Déjà vu: Umewahi kuwa sehemu, au kufanya kitu ukahisi ulichofanya au mazingira ya hapo kwa muda huo yamejirudia kabisa?

NadeOj

Member
Mar 25, 2024
13
34
Hiyo hali inaitwa déjà vu,

Wanasayansi wameielezea kwa theories tofauti wakielezea inasababishwa na nini. Ila bado hamna jibu rasmi linalokubaliwa na wanasayansi:

Theory mojawapo inaeleza kwamba,

Namna ambayo ubongo huhifadhi kumbukumbu, mfano kuna jina unalijua limehifadhiwa kwenye ubongo, utakapolisikia, kuna sehemu ya ubongo ambapo kumbukumbu hiyo ilitunzwa inaamshwa kwaiyo unalikumbuka na linakua sio jina geni.

Sasa wanasayi wanasema inapotokea umefanya kitu cha kufanana sana kwenye mazingira yaleyale, huenda ikapekekea kumbukumbu ya kile kitu kwenye ubongo kuamshwa, kwahiyo unaona kama vile hicho kitu sio kigeni na kimejirudia exactly hiyo hali inaitwa déjà vu.

Hayo ni moja ya maelezo ya wanasayansi kuna theory nyingi zinazo jaribu kuelezea hiyo hali inasababishwa na nini, nyingine pia zinasema ni mojawapo ya tatizo la kiakili katika kuweka kumbukumbu.

Haya watu wa asili mtuambie hali hii inasababishwa na nini
 
Kwa kutumia hili bichwa langu hebu onesha hiyo sehemu ya ubongo inayostuliwa na kurejesha kumbukumbu.
 
Baada ya mwezi nakuja na majibu kupitia kitabu cha Riwaya.

Majibu kwa ufupi kila jambo limewekwa kwenye vina saba. Wewe wa leo ulikuwepo kipindi cha babu yako. Hivyo babu yako ni wewe wa leo. Umezaliwa tena na utajizaa tena kizazi kijacho kumbukumbu zako utasafiri nazo ama zitakufa kulingana na uwezo wako wa Tenkai.
 
Baada ya mwezi nakuja na majibu kupitia kitabu cha Riwaya....
ila vinasaba kwa nilivokua najua, vinabeba kumbukumbu kama, appearance yako kwa ujumla, uongeaji, upole, rangi, kimo na vitu kama hivo.

hata wana biology wanaweza kufanya cloning wakatumia seli kuzalisha kiumbe kinachofanana.

mfano kuna kiumbe alikua na sifa Fulani. wanataka ku duplicate wanafanya cloning
kiumbe kitakachozalishwa kitakua na sifa hizo ila si lazima arudie matukio yaliyofanywa na pia hawezi kuwa na kumbukumbu ya vitu vya kabla hajazaliwa.
 
Mimi huwa kuna sehemu huwa naziota nikiwa katika maeneo hayo sehemu ambazo sijawahi kufika hata siku moja kiuhalisia lkn kwenye ndoto huwa najikuta baada ya mda fulani (wakati mwingine kwa kipindi kirefu) ndoto inajirudia na inakuwa kama mwendelezo wake.
 
Baada ya mwezi nakuja na majibu kupitia kitabu cha Riwaya.

Majibu kwa ufupi kila jambo limewekwa kwenye vina saba. Wewe wa leo ulikuwepo kipindi cha babu yako. Hivyo babu yako ni wewe wa leo. Umezaliwa tena na utajizaa tena kizazi kijacho kumbukumbu zako utasafiri nazo ama zitakufa kulingana na uwezo wako wa Tenkai.
Hili ndio jibu sahihi!!

Asante.sana!!
 
Mimi huwa kuna sehemu huwa naziota nikiwa katika maeneo hayo sehemu ambazo sijawahi kufika hata siku moja kiuhalisia lkn kwenye ndoto huwa najikuta baada ya mda fulani (wakati mwingine kwa kipindi kirefu) ndoto inajirudia na inakuwa kama mwendelezo wake.
Hilo ni kweli!Kuna mwendelezo wa kesi Fulani Huwa naota unajirudia!nimeamua kuikataa Ile ndoto ni mbaya sana!!
 
Kamwe huwezi kujikimbia milele
Ni kama nilimuajiri.dogo mmoja Kwa KAZI na mwenzake sijui aliiba nini alizingua Nini,no kama nilimpiga akaondoka akaenda kwao baada ya siku kadhaa ni kama alikufa,Sasa Ni kama police wanafuatilia hiyoishu,labda ni ndugu walishtaki sijui,Sasa majuzi nikaota ni kama police wanakuja eneo la tukio kutaka details!

Naonekana kwenye ndoto kama naiogopa hiyo ishu kinoma noma aiseh!!

Hadi ilibidi nimuombe Mungu hii ndoto ipotee,naichukia sana aiseh!!
 
Back
Top Bottom