Bongo usijaribu kukata tiketi VIP, utatapeliwa

Lycaon pictus

JF-Expert Member
Jan 31, 2021
7,388
13,030
Wabongo huwa hawajali kumhudumia mtu. Ukiisha walipa imetoka hiyo. Juzi kati Yanga walikuwa na mechi watu waliingia bure na VIP walilipia. Watu wa VIP kufika uwanjani wanaambiwa siti za VIP zimejaa, hawataweza kuingia.
Jana Cheka Tu walikuwa na show yao mlimani siti. VIP 40k regula 20K. Kama kawaida, baadhi ya VIP's wameingia wanaambiwa siti za VIP zimejaa. Hiyo ni mifano tu ya karibuni. Ila tatizo la kukatisha watu tiketi za VIP na kuwaambia siti zimejaa au kuwapa service chini ya kiwango ni kubwa sana nchini, kusema VIP ni namna ya utapeli hapa bongo.

Kuna kipindi Simba SC walikuwa na VIP experience, waliifanya vizuri sana. Watu walichukuliwa hotelini kwenda uwanjani na baada ya mechi wakarudishwa.

Bongo usikate tiketi za VIP, sehemu kubwa utatapeliwa.
 
Ndio maana mm nimeacha kukata Ticket za VIP.

20240417_130436.jpg


KaziKweliKweli/JobTrueTrue
 
Bongo kwanza picha linaanza hata hawaelewi maana ya VIP achana na VVIP, ukikosa siti utaambiwa "kwani kule kwingine hamna siti? Nenda ukakae huko! Sio lazima huku" 😀
 
Back
Top Bottom