DOKEZO Bandari ya Dar kuna Urasimu, mizigo inatoka taratibu sana. Serikali, nini kinaendelea?

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
A

Anonymous

Guest
Bandari ya Dar es Salaam ina changamoto kubwa ya mizigo kuchelewa, hii ni kero ambayo imekuwepo kwa miezi kadhaa sasa na Serikali na mamlaka zipo kimya, kiasi kwamba imefikia hatua baadhi ya watu wenye meli kubwa wanaamua kwenda Mombasa.

Mimi ni mmoja wa waathirika wa changamoto hiyo, kuna mazingira ya urasimu yanayoendelea Bandarini.

Kwa kawaida mzigo unatakiwa kutozidisha wiki moja au au mbili lakini kwa sasa kukaa zaidi ya mwezi au miezi miwili au mitatu.

Kampuni ninazofanya nazo kazi kwa ajili ya kutoa mizigo zimekuwa zikilalamika kuzungushwa na wanaohusika, inavyoonekana kuna mchezo wa kukomoana.

Kuna ndugu yangu naye ameagiza mzigo umefika Bandarini tangu Novemba 2023 na alitarajiwa kuutoa Desemba 2023 lakini hadi sasa Januari inaelekea Februari 2024 mzigo haujatoka na hakuna maelezo anayopata ya maana kama ninayopata mimi.

Baadhi ya Maafisa wengine wanadai makontena ni mengi ndio maana hata mchakato wa kutoa unakuwa taratibu.

Jambo lingine ni kuwa baadhi ya Maafisa wa Bandari wamezidisha tabia ya kuiba vifaa na mali zinazoingizwa kwa kigezo kuwa wanakagua na kupima ubora.

Wamekuwa wakifungua baadhi ya mizigo kwa lengo la kukagua, kinachotokea baada ya hapo wakiondoka na sample hiyo hawarudishi, hivi wanadhani sisi tunapewa bure huko zinazotoka.

Pia, soma: Bandari ya Dar Es salaam sasa inafanya kazi 24/7
 
Walikuwa wanasema itafika kampuni ya DP World.
Yale mazungumzo yaliisha vipi?
Nipo Arusha sasa hivi. Lakini nilipokuwa Dar,miezi michache iliyopita, nilikuwa naona zile meli zinaongezeka siku baada ya siku,ambayo ilikuwa haipaswi kutokea kama dili ya DP World imeshakamilishwa kama inavyodaiwa.
Kwa sababu nikiwa Dar pale,naishi beach,na zile meli naziona from my bedroom window.
Nahesabu meli kumi kule nje,najiuliza kuna nini?
Naongea kuhusu zile meli ambazo zipo pale daraja la Tanzanite.
 
Watching meli from yo bedroom window. Nmeipenda hii big up broo sio mtu akichungulia kwa window yake anakutana na kijiwe Cha gongo. Jungu la maharagwe la mama amina mchafu au anakutana na dambo la taka
 
Bandari ya Dar es Salaam ina changamoto kubwa ya mizigo kuchelewa, hii ni kero ambayo imekuwepo kwa miezi kadhaa sasa na Serikali na mamlaka zipo kimya, kiasi kwamba imefikia hatua baadhi ya watu wenye meli kubwa wanaamua kwenda Mombasa.

Mimi ni mmoja wa waathirika wa changamoto hiyo, kuna mazingira ya urasimu yanayoendelea Bandarini.

Kwa kawaida mzigo unatakiwa kutozidisha wiki moja au au mbili lakini kwa sasa kukaa zaidi ya mwezi au miezi miwili au mitatu.

Kampuni ninazofanya nazo kazi kwa ajili ya kutoa mizigo zimekuwa zikilalamika kuzungushwa na wanaohusika, inavyoonekana kuna mchezo wa kukomoana.

Kuna ndugu yangu naye ameagiza mzigo umefika Bandarini tangu Novemba 2023 na alitarajiwa kuutoa Desemba 2023 lakini hadi sasa Januari inaelekea Februari 2024 mzigo haujatoka na hakuna maelezo anayopata ya maana kama ninayopata mimi.

Baadhi ya Maafisa wengine wanadai makontena ni mengi ndio maana hata mchakato wa kutoa unakuwa taratibu.

Jambo lingine ni kuwa baadhi ya Maafisa wa Bandari wamezidisha tabia ya kuiba vifaa na mali zinazoingizwa kwa kigezo kuwa wanakagua na kupima ubora.

Wamekuwa wakifungua baadhi ya mizigo kwa lengo la kukagua, kinachotokea baada ya hapo wakiondoka na sample hiyo hawarudishi, hivi wanadhani sisi tunapewa bure huko zinazotoka.

Warabu wapo bize wanakunywa kahawa usitegemee ufanisi wowote,viongozi wetu waliingiwa tamaa ya fedha wala sio lengo la kuboresha bandari.
 
Alijitokeza Lukosi kulalamikia hili nafikiri alitishwatishwa huko chamber akaibuka tena kupiga pambio!

BTW: Hii inaweza kuhusiana kwa vyovyote na ile meli kubwa iliyotia nanga juzi na kusepa faster ilhali wenyewe walikuwa tayari wameanza porojo za watalii 2000?
 
Zamani JF ilikua ikileta mada za kiuchunguzi zilikua detailed with facts and evidence

Nowadays kunakua na rather speculative posts
 
Dp world imeanza kazi December sio rahisi hivyo...Pale bandari uwizi ni mwingi haya mambo ya physical inspection na verification ni ujinga kamaa hawana screening basi wache huwezi kufanya ujinga kufungua container moja badala.

Hata hao Dp world wamepewa gati kadhaa kwa iwe hivyo? Kuna ulazima gani meli zifike Dar hata kijiografia kwa usawa meli zinaweza hata kutia nanga Tanga .
 
Mkuu hii habari yako inaumiza kwa mfanyabiashara. Ungeweka taarifa kamili ni hatua ipi mzigo wako umekwama kwenye kutoka.

Suala la Physical Verification ni kawaida ila wakaguzi kuna kiwango cha kuchukua sample na sample ikitoka kuna kiwango kinabakishwa endapo tatizo litatokea ibaki kama sehemu ya kurudia.
 
Dah

Hueleweki kabisa unaongea nini
 
Hizo process ni prolonged ,mfano kuna eneo ya kufanya physical verification mpaka mzigo upelekwe pale unakuta containers ni nyingi ....Zile screening ni za nn pale ? Unaweza kuambiw cranes leo inazingua hawawezi kushusha au kweny containers ttu wakashusha moja.

Ili Dp world aweze kuendana na kasi hiyo lazima aweke mifumo yake sio ujenzi wa kitoto wa hiyo miundombinu sio leo wale kesho.

Wengi wanafikria Dp world 😅😅😅anabadlisha kwa wiki mpaka aweke hiyo mifumo yake ni mwakani tena.
 
Dah

Hueleweki kabisa unaongea nini
Dp world hauhusiki maana kufungua container moja baada ya moja ndio foleni zile cranes zinasumbua hata wafanye akzi masaa 24...Kufanikiwa kwa Dp world ni kuleta miundombinu mipya..

Je pale bandari umeona miundombinu mipya?
 
Wiki inaisha hatuna maji huku makuburi,ubungo na sisi huu urasimu unatuchosha sana ase. Yaani dawasco saivi bora tanesco
 
Bandari ya Tanzania wanatoa siku 7 bure kwa mzigo wa ndani kukaa pale kisha siku zinazofata utalipia storage charges.

Sidhani kama bandari wanaweza wakachelewesha mzigo uliochini ili wapate pesa ya storage. Kama ni ofisa fulani alikwamisha ni vyema ukaweka wazi kwa kumuuliza Wakala wako wa Forodha (Clearing Agent) wapi walimkwamisha.

Unaweza kuta agent alichelewa kufata release order, kuingiza documents, kufatilia na kulipia huduma ya verification.

TPA kwenye mfumo wa kuondoa mizigo saizi wamekuja na mfumo ambao hautaji sana paper work Kwenye kuingiza au kutoa mzigo.
 
Hizo process ni prolonged ,mfano kuna eneo ya kufanya physical verification mpaka mzigo upelekwe pale unakuta containers ni nyingi ....Zile screening ni za nn pale ? Unaweza kuambiw cranes leo inazingua hawawezi kushusha au kweny containers ttu wakashusha moja.

Ili Dp world aweze kuendana na kasi hiyo lazima aweke mifumo yake sio ujenzi wa kitoto wa hiyo miundombinu sio leo wale kesho.

Wengi wanafikria Dp world 😅😅😅anabadlisha kwa wiki mpaka aweke hiyo mifumo yake ni mwakani tena.
Mabadiliko sio haraka kama wengi tunavyofikiri ni kitu cha kukipa muda.

Kwenye Cranes kwa sasa naona wamejitahidi sana ikiwa na kuleta reach stackers mpya.

Physical verification haikwepeki nadhani uwekwe utaratibu mpya wa kutoa foleni ya ukaguzi wa Physical iwe ni kutenga ICD za kukagulia. Containers zote zenye kuhitaji Physical verification inabidi zipelekwe ICD X,Y,Z.

Kwenye bidhaa za kutumia binadamu, wakati wa shipping kuna masharti ya kusafirisha baadhi zinataka joto kiasi fulani, muda wa kukaa njiani hivyo lazima zikifika nchini wakaguzi hukagua kwa macho na kuchukua sampuli
 
Kweli
 
Back
Top Bottom