Madarasa ya Uongozi yaliruka baadhi ya Mada?

Oct 13, 2018
35
259
Na Thadei Ole Mushi

Uganda ipo mbioni kupoteza umiliki wa Uwanja wake wa ndege wa Entebe baada ya wakopeshaji nchini China kukataa ombi lao la kujadili tena mkopo wa Dola za Marekani 200 milioni uliochukuliwa miaka sita iliyopita ili kupanua Uwanja huo wa Entebe. Gazeti la Mwananchi Leo limeripoti habari hii pitia link ifuatayo kuona:-.

Mwaka 218 kwenda 2019 China iliizingua Sana Zambia wakati ilipotaka kushikilia Shirika la uzalishaji Umeme la ZESCO baada ya Zambia kushindwa kuwalipa Deni Leo.

Huko Sri-Lanka nako wachina wameshikilia Bandari ya nchi hiyo kwa Lengo lile lile la kulipa madeni ya China.

Mwaka Huu China wamewakatalia Kenya kuongeza Muda wa Kulipa Deni lake wanalowadai Kenya hivyo wanataka kushikilia Bandari ya Mombasa. Uhuru Kenyata ameenda kuwaangukia IMF kuona kama wanaweza kuwasaidia kuwalipa wachina Hilo Deni kuokoa Bandari yao isichukuliwenna wachina. Fuata Link hii hapa kusoma:-.

Niliwahi kuwasimulia namna Sera ya "conspirancy" inavyofanya kazi Afrika na mataifa mengine na Leo tumepata mfano halisi toka Uganda.

John Perkins kupitia kitabu chake "Confession of an Economic Hit man" anatufunulia jinsi sera ya Conspiracy inavyofanya kazi Duniani.

Perkins anaelezea kazi aliyokuwa akiifanya bila yeye kujua kwenye Kampuni la MAIN (Consulting and engineering Company)

Aliajiriwa kama mfanyakazi kwenye kampuni hiyo ambalo ni Kampuni binafsi ila shughuli zake ziliathiriwa na mkono wa Serikali (Ujasusi) bila yeye kujua.

Kazi yake kubwa ilikuwa ni kushawishi nchi maskini zikope mikopo kwa ajili ya miradi mikubwa katika nchi zao. Miradi kama vile ujenzi wa miundombinu ya Reli,Ujenzi wa Mabwawa ya Umeme, ujenzi wa Bandari, Viwanja vya Ndege nk ambapo utasaidiwa kukopeshwa aidha na World bank, IMF au USAID.

Perkins alikuja kugundua kuwa njia hii ya kukopesha mikopo mikubwa ambayo hailipiki ni njia mojawapo ya Taifa la Marekani kuendelea kupata maeneo ya kunyonya katika nchi maskini.

Perkins anatoa mifano jinsi alivyofanikisha kuingiza Indonesia kwenye Mtego huo na nchi nyingine nyingi.

Kwa Sasa China anatumia Sana "CONSPIRACY POLICY" kiutawala Dunia hasa Afrika Kiuchumi.

Kwa nchi ambazo zinaendelea na zenye rasilimali kama Gesi, Madini na mafuta Marekani na Sasa China huwa hawalali kwenye kuhakikisha inatafuta kuwakopesha.

Wakati tukifuatilia huko Uganda tuendelee kufshamu kuwa Mwaka Jana Serikali ya Awamu ya Tano ilikopa pale Standard Charter Trilion 3.3 za Kujenga SGR Fuata Link kusoma.

Tukiendelea kusoma hayo ya Standard Charter tufahamu pia kuwa pale Exim bank ya China mwaka 2016 tulifanya nao makubaliano ya kupatiwa USD 7.6 Bilioni fuata link tupunguze maneno mengi.

Link ya Mwisho hapo juu isomwe pamoja na hii hapa chini

Kwa Sasa hivi China Pekee imeshakopesha nchi mbalimbali za Africa USD 148 Bilion. Na Inaendelea kukopesha, poleni sana Uganda njia yetu ni Moja waafrica Wote.

Ole Mushi
0712702602

images (36).jpeg
 
Unakopa wakati hujui utalipaje. Kosa kubwa alilofanya Mungu wetu wa mbinguni ni kumuumba mwafrika.

Pigeni madongo, lkn Ni ukweli!
kOSA NI KUWAKO KUTOMJUA MUNGU ANAUKUBW GANI ,HUKU UKIMLINGANISHA NA WANADAMU.
Lakini Baya zaidi ni Kukumba wewe ,kiumbe ambaye shukurani za Akili uliyo nayo ni kumtukana aliyekupa .
Bora ungelikuwa Kichaa unaokota makopo au Pumbaaavu sana wewe Mkosefu wa Shukrani.
 
Hivi unadhani kama Ngombe,Mbuzi,Kuku na Kondoo wangefanywa kuwa wakali kama Simba ,si ungeponea Mboga za majani na Maharage maisha yako yote?
Kama watu wote wengeli kuwa Wasomi na welevu, nani angelimfanyia kazi mwenziwe?
Kama nchi zote zingelikuwa zina kila kitu , kungelikuwa na Misafara ya Biashara Duniani?
Kama Muafrika angelikuwa na Uwezo wa kufikiri kama Mzungu au mchina ,nani angeliupa ulimwengu Utajiri unaohitaji mabumbumbu.
Munguametuumba Hivi tulivyo makusudiili tuweze kuhitajiana na kutegemeana.
Lakini wenye Elimu na Imani ya Mungu wa Kweli hubaki kuwa na Amani ya Kudumu, kwani mali i kupata Mkate wako wa leo, kesho inaMungu.Siyo kulimbiukiza mali kisha kuishimaisha ya Unyama na Uchoyo.
Waafrika hawana Tamaa na si wachoyo kiasili.
 
Tulipigwa (Mkapa), Tukapigwa tena (Kikwete), tukapigwa upya (Magufuli) na tutaendelea kupigwa tena na tena (Samia).
Mkapa alituingiza mkenge (ubinafsishaji na uwekezaji) Kikwete alituingiza mkenge (gesi ya Mtwara, Dowans/Richmond, Madini), Magufuli akatuingiza mkenge (mikopo ya miradi ya umeme, reli) na Samia anatuingiza tena mkenge (mikataba ya bandari ya Bagamoyo, Tanesco).

CCM ni zaidi ya shetani.
CCM ilaaniwe milele.
 
Na Thadei Ole Mushi

Uganda ipo mbioni kupoteza umiliki wa Uwanja wake wa ndege wa Entebe baada ya wakopeshaji nchini China kukataa ombi lao la kujadili tena mkopo wa Dola za Marekani 200 milioni uliochukuliwa miaka sita iliyopita ili kupanua Uwanja huo wa Entebe. Gazeti la Mwananchi Leo limeripoti habari hii pitia link ifuatayo kuona:-.

Mwaka 218 kwenda 2019 China iliizingua Sana Zambia wakati ilipotaka kushikilia Shirika la uzalishaji Umeme la ZESCO baada ya Zambia kushindwa kuwalipa Deni Leo.

Huko Sri-Lanka nako wachina wameshikilia Bandari ya nchi hiyo kwa Lengo lile lile la kulipa madeni ya China.

Mwaka Huu China wamewakatalia Kenya kuongeza Muda wa Kulipa Deni lake wanalowadai Kenya hivyo wanataka kushikilia Bandari ya Mombasa. Uhuru Kenyata ameenda kuwaangukia IMF kuona kama wanaweza kuwasaidia kuwalipa wachina Hilo Deni kuokoa Bandari yao isichukuliwenna wachina. Fuata Link hii hapa kusoma:-.

Niliwahi kuwasimulia namna Sera ya "conspirancy" inavyofanya kazi Afrika na mataifa mengine na Leo tumepata mfano halisi toka Uganda.

John Perkins kupitia kitabu chake "Confession of an Economic Hit man" anatufunulia jinsi sera ya Conspiracy inavyofanya kazi Duniani.

Perkins anaelezea kazi aliyokuwa akiifanya bila yeye kujua kwenye Kampuni la MAIN (Consulting and engineering Company)

Aliajiriwa kama mfanyakazi kwenye kampuni hiyo ambalo ni Kampuni binafsi ila shughuli zake ziliathiriwa na mkono wa Serikali (Ujasusi) bila yeye kujua.

Kazi yake kubwa ilikuwa ni kushawishi nchi maskini zikope mikopo kwa ajili ya miradi mikubwa katika nchi zao. Miradi kama vile ujenzi wa miundombinu ya Reli,Ujenzi wa Mabwawa ya Umeme, ujenzi wa Bandari, Viwanja vya Ndege nk ambapo utasaidiwa kukopeshwa aidha na World bank, IMF au USAID.

Perkins alikuja kugundua kuwa njia hii ya kukopesha mikopo mikubwa ambayo hailipiki ni njia mojawapo ya Taifa la Marekani kuendelea kupata maeneo ya kunyonya katika nchi maskini.

Perkins anatoa mifano jinsi alivyofanikisha kuingiza Indonesia kwenye Mtego huo na nchi nyingine nyingi.

Kwa Sasa China anatumia Sana "CONSPIRACY POLICY" kiutawala Dunia hasa Afrika Kiuchumi.

Kwa nchi ambazo zinaendelea na zenye rasilimali kama Gesi, Madini na mafuta Marekani na Sasa China huwa hawalali kwenye kuhakikisha inatafuta kuwakopesha.

Wakati tukifuatilia huko Uganda tuendelee kufshamu kuwa Mwaka Jana Serikali ya Awamu ya Tano ilikopa pale Standard Charter Trilion 3.3 za Kujenga SGR Fuata Link kusoma.

Tukiendelea kusoma hayo ya Standard Charter tufahamu pia kuwa pale Exim bank ya China mwaka 2016 tulifanya nao makubaliano ya kupatiwa USD 7.6 Bilioni fuata link tupunguze maneno mengi.

Link ya Mwisho hapo juu isomwe pamoja na hii hapa chini

Kwa Sasa hivi China Pekee imeshakopesha nchi mbalimbali za Africa USD 148 Bilion. Na Inaendelea kukopesha, poleni sana Uganda njia yetu ni Moja waafrica Wote.

Ole Mushi
0712702602

View attachment 2027052
Credit to The East Africa NewsPaper.
Hongera mwandishi kachambua vema

Sent from my SM-G9350 using JamiiForums mobile app
 
, sio hao wanaokubali masharti ya kipuuzi?Kwa Sasa hivi China Pekee imeshakopesha nchi mbalimbali za Africa USD 148 Bilion. Na Inaendelea kukopesha, poleni sana Uganda njia yetu ni Moja waafrica Wo
Haya matakataka mengine muwe mnajiongeza kidogo kabla ya kuyaleta hapa. Hivi mtu unapokwenda shule halafu usipate kilichokupeleka shule, hapo na wewe utajitambulisha kwamba una elimu?

Kama huwezi kuchambua upuuzi na mambo ya msingi, kwa nini utafute kupotosha na wajinga wengine?

Hata hivyo ngoja nikwambie kitu, pamoja na kwamba sikusoma takataka hizo: Hata ingekuwa ni kweli hayo yote mnayolishwa na mahasimu wa wachina (na siwatetei hao wachina hapa); wa kulaumiwa ni nani hasa, sio hao wanaokubali kuchukua mikopo yenye masharti yasiyofaa kwa nchi zao?

Angalia tu kwa mfano huo wa kwanza wa Uganda: Dola 200 milioni ndio ishindikane hadi Uganda wakubali kupoteza kiwanja?

Clearly you can do better than this.
 
Ivi hao wazungu waliendeleza mataifa yao kwa kuchukua mkopo wapi
Walikopeshana wenyewe kwa wenyewe kwa masharti nafuu. Mfano Uingereza walikopeshwa na wamarekani kwa masharti nafuu wakati wa vita ya pili ya dunia nk.
 
Haya matakataka mengine muwe mnajiongeza kidogo kabla ya kuyaleta hapa. Hivi mtu unapokwenda shule halafu usipate kilichokupeleka shule, hapo na wewe utajitambulisha kwamba una elimu?

Kama huwezi kuchambua upuuzi na mambo ya msingi, kwa nini utafute kupotosha na wajinga wengine?

Hata hivyo ngoja nikwambie kitu, pamoja na kwamba sikusoma takataka hizo: Hata ingekuwa ni kweli hayo yote mnayolishwa na mahasimu wa wachina (na siwatetei hao wachina hapa); wa kulaumiwa ni nani hasa, sio hao wanaokubali kuchukua mikopo yenye masharti yasiyofaa kwa nchi zao?

Angalia tu kwa mfano huo wa kwanza wa Uganda: Dola 200 milioni ndio ishindikane hadi Uganda wakubali kupoteza kiwanja?

Clearly you can do better than this.
Si umesema hujasoma?
Sasa kama Uganda wanachukuliwa kwa hiyo Dola 200, wewe ni nani mpaka ushangae na kubisha?
 
Back
Top Bottom