Mwanzo nilipokuwa nasoma kitabu cha ufunuo,niliona mahali pakiandikwa kana kwamba ujio wa Yesu,utakuta baadhi ya watu ni watumwa na watwana na wengine mabwana.Nilijiuliza sana jambo hili linawezekanaje katika dunia hii ya sasa watu kuchezea mijeledi kama enzi za zamani!?
Hata hivyo sasa ninaona kila kitu kinawezekana.Historia hujirudia.Kama watu wako tayari kuandamana kufurahia kutawaliwa,hili ni jambo la kusikitisha sana.
Tumekiri kabisa kuwa akili zetu,na maarifa yetu yamefikia mwisho na suluhisho ni kuwakabidhi wanaoweza kufikiri kwa niaba yetu watusaidie kufanya hivyo.
Kwa sasa sioni sababu ya kuwekeza matrilioni ya pesa vyuo vikuu kwani kwa sehemu kubwa havina tija kabisa katika nchi hii.
Serikali iwekeze kwenye fani muhimu kama za udaktari Kilimo na Jeshi tu ambako fani mbali mbali hufundishwa.
Ninaamini kizazi kijacho kitatushangaa sana kwamba mtu anasoma hadi chuo kikuu halafu mshauri wake kwenye masuala nyeti kabisa ya nchi,ni machawa wengi wao darasa la saba.