UZUSHI China kuchukua Uwanja wa Ndege wa Entebbe baada ya Uganda kushindwa kulipa deni

Baada ya tathmini, tumebaini kuwa taarifa hii ni ya uzushi
Source #1
View Source #1
Mwishoni mwa mwaka 2021 kuliibuka taarifa kuwa Serikali ya Uganda imeshindwa kulipa deni kiasi cha dola milioni 207 na kusababisha kutaifishwa uwanja wake wa nddege wa Entebbe. Taarifa hizo zilizochapishwa na vyombo mbalilmbali duniani vilieleza kuwa Uwanja wa Entebe sio mali ya Uganda tena, kwamba Wachina wameutwaa uwanja huo. Taarifa hizo pia zilisambazwa kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii ikiwamo Twitter.

20221028_114334.png
 
Tunachokijua
Serikali ya China ilisemekana kuweza kuchukua Kiwanja kikubwa cha Ndege Entebe baada ya kushindwa kulipa deni ambalo China wanaidai Uganda wameshindwa kulipa kwa wakati na kuenda kinyume na makubaliano walioweka.

Kutokana na uchunguzi wa AidData ya kimarekani wamebaini mkataba kati ya Uganda na chini chini ya benki ya Exim ulikuwa na dosari kubwa Zaidi ya dola milioni 200 kwajili ya kuongeza na kuboresha kiwanja cha ndege cha Entebe ambapo kwa mwaka kina uwezo wa kuingiza dola za kimarekani milioni 68.

Mmoja wa wafanyakazi wa shirika la anga Uganda, AG Kiwanuka alisema katika mkataba wa biashara unavyokopa fedha lazima ulipe kwa wakati uliowekwa la sivyo sheria zingine zitachukuliwa na China haiwezi kuchukua kiwanja cha ndege.

Kutokana na makubaliano ya mkataba kama Uganda ikishindwa kulipa deni, Benki ya Exim ya China itachukua sheria nyingine ikiwemo kuifikisha Uganda mahakamani mwishoni mwa mwezi wa 12 Rais wa Uganda Yoweri Museveni Uganda inayo uwezo wa kulipa deni lote.

Taarifa iliyokuwa ikisambaa iliambatanishwa na picha ambayo ilikuwa ikionesha kuwa uwanja wa Entebbe umebadilishwa jina na kuwa CHINA EBB INTERNATIONAL AIRPORT. Hata hivyo, mnamo tarehe 29 Novemba, Mamlaka ya Usafiri wa Anga ya Uganda (UCAA) ilichapisha picha hiyo kwenye akaunti yake ya Twitter iliyothibitishwa, ikiwa na muhuri wa "FAKE".



Pia, Serikali na ubalozi wa China mjini Kampala walikanusha ripoti kwamba Beijing inaweza kuchukua udhibiti wa uwanja huo. Kwa mujibu wa msemaji wa mamlaka ya usafiri wa anga ya Uganda, Vianney Luggya, Serikali haijawahi kukabidhi uwanja wa ndege wa Entebbe kwa China na kwamba Uganda, siku zote imetimiza ahadi zake kuhusu ulipaji wa mkopo uliotolewa na Benki ya China ya Exim Bank.
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom