Captain Geogre Bantu kurithi usukani kuliongoza jahazi bila Captain Mkuu Gardner G. Habash

Arnold Kalikawe

Senior Member
Sep 28, 2016
147
341
Sisi wengi wakongwe tunakumbuka historia ya Captain Gardner nguli wa vipindi vya redio, alianza kama muuza cassette (Kanda) za audio na video pale jijini mwanza kama mtu wa masoko, ndipo Othman Njaidi baada ya kuuona uwezo wa Gardner wa kushawishi wateja, akamchukua na kumpeleka Clouds FM japo pia Gardener alikuwa kashamwambia Othman Njaidi kuwa anatamani kuwa mtangazaji. Gardner akajiunga clouds kama mtu wa masoko

Baada ya Gardner kuonana na Ruge Mtahaba mara kadhaa, Ruge akasikia hile rafudhi ya Gardener na kusema huyu anapaswa kuwa mtangazaji. Gardner akachukuliwa na kuamishiwa kipindi cha Afrika Bambataa ambacho muongozaji wake alikuwa Amina Chifupa. Amina Chifupa alimnoa Gardner kwenye utangazaji. Kuanzia ikawa historia. Hata hivyo mwaka 2005 Amina Chifupa aliacha utangazaji na kuwa Mbunge wa kuteuliwa, na miaka miwili baadaye alifariki kwa Sonona (Depression) akiwa na miaka 26. Amina Chifupa atakumbukwa kwa kupigana vita vikali vya madawa ya kulevya na kutishia kutoa orodha ya vigogo wanaouza madawa ya kulevya.

Baadae Gadner alikuja na kipindi cha JAHAZI ambacho ndicho kilichompa umaarufu mkubwa na jina la CAPTAAAAIIIIIIN. Yani nahodha. Akishirikiana na watangazaji wengine kama Ephraem Kibonde ambao walikipa Umaarufu mkubwa kipindi hicho na kukifanya kuwa maarufu zaidi. Ephraim Kibonde akaaga mashindano ya kuishi duniani mwaka 2019 baada ya kwenda kumzuka mwanzilishi wa Clouds FM bwana Ruge Mtahaba ambako baada ya mazishi alipata shida ya kiafya ambayo walilazimika kumsafirisha hadi mwanza ambako ndiko umauti ulimfika, na inasemekana alikuwa na uvimbe tumboni.

Maisha ndani ya kipindi cha JAHAZI la Clouds FM yakaendelea huku Captain Gardner akiendelea kushikilia usukani wa kipindi icho bara bara. Huku wakipitia msuko suko wa mawimbi ya TCRA, na kubidi kubadilisha jina la kipindi na kuwa The Traffic Jam, ambapo mtangazaji George Bantu kutoka East Africa Radio alikuwa kashajiunga na nahodha huyo Captain Gardner kuendeshea mitambo ya Kipindi hicho. George Bantu akiwa kama Captain Msaidizi alilishikiria Usukani vyema na baadae Mawimbi makali ya TCRA yalipoa na Captain Gardner na Captain Msaidizi George Bantu wakafanikiwa kurudisha kipindi cha Jahazi Hewani kutoka kuitwa The Traffic Jam. Jahazi likaendelea kukata mawimbi. Baadae Afya ya Gardner ilianza kuonekana kudhorota na watu na mashabiki wengi wakaanza kupata wasiwasi juu ya afya ya nguli huyo, huku yeye akiendelea kuweka mambo sawa na kuficha uvumi huo. Hata hivyo urafiki wa Captain Gardner na Captain Msaidizi George Bantu ulionekana kumea sana na wakawa wana promote sana matangazo ya pombe na kuonekana wakifurahia maisha kwa pamoja kila wakati pamoja na kunywa mivinyo. Ki ukweli urafiki wao ulifahana sana. Watu wakaanza kuishi pombe ndizo zinamfanya aonekane dhoofu. Hivi juzi kati Captain hakuonekana na kusikika kwenye kipindi kwa siku kadhaa mashabiki wakapata wasiwasi, lakini baadae Captain Gardner aliojiwa na kusema ni kweli alilazwa kwa shida ya kupanda kwa pressure ya damu na sasa anaendelea vizuri, na baada ya siku kadhaa leo 20, Aprili 2024 tukaona taarifa zake za kifo zikitangazwa na kituo cha matangazo ya Radio cha Clouds. Na nyimbo za maombolezi kufuatia.

Gardner atakumbushwa kwa namna alivyoitendea vyema tasnia ya utangazaji na kuibua vipaji mbalimbali vya mziki na vya burudani kwa ujumla. Hasa hasa Sauti yake na jingle zake mashuhuri hususani ile ya CAPTAAAAIIIIIIN tutazikumbuka sana.

George Bantu rasmi atasimikwa kuwa Captain Mkuu wa kipindi cha Jahazi, naye atakuwa na Kibarua cha kuliendesha Jahazi bila ya Captain Gardner.

Mungu aipumzishe mahali pema peponi roho ya marehemu Gardner G. Habashi. Tangulia na sisi tutafuata.

Pia soma TANZIA - Gardner G Habash mtangazaji wa Clouds Media afariki dunia
 
Hiki kipindi cha jahazi nakikumbuka sana. Nilikuwaga bado kijana mdogo on my teens miaka ya 2000. Nakumbuka ilibamba sana wakati hule Roman Abramovich alipotembelea bongo utalii nakupanda mlima kilimanjaro. Yani siku iyo nilikuwa kwenye daladala Ephraim na Gardner waliwaponda sana matajiri uchwara wa kibongo enzi hizo kina papa msofe dhidi ya Mmiliki wa Chelsea Abramovich. Yani ulikuwa mjadala mkali kwenye jahazi. Watu kwenye daladala tulicheka sana. Yani nakumbuka kabisa.

Apumzike salama Ruge, Ephraim, Gardner and other silent masses.
 
Watanzania acheni pombe, pombe itaendelea kuwatandika vibaya na kufupisha maisha yenu.
Baada ya Kibonde, Gardner na George Bantu kujigundua wao ni walaibu wakubwa wa pombe, wakaamua kuisifia pombe, kuipa promo na kuvuna matangazo ya pombe.

Sijui ni nini kimehusika kukatisha maisha ya Gardiner, lakini kwa ule ulaibu wa pombe, ni wazi kama asingeua ini, basi angeishia kuua figo au moyo siku moja.

Sad to hear that a talented man like Gardner passed easy and early.
 
Early miaka 50, ulitaka aishi miaka mingapi??
Pombe mnaipondea bure tu, mnaionea pombe aisee.
 
COMBO YAKE NA GEORGE BANTU ITABAKI KUA DUO BORA ZAID BAADA YA ILE YA GH NA EK jahazini
Ni Kibonde pekee aliliweza sana jahazi. Baada ya Kibonde kipindi hicho kiliondolewa kwenye peak time (kutoka saa kumi jioni mpaka saa moja usiku) Milard Ayo akarudishwa saa 10.
 
Captain na Kibonde ndio ilikuwa combo nzuri. Hawakuchosha kuwasikiliza hata wakizungumzia jambo la kawaida sauti zao na mpangilio wao wa maneno maneno ya kuchomekea
 
Hiki kipindi cha jahazi nakikumbuka sana. Nilikuwaga bado kijana mdogo on my teens miaka ya 2000. Nakumbuka ilibamba sana wakati hule Roman Abramovich alipotembelea bongo utalii nakupanda mlima kilimanjaro. Yani siku iyo nilikuwa kwenye daladala Ephraim na Gardner waliwaponda sana matajiri uchwara wa kibongo enzi hizo kina papa msofe dhidi ya Mmiliki wa Chelsea Abramovich. Yani ulikuwa mjadala mkali kwenye jahazi. Watu kwenye daladala tulicheka sana. Yani nakumbuka kabisa.

Apumzike salama Ruge, Ephraim, Gardner and other silent masses.
Dah! Nilikuwa nakifuatilia online ughaibuni! Kipindi kilinifanya nijisikie nyumbani saana!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom