Burkinabe
JF-Expert Member
- Feb 12, 2023
- 1,926
- 3,237
Habari wanajamvi.
Moja kwa moja kwenye mada.
Hivi karibuni kumezuka taharuki ambayo haikuwa na sababu ya msingi, juu ya wapi alipo Makamu wa Rais wa Tanzania, Dkt. Philip Isdory Mpango. Makamu huyu alikuwa hajaonekana hadharani kwa takribani mwezi mzima kwa mujibu ya vyanzo vya habari ikiwamo mitandao ya kijamii.
Hali hii ilipelekea Watanzania waulize ni wapi alipo kiongozi wao huyo kwa muda upatao wiki 2 au zaidi. Kumekuwa na uvumi na habari mbalimbali za kukanganya Umma, huku wengine wakidai yuko nje ya nchi kwa kazi "maalum", wengine anaumwa na anafanyiwa upasuaji wa koo huko Korea Kusini, wengine wakienda mbali zaidi na kusema ameshafariki!
Serikali iliamua kukaa kimya, ukitoa tamko la waziri Mkuu ambalo pia lilikuwa linaacha maswali mengi kwa raia.
Sasa shida imekuja baada ya Makamu wa Rais kuibukia kanisani na baadaye Ikulu na kuanza kuwashutumu Watanzania waliokuwa wanataka kujua yuko wapi na anafanya nini!
Dkt. Mpango, sisi kama Watanzania tulikuwa tunakuulizia kwa sababu ya nafasi yako unayoishikilia kwa sasa na wala siyo vinginevyo.
Ndiyo maana hatujawaulizia Waziri Mkuu Mstaafu Mh. Edward N. Lowasa, Rais Mstaafu wa awamu ya pili Alhaji Mzee Ali Hassan Mwinyi n.k. Hatuwezi kuwaulizia hao siyo kwa sababu hawana umuhimu kwetu, bali kwa sababu hawako kwenye ofisi zetu za Umma na kwa hiyo hawana msaada kwetu wa moja kwa moja kama ulivyo wewe pamoja na viongozi wengine mlioko madarakani kwa sasa.
Nimalizie kwa kukumbushia tu kile ambacho Wakili Mwabukusi aliwahi kusema, kwamba, "kama kuna kiongozi wa Umma ambaye hataki kufuatiliwa na Umma au hataki mambo yake yajulikane kwa Umma, basi ajiudhuru aone kama tutataka kujua chochote kumuhusu yeye au familia yake."