kwa lengo la kuenzi mazuri yake na nsije nikamkosea heshima, hata akiamua yeye kwenda CCM au kuungana na zito nitaendelea kumheshimu maana kila alichokifanya alikifanya kwa dhati ya moyo wake.
Nakutakia kila lenye kheri Dr. Slaa katika tafakuri yako.
Dk,Hahusiki na kilichoandikwa hapo.Niliposikia tetesi za Dr.W.Slaa kususa nilidhani niuzushi tu, la kwa uzi huu nashawishika kuamini Dk.Slaa ameamua kujitenda na chama rasmi.. Ni jambo gumu na la kuumiza sana kuona haya yanatokea wakati huu, hama kweli siasa ni zaidi ya tunavyoielewa wengi wetu.
Wote mlioungana na SLAA katika kipindi hiki kigumu kwenye mada hii na mmechangia ukurusa wa kwanza NIMEWAPA LIKE kwa niaba na weingine. ASANTENI WOTE, ASANTE DR. SLAA, LEO UMEMMALIZA YERIKO NYERERE NA WANAFIKI WOTE WA CHADEMA.Yericko,
Siasa ya unafiki sipendi. Nimenyamaza lakini naona mnazidi kunichokoza. Ni afadhali mngelikaa kimya kama nilivyonyamaza mimi. Uwongo wowote na upotoshwaji wowote sitauvumilia. Nitaukanusha hapo hapo. Hata kama una lengo lako ambalo silifahamu naomba sana usitumie jina langu. Nimefundishwa uwongo ni dhambi siko tayari kushiriki dhambi hiyo.
sina kikao chochote cha Secretariat sina mpango wowote ninaopanga kuwasilisha popote. Naomba watanzania wapuuze propaganda zote zinazofanyika kwa jina langu.
Ningehitaji kutuma taarifa yoyote kwa umma ningeliita Press Conference Mwenyewe au ningelitumia utaratibu wowote uliouliozoeleka.
Naomba kutoa onyo kwa mtu yeyote awaye, matumizi ya jina la Dr Slaa yakome.
mkuu unacheza na hawa watu hawa ni madon king ati anaingia na bondia huyu akishindwa anatoka na alieshinda wanabadili gia hewani balaa.Leo hii Slaa si kamanda tena.. Kisa ujio wa Lowasa.