Biashara haramu ya mbao kwenda China inavyofadhili uasi Msumbiji

ndege JOHN

JF-Expert Member
Aug 5, 2015
19,945
45,921
Usafirishaji wa mbao, unaokadiriwa kuwa na thamani ya dola za kimarekani milioni 23 kwa mwaka, kutoka misitu ya kale ya Msumbiji hadi China unasaidia kufadhili waasi wa itikadi kali za Kiislamu pamoja na mtandao mkubwa wa uhalifu kaskazini mwa nchi hiyo.

Biashara hii haramu ya miti ya inahusishwa na wanamgambo wa Msumbiji wenye mafungamano na kundi la Islamic State katika jimbo la kaskazini la Cabo Delgado, kulingana na taarifa iliyopatikana na BBC kutoka Shirika la Uchunguzi wa Mazingira (EIA).

Miti migumu ya kitropiki inapendwa sana kutengenezea samani za kifahari nchini China. Misitu ya Msumbuji inalindwa chini ya mkataba wa kimataifa, ikimaanisha kuwa miti hiyo hukatwa kwa biashara ndogo tu ambayo haitishii uhai wa misitu.

Hata hivyo, uchunguzi wa siri wa miaka minne wa EIA katika nchi zote mbili umebaini kuwa kuna usimamizi mbovu wa makubaliano ya misitu, ukataji miti haramu na ufisadi miongoni mwa maafisa wa bandari na kufanya biashara hiyo kupanuka bila kudhibitiwa katika maeneo yanayokadhibitiwa na waasi.

Ufichuzi huo unakuja wakati kumezuka upya mapigano kaskazini mwa Msumbiji. Siku ya Ijumaa, waasi wasiopungua 100 walifanya shambulio kubwa zaidi katika kipindi cha miaka mitatu kwenye mji wa Macomia, ambalo hatimaye lilizimwa na jeshi.
"Eneo la shambulio hilo linathibitisha kwamba uasi umesogea kusini zaidi kutokana na kuongezeka kwa wanajeshi kaskazini mwa nchi hiyo. Pia waasi wamepata fedha za kutosha kuajiri katika jimbo jirani la Nampula kusini zaidi," kulingana na mchambuzi wa kutoka Msumbiji, Joe Hanlon.
 

Attachments

  • db9932f0-1287-11ef-82e8-cd354766a224.png
    db9932f0-1287-11ef-82e8-cd354766a224.png
    261.6 KB · Views: 6
  • d7289260-1287-11ef-bee9-6125e244a4cd.png
    d7289260-1287-11ef-bee9-6125e244a4cd.png
    501.6 KB · Views: 6
Back
Top Bottom