Asilimia 90 ya ngano inatoka nje, kwahiyo tunakulaga chapati za Urusi, wananunua wanapaki wanatuuzia

mwanamabadiliko

JF-Expert Member
Oct 30, 2010
843
1,365
Hivi Tanzania hatuwezi kulima ngano, maana tunanunua ngano nyingi sana nje, hizo feza zingebakia hapa.

Ardhi ipo ya kutosha ni. Serikali tu kuweka mipango na kuwawezesha watu. Hizi pesa anazotumia bakharesa kununua ngano Urusi zingerudi kwa watanzania na nchi ingepiga hatua, nimeona watanzania wengi sana hawajaamini kuwa ngano karibu yote inayotumika Tanzania tunaagiza nje.

Pia serikali imetenga ardhi kubwa na ambayo ni potential kwa kilimo Kama hifadhi au pori , serikali ibadili baadhi ya maeneo haya Ila watu wakalime, unahifadhi Nini watu hawana pesa na Wana njaa, serikali ifanye kitu. Mabeberu hayataki tulime hayo maeneo Ili tuendelee kuagiza ngano kwao
 
... hiyo ni ngao; imeripotiwa pia kwamba mahitaji ya mafuta ya kula kwa mwaka ni tani 700,000 ambapo uzalishaji wa ndani ni tani 30,000 wakati tani 670,000 zikiagizwa toka nje! Bado sukari kila mara ni uhaba! Aibu kwa CCM waliolifikisha taifa hapa! Wao muda wote wanawaza uchaguzi na wizi wa kura; mengine yote hadaa.
 
Taifa la watu legelege wanaopenda mteremko kuanzia wanaume mpaka wanawake, kila utapeli ukizuka lazima waibiwe, kila kamari ikija maelfu wanaingia huko, kila umbeya ukizuka Taifa zima wanaujadili.......Leo chief unataka tuzalishe ngano? tuendelee kucheza baikoko tu na Singeli ndio fani yetu hiyo tukomae itatutoa..
 
Enzi ya Mwalimu aliwaleta wazungu kutoka Canada wakatuanzishia mashamba ya NGANO kule Hanang tukawa tunajitosheleza kwa ngano na kupika mikate ya SIHA!!! Ilikuwaje mpaka yale mashamba ya BASUTO yakafa?
Inakuwaje nchi inapiga hatua kwenda mbele ,halafu anakuja mtawala mwingine nchi inarudi nyuma? Lazima kuna kitu tunafanya kama nchi ambacho hakiko sahihi; ni kitu gani hicho?
 
Hivi Tanzania hatuwezi kulima ngano, maana tunanunua ngano nyingi sana nje, hizo feza zingebakia hapa.

Ardhi ipo ya kutosha ni. Serikali tu kuweka mipango na kuwawezesha watu. Hizi pesa anazotumia bakharesa kununua ngano Urusi zingerudi kwa watanzania na nchi ingepiga hatua, nimeona watanzania wengi sana hawajaamini kuwa ngano karibu yote inayotumika Tanzania tunaagiza nje.

Pia serikali imetenga ardhi kubwa na ambayo ni potential kwa kilimo Kama hifadhi au pori , serikali ibadili baadhi ya maeneo haya Ila watu wakalime, unahifadhi Nini watu hawana pesa na Wana njaa, serikali ifanye kitu. Mabeberu hayataki tulime hayo maeneo Ili tuendelee kuagiza ngano kwao
Hatujawahi kufanikiwa kwenye chochote kama nchi. Hata Tanzanite muuzaji ni kenya 🤣🤣
 
Enzi ya Mwalimu aliwaleta wazungu kutoka Canada wakatuanzishia mashamba ya NGANO kule Hanang tukawa tunajitosheleza kwa ngano na kupika mikate ya SIHA!!! Ilikuwaje mpaka yale mashamba ya BASUTO yakafa?
Inakuwaje nchi inapiga hatua kwenda mbele ,halafu anakuja mtawala mwingine nchi inarudi nyuma? Lazima kuna kitu tunafanya kama nchi ambacho hakiko sahihi; ni kitu gani hicho?
... CCM wanapaswa kuwa na majibu! Hili lichama limeivuruga sana hii nchi kiuchumi kwa kiwango cha kutisha.
 
Wazee wa copy and paste now hatutaki gari below mwaka 2010. Ukiwauliza hivi kipato cha mtanzania kwa mwaka ni bei gani, wanajiuma uma. Je mna kiwanda cha magari wanajiuma uma tu.
Watu mnataka wanunue gari za miaka ya karibuni, halafu mmeweka mikodi mikubwa hivi wako serious?

Ngoja nikajidakie gari la kipanya
 
Sukari ya hapa nchini ni kidogo mno, hiyo nyingi unayokula wameagiza nje wanapack tu na kubandika majina yao.
... kwa taifa lenye maono; chama chenye dira kilimo kilitakiwa kipunguze tatizo la ajira kwa kiwango kikubwa mno! Bahati mbaya ndio hivyo tena; sera waliyobaki nayo ni kutawala milele. Kumbe hata maandazi na chapati tunazokula ni imported! Ha ha ha! Kwa mwendo huu kutoboa ni ndoto!

Hivi yale mabilioni yaliyowekezwa kwenye ununuzi wa ndege yangeelekezwa kwenye kilimo cha ngano, shairi, mafuta, na sukari inge-add value kiasi gani kwa nchi? Tushukuru vita vya Ukraine vimetufumbua macho - vitumbua vya mama ntilie ni imported products.
 
Wazee wa copy and paste now hatutaki gari below mwaka 2010. Ukiwauliza hivi kipato cha mtanzania kwa mwaka ni bei gani, wanajiuma uma. Je mna kiwanda cha magari wanajiuma uma tu.
Watu mnataka wanunue gari za miaka ya karibuni, halafu mmeweka mikodi mikubwa hivi wako serious?
... chama chakavu limechoka kila idara! Tusitegemee jipya toka huko; ni hadaa na ghilba tu maono na uwezo sifuri!
 
Hivi Tanzania hatuwezi kulima ngano, maana tunanunua ngano nyingi sana nje, hizo feza zingebakia hapa.

Ardhi ipo ya kutosha ni. Serikali tu kuweka mipango na kuwawezesha watu. Hizi pesa anazotumia bakharesa kununua ngano Urusi zingerudi kwa watanzania na nchi ingepiga hatua, nimeona watanzania wengi sana hawajaamini kuwa ngano karibu yote inayotumika Tanzania tunaagiza nje.

Pia serikali imetenga ardhi kubwa na ambayo ni potential kwa kilimo Kama hifadhi au pori , serikali ibadili baadhi ya maeneo haya Ila watu wakalime, unahifadhi Nini watu hawana pesa na Wana njaa, serikali ifanye kitu. Mabeberu hayataki tulime hayo maeneo Ili tuendelee kuagiza ngano kwao
Ccm mbele kwa mbele.
 
... kwa taifa lenye maono; chama chenye dira kilimo kilitakiwa kipunguze tatizo la ajira kwa kiwango kikubwa mno! Bahati mbaya ndio hivyo tena; sera ni kutawala milele. Kumbe hata maandazi na chapati tunazokula ni imported! Ha ha ha! Kwa mwendo huu kutoboa ni ndoto!

Hivi yale mabilioni yaliyowekezwa kwenye ununuzi wa ndege yangeelekezwa kwenye kilimo cha ngano, shairi, mafuta, na sukari inge-add value kiasi gani kwa nchi? Tushukuru vita vya Ukraine vimetufumbua macho - vitumbua vya mama ntilie ni imported products.
Kilimo nchi hii uwa ni sehemu ya kujipigia pesa kama enzi kilimo kwanza. Watu walipiga pesa na matokeo hakuna.
Hatuko serious kwenye kila kitu tunashika shika tu. We are jack of many trades, master of none.
Yani walau tungekuwa na jambo moja tu tulilofanikisha kweli kweli lakini hakuna
 
... kwa taifa lenye maono; chama chenye dira kilimo kilitakiwa kipunguze tatizo la ajira kwa kiwango kikubwa mno! Bahati mbaya ndio hivyo tena; sera waliyobaki nayo ni kutawala milele. Kumbe hata maandazi na chapati tunazokula ni imported! Ha ha ha! Kwa mwendo huu kutoboa ni ndoto!

Hivi yale mabilioni yaliyowekezwa kwenye ununuzi wa ndege yangeelekezwa kwenye kilimo cha ngano, shairi, mafuta, na sukari inge-add value kiasi gani kwa nchi? Tushukuru vita vya Ukraine vimetufumbua macho - vitumbua vya mama ntilie ni imported products.
Na kwa mdororo huu wa uchumi hizo ndege tutazipaki tu
 
Back
Top Bottom