Blackberry na Nokia zilipendwa sana miaka ya nyuma, ila walikuja kuanguka vibaya sana

Arnold Kalikawe

Senior Member
Sep 28, 2016
147
341
Blackberry na Nokia yameanguka, tena yameanguka sana. Pamoja na kuwa na simu kali zenye kamera nzuri, speed kubwa ila wakaanguka.

Walianguka kwa sababu hawakuwa na viongozi wenye kufocus ulimwengu jinsi ulivyo. Yaani walikuwa katika miaka ya 2000 lakini akili zao zilikuwa zinafanya kazi ya miaka 1990.

Wakati teknolojia inakuwa, watu wanaamua kumove kutoka sehemu moja kwenda nyingine, wao walibaki palepale kwa kuamini kwamba ni kampuni kubwa na watu watakuja wenyewe.

Hili ni kosa kubwa sana walilofanya. Unapokuwa kiongozi wa kampuni yotote ni lazima uwe na focus kubwa, kwamba dunia ipo hapa, itakapobadilika, na wewe unatakiwa kubadilika haraka.

Mabosi wenye akili za miaka ya 90 bado wanaamini huwezi kufanyia kazi nyumbani. Yaani kazi ya kufanyia nyumbani, ni lazima ufike ofisini. Ila mabosi wenye akili ya miaka 2020, wewe fanyia kazi nyumbani, itume kwenye email mambo yaendelee.

Una kipaji cha uandishi, muziki, ni lazima ujue kwamba dunia imebadilika. Leo tukiandika hadithi ama vitabu, hatuwezi kuandika kama akina Ben Mtobwa kwa sababu wao walikuwa wanaandika kulingana na ulimwengu wao, miaka yao, ila leo ukiandika, ni lazima uandike kupitia ulimwengu wako na miaka yako.

Leo unapofungua biashara mahali, usitake kufanya biashara kama ya miaka 90, ni lazima ujue dunia imebadilika, natakiwa kufanya biashara kisasa.

Si mpaka mteja aje dukani ndio aone bidhaa yako, inatakiwa utumie hata mitandao kuwaonyesha bidhaa zako.

We have to change, we have to accept the time. Kila unachokifanya, kumbuka hii ni miaka ya 2020 na si miaka ya 2000.

Nokia na Blackberry kiliwafelisha hicho tu. Tulikuwa miaka ya 2010, wao bado walistuck miaka ya 2000.

1714646846122.jpg
 
Mkuu ni ushindani wa soko hasa kwa nokia kwani bado wana simu zenye maunyama. Umeweka picha ya nokia asha na blackberry je kwa kipindi hicho kulikuwa na nini sokoni.?
 
Back
Top Bottom