SteveMollel
JF-Expert Member
- Jul 12, 2015
- 8,534
- 23,980
Baada ya kutokea kwa mauaji ya watu kadhaa, polisi wanafika eneo la tukio kwa lengo la kufanya uchunguzi.
Katika eneo hilo wanakutana na miili isiyopungua mitatu, yote imelala mfu, wanaikagua na kujiridhisha.
Wanaupata mwili mwingine ndani ya 'basement', mwili wa msichana mzungu, makadirio ya miaka ishirini, wanaukagua na kubaini mwili huo una tofauti na miili mingine yote.
Moja, mwili huu hauna mahusiano yoyote na eneo hili ulipokutwa. Si mkazi, jirani wala rafiki.
Pili, mwili hauna alama yoyote ya majeraha yenye mahusiano na kifo cha marehemu.
Tatu, hamna rekodi yeyote ya kutambua mwenye mwili huo ni nani. Kwasababu hiyo Polisi wanaukatia jina la kubuni: Jane Doe kisha wanaubeba na kuupeleka kwa wataalamu kwaajili ya uchunguzi zaidi. Zoezi hilo linaitwa 'Autopsy'.
Upande wa pili, wataalamu wa kuchunguza miili iliyokufa, Austin pamoja na baba yake mzazi, wapo kazini majira haya ya usiku.
Yani wakati wewe unarithi shamba kwa mzee wako, mwenzio anarithi mochwari kupambana na maiti. Uzuri pale bar mhudumu haulizi pesa ya bia umeitolea wapi.
Hapo kazini anakuja msichana mmoja mrembo, 'girlfriend' wa Austin, kwa lengo la kumpitia mpenziwe waende zao mtoko.
Msichana huyo anaona maiti moja imefungwa kengele ndogo mguuni. Anashangaa na kuuliza, hii ni nini?
Baba Austin anamtoa shaka, hiyo ni teknolojia ya zamani. Maiti ilifungiwa kengele ili kama mtu hajafa na ikatokea ameamka basi waliokaribu watasikia kengele na kuja upesi kumsaidia.
Haipiti muda, mwili mpya unaingizwa eneo hili kwaajili ya kutendewa kazi. Kwasababu hiyo, Austin anamwomba mpenziwe arudi baadae kwani kwa sasa kuna kazi ya kufanya.
Mwanamke anaaga na kazi inaanza rasmi.
Kufungua mfuko, ni mwili wa Jane Doe.
Wanaupekua.
Mwili hauna kovu lolote. Maungio ya mikono na miguu yamevunjika. Mdomoni jino moja halipo. Viini vya macho yake vina rangi ya kufifia.
Wanamchana kukagua viungo vyake vya ndani, wanakuta vina ishara na alama za kuungua. Wanastaajabu ameunguaje ndani wakati nje hana hata doa?
Mara wanasikia sauti ya purukushani juu ya paa, Austin kwenda kutazama anamkuta paka wa baba yake amekufa.
Baba anahuzunika maana paka huyu alikuwa ni kumbukumbu ya marehemu mkewe. Anaomboleza kidogo kisha anarejea tena kazini kuendelea na uchunguzi wa Jane Doe.
Mara hii, anakumbana na kitambaa kidogo kilichojifunga. Kukitazama ndani kuna alama na michoro pia kuna lile jino lililong'olewa mdomoni mwa marehemu.
Hii inamaana Jane Doe katika enzi ya uhai wake, alimeza au alimezeshwa kitambaa hicho na jino lake. Kwanini? Hamna anayejua.
Wanakagua ngozi yake kwa ndani, wanaona ina alama zilezile zilizochorwa katika kile kitambaa kidogo.
Wakiwa wanaendelea kupembua, wanashtuka taa zinakonyeza. Mara moja. Mara mbili. Mara tatu. Mara zinapiga shoti na giza totoro linameza chumba kizima kufumba na kufumbua!
Sasa hamna kuonana bali kukisia. Hamna kushika bali kupapasa.
Hata kama ni wewe, tumbo lisingeitika abeeh?
Baba anawasha 'lighter' wapate ahueni ya kutazama japo mwanga wake ni hafifu.
Wanaangaza macho, mwili wa Jane Doe upo palepale walipouacha, ila wanapoangaza kwenye makabati ya kuhifadhi maiti, mambo yapo kinyume.
Milango ipo wazi na miili yote haipo!
Hapa ndo mate yanatawanyika mdomoni, ulimi unabaki kuwa mkavu. Mapigo ya moyo yanahamia tumboni, na baridi lisiloeleweka linakupapasa miguuni mpaka kichwani.
Wanakimbilia kwenye lifti, milango haifungi. Huko nje, mvua kubwa inanyesha, imeangushia mti mkubwa kwenye mlango wa dharura, mlango hauwezi kufunguka.
Tazama simu, mtandao uko chini vibaya mno, ukipiga inajikata tu yenyewe.
Wafanye nini?
Wanarudi kwenye chumba cha maiti kukabiliana na Jane Doe kwani mwili wake ndo' umeleta balaa. Wanaumwagia mafuta na kuupiga kiberiti!
Moto unasambaa. Wanahaha tena kuuzima kwa 'fire extinguisher'. Moto unakata lakini wanashangaa mwili wa Jane Doe uko vilevile, hauna chunusi, harara wala tangotango!
Kidogo wanasikia sauti ya lift, wanakimbilia huko upesi kujiokoa. Kufika lift haipandi wala haishuki.
Wanaangaza ndani ya kiza hiki kinene.
Jasho jembamba linachuruza.
Mara wanasikia sauti ya kengele.
Sauti ya kengele inasogea.
Unaikumbuka kengele hii? Unaikumbuka kazi yake ni nini?
Baba anashikwa na hofu kali, anarusha shoka lake gizani, shoka linakita humo na mara kunakuwa kimya. Kengele inanyamaza.
Wanatoka kwenda kutazama, wanakuta mwili wa mchumba wake Austin umelala chini. Shoka limemgonga na anavuja damu akifa.
Maskini. Alikuja kumpitia mpenzi wake kama walivyoahidiana, sasa yuko chini anakata kauli.
Kuna atakayenusurika humu?
Jane Doe ni nani? Anahusika nini na mauaji haya?
Nisikupotezee muda, kaitazame Movie ya; "The Autopsy of Jane Doe".