Naunga mkono hoja hiiWakuu,
Wewe mbunge unajua upo hapo kuwakilisha wananchi, au unawakilisha kundi fulani kama watu wenye ulemavu nk, lakini mwanzo mwisho mama ametenda hiki, mama ametenda kile, hakuna kama yeye, dunia haijawahi kuona kama huyu!
Hivi hamuoni aibu? Hamsikii haya kwa huu ujinga mnaofanya? Yaani bunge limekuwa kama takataka sasa hivi kuangalia sifa zenyu za kipuuzi. Si wanaume wala wanawake wote mnatia kinyaa!
Inabidi tuwakumbushe nini kimewapeleka hapo? Maana inaonekana hamuelewi kabisa kilichowapeleka hapo. Wananchi wenu wana matatizo kibao lakini mmekalia mama anafanya hivi, mama anafanya vile, bure kabisa.
Na sisi wapiga kura embu tuwe serious basi, unaona mbunge wako mweupe na mjinga kama hivi piga chini. Mwisho wa siku wewe ndio unaathirika wao wakigeuka chawa, koi zetu zinaishia mifukoni mwao, huduma zinazidi kuwa mbovu huku wewe unazidi kuwa masiki.
Amka, hakuna chama chochote kimezaliwa na wewe, PIGA CHINI!
View attachment 2967161
Nini sasa hiki?
View attachment 2967168
Kingwangalla ni ujinga gani huu unaongea? Comfortable kabisa kwamba umeenda kuwawakilisha wananchi? Shame on you.