#COVID19 Covid19 na wimbi la conspiracy theories zake

Yoda

JF-Expert Member
Jul 22, 2018
38,029
46,855
Ugonjwa uliolipuka mwishoni mwa mwaka 2019 ambao kwa sasa unaelekea umedhibitwa kikamilifu baada ya miaka mitatu bado haujajulikana chanzo chake. Hizi hapa ni baadhi ya nadharia za chanzo chake,

1.Kampuni kubwa za dawa za magharibi zilitengeneza janga ili kufanya biashara ya kuuza chanzo. Support ya hili ni jinsi chanzo zilivyolazimishwa.

2.Virusi vilitengenezwa na Wamarekani kuwamaliza Wachina ika backfire hadi kwao wenyewe

3.Virusi vilitengenezwa maabara na wazungu kuwamaliza races nyingine duniani ika backfire hadi kwao wenyewe

4.Virusi vilitengenezwa maabara na Wachina kuwamaliza Wamarekani vika backfire kwao wenyewe.

5.Virusi vilivuja bahati mbaya katika majaribio ya kimaabara huko Wuhan China.

6. Teknolojia ya mawimbi ya mtando ya G5 iliviibua virusi.

7.New World Order(NWO) walitengeneza virusi kwa ajili ya ajenda zao za depopulation.

8.Virusi vilitoka kwa wanyamapori vikarukia kwa binadamu katika (wet markets) masoko ya wanyamapori huko China. Hii ndio theory ambayo wanasayansi wengi mainstream wanaikubali.
 
Hilo lilishapita kama MWAMBA alivyosema, ni vimafua tu!

Tujengewe uwezo kama nchi kuweza kutambua CHANJO zinazoletwa zina nini hasa ndani na kwaajili ya nini, effects zake ni nini!

Ndo tumeshadungwa MICHANJO, shukrani kwa awamu ya 6, kama ndio muendeleo wa DEPOPULATION ya NWO au LGBTQ agenda, basi tumshukuru mama kwa juhudi zake hizo.

Chanjo tulizopigwa, nini matokeo yake siku za usoni?

NJE ya masa; nilisikia Cancer haina chanjo wala kinga kwa sasa!
- Hizo wanazowapa watoto wa kike chini ya miaka 14 huko mashuleni wakisema ni kwaajili ya kuzuia cancer ya mlango wa kizazi, inatumika duniani kote? Ulaya na Amerika wanafanya hivyo?
 
Back
Top Bottom