Babu Tale afunguliwa maombi mengine ya kufungwa Mahakama Kuu

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,435
8,254
Baada ya kuponea chupuchupu kutupwa jela mwaka 2018, sasa mbunge wa Morogoro Kusini Mashariki, Hamisi Shabani Taletale, maarufu kama Babu Tale anachungulia tena jela baada ya mchakato kumtupa jela kuanza tena upya.
Babu Tale ambaye ni mmoja wa wakurugenzi wa kampuni inayojihusisha na shughuli za burudani, Tip Top Connections Company Limited yuko hatari kufungwa jela kutokana na kushindwa kumlipa mhadhiri wa dini ya Kiislam, Sheikh Hashim Mbonde, fidia ya Sh250 milioni.

Tayari Sheikh Mbonde ameshafungua maombi Mahakama Kuu akiiomba mahakama hiyo iamuru Babu Tale ambaye pia ni meneja wa msanii maarufu wa muziki wa kizazi kipya (Bongo fleva), Abdul Nassib maarufu kama Diamond Platnumz akamatwe na afungwe kwa kushindwa kumlipa fidia hiyo.

Sheikh Mbonde amefungua maombi hayo dhidi ya Tip Top na Babu Tale baada ya Mahakama ya Rufani kutupilia mbali taarifa yao ya kusudio la kukata rufaa kupinga hukumu ya Mahakama Kuu iliyowaamuru kulipa fidia hiyo, Agosti 17, 2022.

Mahakama hiyo iliitupilia mbali taarifa hiyo ya kusudio la kukata rufaa, kufuatia maombi ya Sheikh Mbonde, baada ya kukubaliana na hoja zake kuwa kina Babu Tale hawakuweza kuchukua hatua muhimu ndani yaani kuwasilisha sababu za rufaa ndani ya muda.

Maombi hayo ya madai anuani namba 467 ya mwaka 2022 ya Sheikh Mbonde yaliyopangwa kusikilizwa na Jaji Obadia Bwegoge yamepangwa kutajwa mahakamani hapo Novemba 29, 2022.

Hata hivyo baada ya Mahakama Kuu kutupilia mbali taarifa yao ya kusudio la kukata rufaa, kina Babu Tale nao wamewasilisha maombi mengine ya kibali cha kuwasilisha taarifa ya kusudio la kukata rufaa nje ya muda.

MWANANCHI
 
Toka maktaba

24 May 2018

Sheikh Mbonde alivyojipanga kutumia mamilioni Babu Tale akae jela​

Alhamisi, Mei 24, 2018 — updated on Februari 22, 2021

Muktasari:​

Ameshalipa Sh1,080,000 na kusema ataendelea kuwalipia kiasi kama hicho kila mwezi
Dar es Salaam. Baada ya mkurugenzi wa kampuni ya Tiptop Connection Limited, Hamis Shaaban Taletale maarufu kwa jina la Babu Tale, kukaa mahabusu katika kituo cha Polisi akisubiri amri ya kupelekwa kifungoni, mdai katika kesi hiyo amesema atatumia mamilioni kuhakikisha anakaa jela.

Hukumu hiyo iliyotolewa na Jaji Augustine Shangwa Februari 18, 2016, iliamuru Babu Tale na ndugu yake Idd Taletale kumlipa fidia ya Sh250 milioni, Mhadhiri wa Dini ya Kiislamu, Sheikh Hashim Mbonde kwa makosa ya kutumia mahubiri yake kibiashara bila ridhaa yake.

Hati ya kuwakamata Babu Tale na ndugu yake ilitolewa Aprili 4, mwaka huu kutokana na maombi ya Sheikh Mbonde kupitia wakili wake, Mwesigwa Muhingo.

Sheikh Mbonde aliwasilisha maombi hayo baada ya Babu Tale na nduguye kushindwa kutekeleza hukumu hiyo, yaani kumlipa kiasi hicho walichoamriwa na Mahakama wala kubainisha mali za kampuni yao, au zao binafsi, ili zipigwe mnada kulipia fidia hiyo.

Baada ya Sheikh Mbonde kuwasilisha maombi ya kuwafunga jela Babu Tale na nduguye, mahakama ilimwelekeza kuwalipia wafungwa hao watarajiwa fedha za chakula na matumizi mengine kuziwasilisha gerezani. Kwa mujibu wa Mahakama, gharama za kuwahudumia wafungwa hao wakiwa gerezani ni kama ifuatavyo:

Vifaa ambavyo ni taulo ya kuogea Sh12,000; godoro Sh40,000; mto wa kulalia Sh10,000; chandarua Sh13,000; mashuka manne Sh48,000; kandambili (malapa) Sh3,000; mswaki na dawa ya meno Sh2,000 ambazo jumla ni Sh128,000 kwa mtu mmoja na kwa watu wote wawili ni Sh256,000.

Chakula, kifungua kinywa Sh7,000; chakula cha mchana Sh8,000; maji lita tatu 3,000, jumla Sh18,000 kwa mtu mmoja kwa siku na kwa wote wawili ni Sh36,000. Wote kwa mwezi ni Sh1,080,000. Pia, kuna fedha za tahadhari kiasi cha Sh800,000 kwa kila mfungwa na kwa wote wawili jumla ni Sh1,600,000.

Sheikh Mbonde alisema kuwa tayari ameshawalipia wafungwa hao fedha za chakula za mwezi mmoja kiasi cha Sh1,080,000 na kusema ataendelea kuwalipia kiasi kama hicho kila mwezi.

Alisema fedha za matumizi mengine kama yalivyoainishwa na mahakama, ziko tayari na kwamba hizo ataziwasilisha kwa uongozi wa gereza baada ya wafungwa hao kufikishwa huko
 
Dah!Kwa hiyo sheikh anataka babu Tale akahenye kupango aka msambweni?Awe mwenye kusamehe na wakae wayamalize.
 
Awamu hii ya sita unaweza kusikia Taletale naye anakwenda mahabusu kama vijana wengine wa UVCCM waliokuwa MaDC, Wakurugenzi wa Manispaa n.k huku wakishangaa mbona awamu ya tano walikuwa hawaguswi
 
sinza pazuri njoo umtetee meneja wa Asake wa Tandale anaburuzwa jela uchawi umebuma safari hii.
A6802C52-9AE7-454F-BA51-8BF22964FA93.png
 
Kesi inahusiana na nini?mbona hamuielezei

Ova
Hukumu hiyo iliyotolewa na Jaji Augustine Shangwa Februari 18, 2016, iliamuru Babu Tale na ndugu yake Idd Taletale kumlipa fidia ya Sh250 milioni, Mhadhiri wa Dini ya Kiislamu, Sheikh Hashim Mbonde kwa makosa ya kutumia mahubiri yake kibiashara bila ridhaa yake.
 
Back
Top Bottom