Chapulines: Kitoweo cha Panzi kutoka Mexico

Damaso

JF-Expert Member
Jul 18, 2018
1,590
2,089
Chakula ni kipengele muhimu cha maisha ya binadamu, ni bidhaa ambayo wakati mwingi huwa ni matokeo ya jitihada, riziki na starehe. Hata hivyo, linapokuja suala la uchaguzi wa mapishi, mapendekezo yanaweza kutofautiana sana kutoka kwa mtu hadi mtu. Ingawa watu wengine wanaweza kupata sahani fulani ladha na kuvutia, wengine wanaweza kuwa na maoni tofauti na kwa Imani nyingi mapishi huonekana kama ibada, kuaznia maandalizi yake na hata maeneo ambayo huzungumzwa wakati wa upishi. Chapulines, ni chakula cha kitamaduni kutoka Oaxaca, huko Mexico, ni mfano mmoja kama huo wa chakula ambacho kwa asili kinaonekana kubeba utadamuni wao.

Kiungo kikuu katika chakula hiki ni Panzi yaani wanategeneza Panzi safi na kuwaandaa pamoja na viungo vingine kutengeneza chakula, na jambo hili huonekana kama sio sahihi sana ka upande wa wanaharakati wa kupigania mazingira, mpaka kuzua mijadala kuhusu thamani yao ya lishe na umuhimu wa kitamaduni.
Chapulines_comestibles_botana.jpg

Ulaji wa wadudu ulianza maelfu ya miaka, na ushahidi wa jamii ambazo zimewahi kujipatia vitoweo vya wadudu zipo nyingi sana, ila kwa Mexico kuna jamii kama vile Mayans na Aztec ambazo ziliwahi kutumia wadudu kama mboga au chakula kabsa. Huko Oaxaca, Mexico, chapulines kimekuwa chakula cha kitamaduni kwa karne nyingi sana, na watu wamekuwa wakikitumia kila siku pasipo matatizo yoyote. Tabia ya kula panzi imekita mizizi yake haswa katika tamaduni za jamii za Zapotec pamoja na Mixtec, ambapo wadudu huchukuliwa kuwa chanzo muhimu cha protini na virutubisho.

Ulaji wa chakula hiki cha chapulines, takwimu mbalimbali kutoka kwa wapishi ghuli duniani, zimechangia kuongeza uelewa wa kitamaduni na upishi wa chakula hiki ndani ya Amerika ya Kusini na dunia kwa ujumla. Mtu mmoja mashuhuri ni Abigail Mendoza, mpishi mashuhuri na ghuli haswa kwenye mapishi ambaye anatokea Mexico Oaxaca. Mendoza amekuwa na jukumu muhimu katika kukuza vyakula vya kitamaduni vya jamii ya Zapotec, ambavyo vinajumuisha vyakula ambayo vinajumuisha kitoweo cha chapulines. Juhudi zake katika kuhifadhi taratibu za asili ya upishi zimepata usikivu na sifa duniani kote, zikitoa mwanga juu ya umuhimu wa chapulines kama ishara ya kitamaduni na furaha ya upishi.
46666185971_5ea4992c03_b.jpg

Chapulines, kama chakula cha kitamaduni, kimeweka alama yake kwenye ulimwengu wa upishi, katika uchanya na hasi. Kwa upande wa athari chanya, chapulines zinatambuliwa kwa thamani yao ya lishe bora haswa protini na kadhalika. Panzi hawa wanaoweza kuliwa wana protini kwa kiwango kikubwa sambamba na nzige, pia wana viwango vingi vya vitamini, na hivyo kuwafanya kuwa mbadala wa afya kwa jamii za watu wengi. Zaidi ya hayo, shughuli ya uvunaji wa wadudu hawa kwa ajili ya chapulines imepata umakini katika miaka ya hivi karibuni. Watu wanaojali mazingira wanaona wadudu kama suluhisho linaloweza kuleta mbadala katika usalama wa chakula ulimwenguni. Baadhi ya wanaharakati wa mazingira wameona kuwa Chapulines, inaweza kuwa sehemu bora sana ya chakula endelevu, kwani kuna uwezo wa kuchangia vyema katika mapambano dhidi ya njaa duniani.

Kwa upande mwingine, walaji na watumiaji wa chapulines wamekabiliwa na upinzani, hasa katika tamaduni za Magharibi, ambapo wazo la kula wadudu linaweza kukutana na kuchukiza sana. Unyanyapaa wa kitamaduni unaozunguka chapulines kama "chakula kibaya zaidi" unaweza kuhusishwa na kutofahamika, kwani wadudu hawatumiwi sana katika nchi za Magharibi. Mtazamo huu hasi umezuia kukubalika kwa chapulines kama chaguo bora la upishi.
0_tELspi1Xz_w5Vmza.jpg

Hata hivyo, mitazamo inayopinga matumizi ya chapulini pia ipo. Baadhi ya watu wanasema kuwa chapulines, licha ya manufaa yao ya lishe, ni vigumu kuingiza katika mfumo wa vyakula duniani kutokana na mapendekezo ya ladha na utamaduni wa kila jamii duniani. Wengine wanaelezea wasiwasi wao kuhusu usafi wa wadudu hao pamoja na maandalizi ya chakula hicho.

Kwa hapa nyumbani tunakula Senene, Kumbikumbi na wadudu wengine, je ukipewa sahani ya wali na mboga ya chapulines utakula au ndo utaishia kukemea tu? Ila kwangu ninaona ni kama Senene au Kumbikumbi tu! Ukipita mitaa ya Calle Alcalá, au Andador de Macedonia Alcala.​
 
Back
Top Bottom