#COVID19 China imepinga juhudi za Marekani kuchunguza zaidi iwapo Covid 19 ilitoka katika maabara moja ya China

stakehigh

JF-Expert Member
Aug 9, 2019
6,428
3,534
Rais wa Marekani Joe Biden amesema anatarajia matokeo kuhusu ripoti ya upelelezi wa chanzo cha virusi hivyo.

Wizara ya kigeni nchini China iliishutumu Marekani kwa kufanya siasa na kuirushia lawama.

Imepinga uhusiano wowote kati ya Covid 19 na maabara moja ya virusi katika mji wa China wa Wuhan.

Covid-19 kwa mara ya kwanza ilibainika mjini Wuhan mwisho mwisho wa mwaka wa 2019.

Tangu wakati huo, zaidi ya maambukizi milioni 168 yameathibitishwa duniani huku takriban vifo milioni 3.5 vikiripotiwa.

Maafisa wa China walihusisha soko moja la vyakula vya baharini mjini Wuhan na maambukizi ya kwanza ya ugonjwa huo, na kuwafanya wanasayansi kuwa na dhana kwamba virusi hivyo mara ya kwanza viliingia kwa binadamu kutoka kwa Wanyama.

Shirika la Afya duniani WHO limesema kwamba hakuna uwezekano kwamba virusi hivyo vilisambaa kutokana na virusi vilivyovuja katika maabara , kufuatia ziara ya Wuhan mapema mwaka huu ili kuchunguza chanzo cha mlipuko wa virusi hivyo.

------------

Rais wa Marekani Joe Biden amesema anatarajia matokeo kuhusu ripoti ya upelelezi wa chanzo cha virusi hivyo.

Wizara ya kigeni nchini China iliishutumu Marekani kwa kufanya siasa na kuirushia lawama.

Imepinga uhusiano wowote kati ya Covid 19 na maabara moja ya virusi katika mji wa China wa Wuhan.

Kwanini dhana ya kuvuja kwa virusi hivyo inachukuliwa kwa umuhimu mkubwa.

Covid-19 kwa mara ya kwanza ilibainika mjini Wuhan mwisho mwisho wa mwaka wa 2019 .

Tangu wakati huo , zaidi ya maambukizi milioni 168 yameathibitishwa duniani huku takriban vifo milioni 3.5 vikiripotiwa.

Maafisa wa China walihusisha soko moja la vyakula vya baharini mjini Wuhan na maambukizi ya kwanza ya ugonjwa huo, na kuwafanya wanasayansi kuwa na dhana kwamba virusi hivyo mara ya kwanza viliingia kwa binadamu kutoka kwa Wanyama.

Shirika la Afya duniani WHO limesema kwamba hakuna uwezekano kwamba virusi hivyo vilisambaa kutokana na virusi vilivyovuja katika maabara , kufuatia ziara ya Wuhan mapema mwaka huu ili kuchunguza chanzo cha mlipuko wa virusi hivyo.

Mtaalamu wa masuala ya virusi katika WHO Marion Koopmans , ambaye alikuwa miongoni mwa waliokuwa katika ziara hiyo , aliambia BBC kwamba iwapo utawala wa Marekani una habari yoyote ni vyema kuitoa.

Lakini ripoti za vyombo vya habari vya Marekani za hivi karibuni zinasema kwamba kuna ushahidi wa kutosha kwamba virusi hivyo huenda vilivuja kutoka kwa maabara ya China , pengine kwa bahati mbaya.

Kwanini mzozo huu unajitokeza sasa?

Katika taarifa siku ya Jumatano, Rais Biden alisema kwamba aliomba ripoti kuhusu chanzo cha virusi hivyo baada ya kuchukua madaraka, ikiwemo iwapo vilitoka kwa mnyama au kutoka kwa maabara ". Alipoipokea mwezi huu aliagiza ''ifuatiliwe zaidi''.

Security personnel keep watch outside the Wuhan Institute of Virology during the visit by the World Health Organization (WHO) team tasked with investigating the origins of the coronavirus disease (COVID-19), in Wuhan, Hubei province, China February 3, 2021.

Bwana Biden alisema kwamba idadi kubwa ya majasusi, waliafikiana kuhusu dhana hizo mbili, lakini hawaamini kwamba kuna habari za kutosha kuona iwapo kati ya hizo mbili kuna moja ilio sahihi zaidi ya nyengine ".

Anasema kwamba amevitaka vitengo kadhaa kuimarisha juhudi zao za kukusanya na kutathmini habari ambazo zinaweza kupata chanzo chake''.

Siku ya alhamisi, bwana Biden aliambia maripota kwamba alipanga kutoa ripoti hiyo, ''hadi iwapo kuna kitu sikijui''.

Waziri mkuu wa Canada Justin Trudeau baadaye aliunga mkono juhudi za Marekani na mataifa mengine za kutaka kuelewa zaidi chanzo cha virusi hivyo.

Siku ya Jumatano tangazo hilo liliwakasirisha maafisa wa China.

Msemaji wa wizara ya kigeni nchini China Zhao Lijian alisema kwamba inaonyesha kwamba Marekani haijali kuhusu ukweli na haijali kuhusu tafiti za kisayansi kuhusu chanzo cha virusi hivyo.

''Lengo lao ni kutumia mlipuko huu kutafuta njia za kutenga mataifa mengine, kufanya siasa na kurushiana lawama. Hawaheshimu sayansi na kufikiria kuhusu maisha yaliopotea mbali na juhudi za kukabiliana na maradhi hayo'', alisema

Msemaji huyo alisema kwamba ujasusi wa Marekani una 'historia chafu' ya kusambaza habari.

Taarifa kutoka kwa ubalozi wa China nchini Marekani ambao haikuzungumzia moja kwa moja kuhusu agizo la bwana Biden ilisema kwamba ''kampeni ya kuchafuliana jina na kurushiana lawama inarudi''.

Je, nadharia ya kuvuja kwa virusi hivyo inasema?

Ni tuhuma kwamba huenda virusi vya corona vilivuja kwa bahati mbaya kutokana na kuwepo kwa maabara katika mji wa kati wa China wa Wuhan ambapo maambuzki ya kwanza ya virusi hivyo yaliripotiwa.

Wanaounga nadharia hiyo wanasema kwamba hilo lilitokana na maabara kubwa ya kufanya utafiti mjini humo.

Taasisi hiyo ya virusi mjini Wuhan imekuwa ikifanyia utafiti virusi vya popo kwa zaidi ya muongo mmoja sasa.

Maabara hiyo ipo kilomita chache kutoka kwa soko la Huanan ambapo maambukizi ya kwanza yalitokea.

Wale wanaounga mkono nadharia hiyo wanasema kwamba huenda vilivuja kutoka kituo hicho na kusambaa hadi katika soko.

Wengi wanasema kwamba huenda ni virusi vilivyopatikana kutoka kwa Wanyama pori badala kutengenezwa.

Nadharia hiyo yenye utata ilianza mapema wakati wa mlipuko huo na kukuzwa na aliyekuwa wakati huo rais wa Marekani Donald Trump.

Wengine walipendekeza kwamba huenda virusi hivyo vilitengenezwa kama silaha ya kibaiolojia.

Huku wengi katika vyombo vya habari na siasa wakipinga nadharia hiyo wakati huo, wengine walitaka uchunguzi zaidi kufanywa.

Hatahivyo wazo hilo lilizuka tena wiki hii.

Je, wanasayansi wanafikiria nini?

Uchunguzi wa WHO ulitakiwa kupata ukweli lakini wataalamu wengi wanaamini ulitoa maswali mengi zaidi ya majibu.

Kundi moja la wanasayansi walioteuliwa na WHO lilikwenda Wuhan mapema mwaka huu ili kuchunguza chanzo cha mlipuko huo.

Baada ya kufanya uchunguzi kwa siku 12 , ikiwemo ziara ya kwenda katika maabara hiyo, wanasayansi hao walitamatisha kwamba nadharia hiyo ya kuvuja kwa virusi ilikuwa 'haiwezekani.

Je, China inalichukuliaje swala hilo?

China imepinga madai kwamba virusi hivyo vilivuja kutoka kwa maabara huku ikidai kwamba huenda virusi hivyo viliingia nchini humo kutoka taifa jingine kupitia chakula.

Serikali ya China inadai kwamba utafiti mpya uliochapishwa na mmoja ya wanasayansi wake kutokana na sampuli zilizokusanywa kutoka kwa popo ulibaini aina nane ya corona zilizopatikana katika popo.

Gazeti hilo linasema kwamba virusi vya corona kutoka kwa pangolins ndio tisho kubwa kwa afya ya binadamu zaidi ya vile vingine kwa sasa.

Chanzo: BBC Swahili
 
Pamoja na yote hayo, Marekani kuvielekeza vyombo vyake vya "ujasusi", kufanya uchunguzi zaidi ili kubaini ukweli wa janga hili, hawajakurupuka, tuendelee kuvuta subira ukweli utajulikana.
 
Back
Top Bottom