Bunge kusitisha kurusha 'LIVE' vikao vyake!

Tumsifu Samwel

JF-Expert Member
Jul 30, 2007
1,407
159
BUNGE linatarajia kufuta utaratibu wa kurusha matangazo ya moja kwamoja kupitia televisheni kwa madai ya kukomesha vitendo vya baadhi ya wabunge kukiuka kanuni za bunge na kuleta vurugu kwa kutafuta umaarufu bila kujua kwamba tabia hiyo inaleta picha mbaya katika jamii.

Hayo yamesemwa na Katibu wa Bunge Dk.Thomas Kashilila jijini Dar es salaam wakati akitoa taarifa ya mapendekezo ya kuanzisha kamati ya bajeti na kuvunjwa kwa baadhi ya kamati za bunge.

Amesema kuwa ili kuleta maadili kwa baadhi ya wabunge ambao wamekuwa wanashindwa kufuata kanuni za bunge na kutumia nafasi hiyo kwa kutafuta umaarufu kwa sasa wameomba kufutwa utaratibu wa kurusha matangazo ya bunge ya moja kwa moja badala yake watarekodi ili kuondoa hoja zisizokuwa za msingi.

Ameongeza kuwa kuna idadi kubwa ya wabunge wamekuwa wakikiuka kanuni za bunge makusudi na kusababisha kuleta vurugu bungeni wakati jamii ikiendelea kutazama mabishano yasiyokuwa na hoja za msingi.

Dk Kashilila amesema kuwa kwa sasa kuna baadhi ya kamati za bunge ambazo zimevunjwa kutokana na baadhi ya kamati hizo kuingilia katika utendaji jambo ambalo limekuwa likipoteza maana ya kamati hizo.

Hivi karibuni baadhi ya kamati ikiwemo ile ya Mashirika ya umma POAC zimefutwa na kuacha maswali mengi kwa baadhi ya wananchi juu ya hatua hiyo.
 
BUNGE linatarajia kufuta utaratibu wa
kurusha matangazo ya moja kwamoja
kupitia televisheni kwa madai ya
kukomesha vitendo vya baadhi ya wabunge
kukiuka kanuni za bunge na kuleta vurugu
kwa kutafuta umaarufu bila kujua kwamba
tabia hiyo inaleta picha mbaya katika jamii.

Hayo yamesemwa na Katibu wa Bunge
Dk.Thomas Kashilila jijini Dar es salaam
wakati akitoa taarifa ya mapendekezo ya
kuanzisha kamati ya bajeti na kuvunjwa
kwa baadhi ya kamati za bunge.

Amesema kuwa ili kuleta maadili kwa
baadhi ya wabunge ambao wamekuwa
wanashindwa kufuata kanuni za bunge na
kutumia nafasi hiyo kwa kutafuta umaarufu
kwa sasa wameomba kufutwa utaratibu wa
kurusha matangazo ya bunge ya moja kwa
moja badala yake watarekodi ili kuondoa
hoja zisizokuwa za msingi.

Ameongeza kuwa kuna idadi kubwa ya
wabunge wamekuwa wakikiuka kanuni za
bunge makusudi na kusababisha kuleta
vurugu bungeni wakati jamii ikiendelea
kutazama mabishano yasiyokuwa na hoja za
msingi.

Dk Kashilila amesema kuwa kwa sasa
kuna baadhi ya kamati za bunge ambazo
zimevunjwa kutokana na baadhi ya kamati
hizo kuingilia katika utendaji jambo ambalo
limekuwa likipoteza maana ya kamati hizo.
Hivi karibuni baadhi ya kamati ikiwemo ile
ya Mashirika ya umma POAC zimefutwa
na kuacha maswali mengi kwa baadhi ya
wananchi juu ya hatua hiyo.
Mwisho.
 
This is silly!! Kama kanuni zipo na zinavunjwa, kwa nini wahusika wasichukuliwe hatua kwa mujibu wa taratibu za uendeshaji wa bunge badala ya kuwaadhibu wananchi kwa kuwanyima haki ya kujua nini kinaendelea bungeni kwa wakati huo (live dialogue) kwa maendeleo ya wananchi wenyewe. Ama ukubwa wa pua si wingi wa makamasi. Magamba walidhani kuwa wengi bungeni watakuwa na hoja za maana kumbe wengi wao ni Low Thinkers!!, Chezea CDM!!
 
Halafu "oooh, Tanzania ni nchi yenye uhuru wa habari".

Nyoooo.

Nani ataondoa hoja "zisizo za msingi"? Kwa muongozo gani?

Kama kuna wabunge wenye "hoja zisizo za msingi" kwa nini bunfe lisiache wananchi waone wabunge wao wanavyotoa "hoja zisizo za msingi" live ili kuwaelewa zaidi na kuweza kuamua vizuri zaidi kama wataendelea kuwachagua au watawamwaga uchaguzi ujao?

Kwa nini bunge linaingilia uhuru wa vyombo vya habari?

Kwa nini wanahabari wasilishitaki bunge mahakamani?

Kwa nini wabunge wasitunge sheria ya "freedom of information" itakayohakikisha bunge haliwezi kupitisha maazimio ya kidikteta kama haya?
 
Yani maccm always kila siku hawfirii! Hivi awaju kama ni haki yetu kuona wabunge wanavyo peleka kero zetu bungeni?

Hivi ubabe wa makinda na ndugai suluhu yake ni kutoonesha vipindi vya bunge kwenye tv.. Huu ni uwenda wazimu kabisa!
 
Huyo kweli hana akili

- Ni haki yetu watanzania kuona mhimili huu unafanya kazi sahihi moja kwa moja na si vinginevo

- Wanatumia fedha za walipa kodi kwanini watuwekee masharti? kwanza itatuongezea sababu za kuiondoa ccm 2015.

- Kama sheria, kanuni na taratibu zinafuatwa hofu ya nini kama sio kuweweseka? wafanye waone matokeo yake.

Vyovyote vile huwezi kuwazibiti watu wazima na akili zao kwa mbinu dhaifu kama hiyo chadema ni vichwa makini

watatoka na mkakati makali zaidi.
 
“Anyone who stops learning is old, whether at twenty or eighty. Anyone who keeps learning stays young.”
― Henry Ford

Naona ccm na serikali yake imezeeka vya kutosha. Kuturudisha zama za kale za mawe ni ishara ya woga, kufilisika, kukosa fikra sahihi zinazohitajika katika dunia ya leo. Hawa hawana sababu ya kuendelea kuwapo madarakani. Wanaweweseka, tunahitaji kuona NGUVU YA UMMA sasa.
 
Tutaandamana mpaka kieleweke Bunge linajadili mambo yanayohusu shida za watanzania na wnaoona ni watanzania na wabunge wenyewe wanawakilisha watanzania, hapa wanataka kuficha nini? nasema watanzania tutasimama wote kuhakikisha hii kitu haipiti.
 
Siri itakuwa tatizo zaidi kwa jamii? hivyo ni vigumu kuzuia kitu ambacho baada ya muda itabidi kiruhusiwe!. Wabunge hawaendi bungeni kuchekeena wakati nchi ina rushwa, viongozi hawafanyi kazi na mikataba mibaya inatengenezwa. Wabunge wakitaka sifa kwa jamii kwa kukomesha kiwango kidogo cha elimu kuna ubaya gani?? Bunge gani la nchi ya kidomokrasia ni la siri? Rusia watu wanapigana bungeni, UK watu wanatukananana na waziri mkuu, US kuna matusi bungeni. Huwezi kusema kitu kibaya kwa jamii wakati wabunge ni wa wakilishi wa jamii. Hakuna Demokrasia safi.
 
Hatimaye Serikali ya Chama cha Mapinduzi imeamua kusitisha kurusha matangazo ya Moja kwa Moja kutoka MJENGONI Dodoma!Maana yake nn?ni kuwa wamechoka kuona wanavyodhadhalishwa na wapinzani!Kweli ndugu Zangu wa CCM wamefirisika kifikra nachoamini mimi Apetizer kuwa kulikimbia tatizo sio njia sahihi ya kulisolve bali ni kuliongeza na kulifanya kuwa kubwa!Hakika mwisho wa CCM umefika wanachokifanya ni kutapatapa tu!Wekeni hoja acheni usanii kama mwenyekiti wenu!
 
Back
Top Bottom