DC Muro aongoza timu kumaliza mgogoro wa ardhi wa miaka 18 Ikungi

BWANKU M BWANKU

JF-Expert Member
Jan 12, 2019
335
420
DC Muro aongoza timu kumaliza mgogoro wa ardhi wa miaka 18 Ikungi.

Mkuu wa wilaya ya Ikungi Mhe. Jerry C. Muro pamoja na viongozi wa kata ya Irisya wakiongozwa na mwenyekiti wa halmashauri ya ikungi Mhe. Ali juma mwanga ambae ni diwani wa irisya wamefanikiwa kuumaliza mgogoro wa ardhi baina ya Mama Hadija Mohamed na Ndugu Masoud Jumanne Tipa wa kitongoji cha mghondwe kijiji cha munyu kata ya irisya

Mgogoro huo uliodumu kwa miaka 18 mara baada ya kumalizika kwenye baraza la ardhi kata na wilaya lakini bado wananchi hao waliendelea kuvutana hatua iliyosababisha eneo kutolimwa katika msimu huu wa kilimo hatua ambayo Mkuu wa wilaya Mhe. Muro amesema haipaswi kuendelea kuachwa mana lazima ardhi ilimwe wananchi waondokane na umasikini

Akizungumza mara baada ya kutembelea shamba hilo na kukagua nyaraka za umiliki na kufuatilia mwenendo wa shauri hilo katika mabaraza ya ardhi Mhe. Muro amebaini Mama Hadija Mohamed ambae ni mjane ana nyaraka zote muhimu za umiliki ikiwemo hati ya makazi ya kimila na nyaraka alizonunua shamba hilo kutoka kwa Marehemu Robert mikindo ambae alipewa shamba hilo na baba mzazi wa Masoud Jumanne mtipa ambae yeye ameendelea kulalamikan kuwa eneo hilo ni la urithi wakati baba yao alishalitoa kwa marehemu Robert mikindo ambae alimuuzia mama Hadija mohamed ambae amekuwa akilitumia shamba hilo kwa miaka zaidi ya 15

Awali mwenyekiti wa halmashauri ya ikungi ambae ni diwani wa kata ya irisya amesema kumalizika kwa mgogoro huo kutatoa nafasi ya kuendelea kwa shughuli za kilimo katika msimu huu wa kilimo hatua itakayomsaidia mama mjane kujikimu kimaisha na familia yake

Tazama picha za tukio 👇🏾👇🏾

Imetolewa na ofisi ya mkuu wa wilaya Ikungi
13/01/2023

IMG-20230113-WA0023.jpg

IMG-20230113-WA0024.jpg

IMG-20230113-WA0025.jpg

IMG-20230113-WA0026.jpg

IMG-20230113-WA0026.jpg

IMG-20230113-WA0027.jpg

IMG-20230113-WA0027.jpg
 

Attachments

  • IMG-20230113-WA0022.jpg
    IMG-20230113-WA0022.jpg
    80.3 KB · Views: 2
Mwambie yule jamaa aliyemsingizia unyang'anyi wa uongo na kumfunga miaka 30 katoka jela
 
Back
Top Bottom