Bado yuko fresh, baada ya miaka mia moja ya kifo chake

Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Feb 4, 2009
75,016
156,388
UNAWEZA KUDHANI AMELALA, KUMBE AMEKUFA.
1714493296622.jpg
Ni miaka mingi toka afariki dunia, lakini hakuzikwa. Badala yake serikali iliamua kuuhifadhi mwili wake ili uwe ukumbusho kwa vizazi vijavyo. Hiyo ni kutokana na umuhimu na mchango mkubwa aliokuwa nao mtu huyu katika taifa lake.

Ni miaka 100 sasa, mwili huo umehifadhiwa huko Urusi, katika eneo la Red Square lililopo mjini Moscow.

Huo ni mwili wa Vladimir Lenin Ilyich aliyekuwa kiongozi wa kwanza wa muungano wa usovieti U.S.S.R.

Mnamo mwezi machi 1923, Lenin alipata tatizo la kupooza 'stroke' na kupoteza uwezo wake wa kuongea. Hatimaye tarehe 21 Januari 1924 alifariki dunia. Baada ya kufariki, bwana Joseph Stalin alichukua madaraka, na serikali ikakusudia kuhifadhi mwili wake ili ubaki kumbukumbu kwa vizazi vijavyo.

Ikatangazwa tenda ya ujenzi wa chumba maalumu cha kuweka mwili huo. Alexey Shchusev akapata tenda hiyo na kuanza ujenzi wa 'mausoleum' jengo la kuhifadhi mwili wa marehemu, na ujenzi ulikamilika mwaka 1930.

Jukumu la kutunza na kuhudumia mwili huo wamepewa kundi la wanasayansi kutoka taasisi ya Moscow’s Institute of Medicinal and Aromatic Plants. Wanasayansi hawa ndio ambao walihusika na kuutunza mwili wa Rais Ho chi mihn wa Vietnam.

Kila wiki, walikuwa wanaukagua mwili wa Lenin, na kuhakikisha upo katika hali inayotakiwa. Mwili wa Lenin umehifadhiwa ndani ya (sarcophagus) kioo maalumu.

Mwanzoni mwa miaka ya 1990, kuliibuka kwa mjadala mkali nchini Urusi ambapo kuna watu walikuwa wanataka kuuondoa mwili huo na kwenda kuuzika, huku wengine wakitaka mwili uwepo ili watu waendelee kuuona.

Aliyekuwa rais wa wakati huo bwana Boris Yeltsin wala hakuthubutu kuingilia mzozo huo kwa kuhofia hasira za wanachama wa chama cha kikomunisti. Pia hata Rais Vladimir Putin naye hakutaka kujihusisha na swala hilo huku akisema kuwa uamuzi wa kuzika mwili wa Lenin upo kwa wananchi wenyewe.

***

Naam, hivyo ndivyo jinsi mwili wa Vladimir Lenin ulivyohifadhiwa na kutunzwa. Utaalamu huu wa kutunza maiti unajulikana kama 'mummification' ulianzishwa na wamisri wa kale ambapo miili ya mafarao ilihifadhiwa na ipo hadi leo hii.

Marais kadhaa walifanyiwa mummification, ikiwemo Agostino Neto wa Angola na Kim II Sung wa Korea kaskazini.

***

Ahsante.
 
Back
Top Bottom