MamaSamia2025
JF-Expert Member
- Mar 29, 2012
- 12,231
- 27,662
Leo ninaandika nikiwa na hasira zilizochanganyikana na huzuni kwa upotoshaji mkubwa unaofanywa na huyu daktari pamoja na madaktari wengine uchwara wanaolazimisha ionekane kuwa nchi ipo kwenye tatizo kubwa la unene uliopitiliza wakati ni kinyume chake.
Tumekuwa tukiwasikia msile wanga mara usikun kuleni tu matunda na maji mengi wakati wananchi wengi wanakula tu ili kuzuia msiba na sio kuzingatia mlo kamili kwasababu ya umaskini.
Hizo nguvu mnazotumia kwa ajili ya kikundi cha watu wachache mngetumia kuonyesha ukubwa wa tatizo la lishe kwa wananchi mngepata thawabu. Dr Janabi huna tofauti na mke wa mfalme wa Ufaransa aliyesema watu kama hawana mikate wale keki.
Kwa mujibu wa mtandao wa STATISTA hadi kufikia November 2021 kulikuwa na 31.8% ya watoto wa chini ya miaka miatno wenye utapiamlo uliokithiri (Chronic Malnutrition). Ni 4% tu ya watoto huzaliwa wakiwa overweight.
Kimsingi hivyo vyakula anavyosema Janabi watu wasile ni ndoto za watanzania wengi kuvipata angalau mara moja kwa siku. Mikoa mingi ya Tanzania inakabiliwa na tatizo la lishe. Ninachoona ni ndugu Janabi kudhani maisha anayoishi yeye ndo wanayoishi watanzania wote. ASIJISAHAU
Ninatoa wito kwa serikali za mitaa kupambana ili mashuleni watoto wawe wanapata chakula. Wale wazazi/ walezi wapumbavu wanaokataa kuchangia vyakula kwa kisingizio cha ELIMU BURE wakamatwe watupwe tu ndani maana wanaturudisha nyuma. Haihitaji utafiti kujua kama kuna tatizo kubwa la lishe karibu maeneo yote nchini.