Dkt. Siko tayari kuhongwa nikae kimya ili nisipokonywe hiyo title, mapambano ya Bandari yako palepale

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,482
8,336
Muda mfupi baada ya kuvuliwa hadhi ya Ubalozi, Mwanasiasa Mkongwe, Dkt. Willbroad Slaa amesema "Niliwakilisha nchi yangu kimataifa, wanaojua ubora wa ubalozi wangu ni nchi ambazo nilizihudumia. Ubalozi ni historical, hautafutika.

Nilishawapa ruhusa niko tayari wachukue ubalozi kwa sababu siko tayari kuhongwa ili nisiseme nikakaa kimya ili nisipokonywe hiyo title. Kwa sababu mimi ndio muathirika naomba kusema mapambano ya bandari yako palepale, sisemi kwamba yataongezeka ama kupungua kwa sababu tayari nilikuwa kwenye gia ya tano"

Kauli ya Dkt. Slaa baada ya kuvuliwa hadhi ya Ubalozi na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan
 
Back
Top Bottom